Soko la Network Engineering Tanzania

Soko la Network Engineering Tanzania

Francesco lupenza

New Member
Joined
May 26, 2019
Posts
4
Reaction score
0
Wadau naomba ushauri juu ya soko (kwa upande wa ajira) mimi nasoma Bachelor of Computer Engineering, MUST, siko interested sana na coding.

Nafkiria kuspecialize na Network & System Administration kwenye suala la ajira iko vp hii? Na ni sector zipi zina uhitaji wa ao watu wa network?
 
Mimi sijui chochote kuhusu hayo mambo ila nimewiwa kukupongeza kwa kujitambua na kutaka ku specialize(kunobea) ktk kitu fulani.

Usiwaze kazi kama kweli utabobea na ukawa ujuzi wa uhakika basi kazi zitakutafuta.

Watu mnaosomea mambo ya computer na teknolojia zingine mkiwa mnasoma msiwaze soko la Tanzania tu. Jijengeni kitaaluma ili muwe na uwezo wa kushindana na watu wengine duniani. THINK GLOBALLY.
 
Kama muda unao usiache kujifunza programming.
 
kwanin boss,, naomba kueleweshwa vzuri
Kwanini uji limit katika kupata ujuzi?
Kama systems administrator utahitaji ku automate data aggregation processes.Ujuzi wa scripting languages utauhitaji hapa.Kuna systems admins wengi tu hawajui programming lakini ukitaka kujipanulia wigo wa ajira then programming itakubeba.
 
Nashukuru sana boss nmekupata
 
Wadau naomba ushauri juu ya soko (kwa upande wa ajira) mimi nasoma Bachelor of Computer Engineering, MUST, siko interested sana na coding.

Nafkiria kuspecialize na Network & System Administration kwenye suala la ajira iko vp hii? Na ni sector zipi zina uhitaji wa ao watu wa network?
Mimi kijana nimemaliza kidato cha nne nlikua naomba ushauri wenu nataka nianze kupiga diploma in INDUSTRIAL ENGINEERING
naomba kuuliza hii field ipo vizuri au ndo michosho
pia kwa ataeweza nishauri juu ya kozi hizi mbili ipi ipo vizuri kwa upande wa ajira saiv
ELECTRICAL AND ELECTRONICS au
COMPUTER ENGINEERING
 
Electrical and Electronics
 
Wadau naomba ushauri juu ya soko (kwa upande wa ajira) mimi nasoma Bachelor of Computer Engineering, MUST, siko interested sana na coding.

Nafkiria kuspecialize na Network & System Administration kwenye suala la ajira iko vp hii? Na ni sector zipi zina uhitaji wa ao watu wa network?
Kwa hiyo uliambiwa networking haina programming? Wewe sema unaikimbia programming sio "una specialize" !

Programming ni kama hesabu kwa wanafunzi wa chuo, hata kama unasoma socialogy lazima ukutane na hesabu.

Vivyo hivyo kwa programming, kama uko kwenye IT au computer related field JUA PROGRAMMING HAIKWEPEKI.

Nikupe huu mfano, unataka kubase kwenye networking, je umewahi kujiuliza cyber attacks zinafanywa kwa kutumia nini kama si programming? Je utaweza kuzuiaje attacks kama hujui programming?

Au nyie ndio wale watu mnaojiita IT alafu mnatengeneza mifumo mibovu na hovyo yenye viwango duni?

Narudia tena kama uko kwenye field za IT programming haikwepeki. Kama ukiona hipendi programming nenda kasome socialogy maana utakuja fungwa kwa kutia hasara kampuni ya watu au serikali.

NB: its not too late, sit down and ask yourself unakwama wapi kwenye coding? Anza leo kuipenda programming otherwise utaisoma namba hapo badae.
 
Back
Top Bottom