Soko la Mbagala sasa liko safi na linafikika kwa urahisi. Masoko machafu yote yabomolewe na kujengwa upya

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Mwaka jana kabla soko la Mbagala kuungua moto niliingia sokoni ili nipate mahitaji muhimu .
Lile soko lilikuwa chafu na wakati wa mvua linatoa harufu mbaya sana.

Njia za kuingilia na kutokea hazijulukani. Bidhaa ziko hovyohovyo. Huwezi kuingia mara mbili kama hujazoea uchafu.

Jana nilipita Mbagara nikaulizia SAMAKI nikaambiwa sasa hawapo nje tena mpaka ndani sokoni. Ashukuriwe Mungu kumbe tayari limeshajengwa na kukamilika. Nikaingia , kwa hakika linavutia sasa, hewa ya kutosha na mazingira yako safi kiasi.

Sasa masoko yote machafu hapa Dar es salaam yachomwe moto. Kipindupindu chanzo chake kikuu ni uchafu.

Tusioneane aibu aidha wamachinga watolewe kwa hiyari kupisha ujenzi kisha wale wa awali kupewa kipaumbele wakati wa kugawa vizimba.

Wakikataa watolewe kwa nguvu na wakati wa kugawa vizimba wasipewe kipaumbele.
 
picha
 
Tegeta pia wanajitaidi kwa usafi japo sio sana🔋
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…