Sokoni Leo ni App iliyotengenezwa kwa ajili ya simu za Android, maalum kwa kutoa taarifa muhimu kuhusu mazao yanayopatikana sokoni. Utaweza kujua bei ya mazao mbalimbali yaliyopo sokoni rejareja au jumla.
Hii itakurahisishia wewe mteja au hata mkulima kujua bei ya mazao ilivyo sokoni. Kwa sasa ni soko la kariakoo tu ndilo lililounganishwa hata hivyo tunatarajia kuongeza masoko zaidi baadae. Bei za mazao yanayoonekana katika program hii ni bei halisi kama zinavyoonekana kwenye tovuti ya Soko la Kariakoo (http://www.kariakoo.or.tz/sw/).