NFRA? au bei yao ndogo?
tatizo la serikali hutalipwa leo wala kesho.utasubiri sana
Lakini ndiyo wana bei lau nzuri, hawa wenzengu na mimi wachuuzi wanataka super profit! Sku hizi NFRA hawacheleweshi saana, ndani ya mwezi unaweza kupata cheque yako, lakini jaribu kuongea na regionala manager kwanza uskilize kama wana funds. Sivyo ujaribu kucheki na jamaa wa kutoka Kenya.
Wadau habari za majukumu! naombeni mnisaidie mahali ambao lipo soko la uhakika la zao la mahindi Tanzania nisaidieni Nina magunia kama 500,na ikiwezekana nisaidieni taarifa mabali mbali toka huko mnakokaa Mimi Niko mkoa wa manyara wilaya ya mbulu.tafadhali sana katika hili na subiria mchango wenu wenye tija kwangu kama kuna mwenye taarifa tuwasiliane kwa namba hizi za simu 0787509377 au 0788693495.
Ndugu mimi ni mfanya biashara wa nafaka,kimsingi bei ya mahindi kwa mwaka huu ni hovyo na sifikiri kama itapanda,sababu mojawapo kubwa inayopelekea mahindi kutokupanda ni bei ya chini ya mchele,hivi sasa mchele upo hata wa 1000 kwa 1kg,nafikir wewe utakua shahidi kwa sehem nyingi za tz ipo dhana kwa muda mrefu kwamba ubwabwa ni chakula chakifahari ambacho kwa mwaka huu bei yake iko sawa na bei ya unga,hivyo kama unga/mahindi yatapanda consumer wata shift kwenye mchele,kifupi tafuta namna uuze mahindi yako,kwa dar 1kg ya mahindi imeporomoka kutoka 570 kwa 1kg mwezi wa kwanza hadi kufikia 490 kwa 1kg kwa sasa.
NFRA? au bei yao ndogo?
nilisoma gazeti recently kuna wakulima huko Ruvuma wanaidai NFRA hadi leo na hawa waliiuzia mahindi msimu uliopita, na serikali nayo ndo hio inajinasabu haina fedha.
wadau nawashukuruni hadi hapa tulipofikia,naendekea kukaribisha mawazo zaidi.
Kwasasa yameporomoka sana bei hivyo kama huna haraka na hiyo pesa ni bora ukatafuta dawa nzuri za vidonge(gesi) ama zile za pakti(gesi) ukayatibu vizuri ili uuze msimu wa mwezi wa saba au mwezi wa nane.
mkuu mombasa gunia ni ksh 3000.
jaribu kufuatilia