Mimi nadhani kulingana na idadi ya wati inavyozidi kuongezeka na changamoto zinavyozidi kuongezeka ndivyo mahitaji pia yanavyozidi kuongezeka. Ukisikia watu wenye matatizo ya kisheria yanazidi idadi ya wahitimu kila mwaka. Hapa Tanzania tuna mahitaji mengi yanayohitaji wanasheria kuliko idadi ya watu waliopo. Hivyo, kama ni changamoto ya ajira hiyo ni kwa kila fani siyo sheria tu. Na hata kama ajira hi haba, haina maana kuwa ukihitimu na kuwa mwanasheria basi utakosa ajira.
Chukulia katika eneo la biashara kuna wanaofirisika na kuna wanaokuwa matajiri. Katika maisha ya ndoa, kuna wale ambao ndoa zao zinavunjika na kuna wanaoa au kuolewa. Hivyo, kwa mtazamo wangu hakuna mtu ambaye yuko kwenye loss. Kinachotakiwa ni competency. Mwanasheria mzuri na mwadilifu hata kama kuna tatizo la ajira yeye anakuwa marketable. Si ulishaona mtu anauza duka na bidhaa zote kwa vile anadhani hakuna wateja na kwenda kufungua sehemu nyingine na wakati huohuo mtu mwingine anayenunua duka na bidhaa hizo yeye anapata wateja? Hivi ndivyo life ilivyo. Kama una kipaji cha kuwa mwanasheria - unapenda kuwa mwanasheria na unaweza kuwa mwanasheria mzuri, piga moyo konde, the future will unfold for you!