Soko la Wachezaji Uingereza kufungwa Mapema

Soko la Wachezaji Uingereza kufungwa Mapema

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
EPL.png


Klabu za Ligi ya Premia zimepiga kura na kuidhinisha soko la kuhama wachezaji lifungwe kabla ya msimu kuanza mwaka ujao.

Mameneja walikuwa wamelalamika kwamba nafasi ya wachezaji kuhama ligi ikiendelea hutatiza klabu na maandalizi.

Kuanzia msimu ujao, dirisha la kuhama wachezaji litafungwa saa 17:00 BST Alhamisi itakayokuwepo kabla ya ligi mpya kuanza.

Kura hiyo haikuwa kwa kauli moja na klabu bado zitaweza kuendelea kuuza wachezaji hadi mwisho wa dirisha la kawaida la kuhama wachezaji.

Dirisha la kuhama wachezaji kote Ulaya huendelea kuwa wazi hadi tarehe 31 Agosti.

Hatua ya klabu hiyo za Ligi ya Premia ina maana kwamba ingawa klabu zitaweza kuendelea kuuza wachezaji hadi siku hiyo, ununuzi utafikia kikomo tarehe 9 Agosti msimu wa 2018-19.

Klabu za ligi nyingine za Ulaya bado zitaweza kununua na kuuza wachezaji hadi 31 Agosti.

Uhamisho wa wachezaji katika ligi nyingine ndogo za England na Wales ((Championship, League One na League Two) hautaathiriwa.

Wasimamizi wa ligi hizo wamedokeza kwamba huenda wakafuata njia hiyo ya Ligi ya Premia lakini wanahitaji mashauriano zaidi.

Klabu za Ligi ya Premia zilizounga mkono mabadiliko hayo bado hazijabainika kabisa, ingawa inaaminikakwamba zilikuwa 14 kati ya 20.

Mabadiliko hayo hata hivyo hayatafupisha muda wa klabu kununua wachezaji kwani soko litafunguliwa mapema na litakuwa wazi muda wa wiki 12, kuambatana na sheria za Fifa.
 
Kwa kuwa bado mchezaji anaweza kuondoka hata dirisha la usajili la premia likifungwa bado timu zitaendelea kuathirika.Mwisho wa kununua lakini sio mwisho wa kuuza.

Hatua hii inazuia fujo za usajili within premier league teams wakati ligi inaendelea lakini haizuii timu kuondokewa na wachezaji kwenda ligi zingine.

Ingefaa kwa ligi zote kubwa dirisha lifungwe kabla ligi itakayowahi kuanza haijaanza
 
Back
Top Bottom