Caren
JF-Expert Member
- Feb 12, 2010
- 278
- 91
jamani naomba kuuliza nataka nikasome sheria najua soko lake gumu lakini vitu gani vya ziada ambavyo vinaweza kunisaidia kupata ajira haraka(kufikiriwa pale nitakapoomba kazi),mfano nilisikia watu wanao soma international relations ni vizuri kujua ligha za kigeni kama french,arab.madiodo gani yanahitajika kwenye sheria?
Fayamario,
asikudanganye mtu hakuna wakati soko la ajira ya wanasheria litapungua! idadi ya wanasheria tulio nao ni ndogo mno! we piga shule uwe wakili. For your information upto August 2011 nchi hii ina mawakili 2300 tu wanaohudumia watu karibu milioni 40. Tatizo lililopo ni kuwa wanasheria wengi wako mjni hasa dar, Mwanza na Arusha. Inategemea ni kwa kiasi gani wanasheria wanabadilika na kuamua kwa makusudi kwenda pale huduma yao inapohitajika zaidi.
Nitakupa mifano:
1. Mkoa wa Mtwara una High Court Zone na majaji wawili lakini wakili ni mmoja tu. Hapa panahitaji mawakili zaidi ya kumi (at least). Demand ipo.
2. Mkoa wa Mara una kesi za mauaji za kutosha na border post ya Sirari. Hapa pana hitaji mawakili zaidi ya 15 lakini yupo mmoja. Migori iliyopo 5 km from Sirari on the Kenyan side wako advocates 15 na hawawezi kuhandle cases.
3. Mkoa wa Tanga una High Court Zone lakini una advocates 5. Mombasa which is only 3 hours from tanga ina advocates 70 na hawatoshi. (Mind you hakuna tofauti san ya cultures kati ya Tanga na Mombasa).
4. Tabora ina High Court Zone inayohudumia mikoa ya Tabora, Kigoma. Kuna kesi za mauaji zaidi ya 3000 hazijaanza kusikilizwa kwa kukosa mawakili. Mawakili wako 5. Wako busy kweli.
5. Lindi, Manyara hazina mawakili,
6. Mikoa ifuatayo ina mawakili (roughly) kama ilivyoainishwa Singida (4), Pwani (2), Dodoma (10), Mbeya (5).
Hapo nimetaja mawakili. Sikuongea suala kwamba wilaya 80 Tanzania Bara hazina mahakimu wakazi hata mmoja (ili uwe RM unahutaji LLB). Normally kila RM's court inatakiwa iwe na at least 3.
Kwa hiyo demand ipo ya kutosha na soko lipo.
what we need to do as lawyers:-
1. Get out of mentality kuwa ili uwe sucessfull lazima uwe katika miji mikubwa
2. Forget the dreams za kutaka kuajiriwa na kuembrace ujasiriamali
3. Seek how you can develope the passion to help poor people and middle income earners who will glady be your clients forever
4. MOST IMPORTANTLY - create the demand for legal services. Charge reasonably. let people know that you are a person they can turn to. I can assure you that many people fear lawyers n they dont come to them for assistance.
Jiulize watanzania wangapi wasomi kabisa wa digrii hapa mjini including lawyers wanasaini mikataba ya upangaji wa nyumba au ya ajira bila kushirikisha wanasheria. Ukipata hiyo idadi utaelewa demand ni kubwa na supply for the next ten years haitatosha.