Sokwe muigizaji ameingiza $Bill 2.5 kupitia filamu ambazo ameigiza

Sokwe muigizaji ameingiza $Bill 2.5 kupitia filamu ambazo ameigiza

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Crystal ni sokwe jike wa aina ya "Tufted Capuchin" mwenye umri wa miaka 31, aliyezaliwa California mwaka wa 1994. Amekuwa mwigizaji mahiri wa Hollywood tangu mwaka wa 1997 na ameonekana kwenye zaidi ya filamu na vipindi vya televisheni 30.

Ukurasa wake wa IMDB una orodha ya kazi zake zenye mafanikio makubwa zaidi inawezekana kuliko hata kwa baadhi ya waigizaji wengine ambao unawafahamu. Safari yake ya uigizaji ilianza akiwa mtoto sokwe katika filamu ya Disney ya mwaka wa 1997 inayoitwa "George of the Jungle" filamu ambayo ilifanya vizuri sana. Muongo mmoja baadaye, alipata nafasi iliyompa umaarufu mkubwa kama Dexter (sokwe mkorofi) katika filamu ya "Night at the Museum" akishirikiana na Ben Stiller.

Na jambo la kuvutia zaidi ni kwamba ushiriki wake katika filamu zote tatu za mfululizo ambazo aliigiza alipokelewa vizuri sana. Mwaka 2011 aliigiza kama sokwe anayejihusisha na biashara ya dawa za kulevya katika filamu ya "The Hangover Part II", filamu hiyo iliyiingiza dola milioni 177.8 katika wiki yake ya kwanza. Ikiweke rekodi ya kuwa filamu yenye kiwango cha juu zaidi cha mapato ya wiki ya tu kwanza katika historia ya filamu za vichekesho.

wakati huo muigizaji Ken Jeong, aliyeigiza naye, alieleza waziwazi: "Yeye si sokwe tu, bali ni mwigizaji. Na huenda akawa ndiye mwigizaji bora zaidi ambaye nimewahi kufanya naye kazi." Tangu wakati huo, ameonekana katika filamu na vipindi kama "We Bought a Zoo", "Zookeeper" "Community", na filamu ya Steven Spielberg ya mwaka wa 2022, "The Fabelmans".

Katika filamu tano tu kati ya hizo, amechangia katika mapato ya jumla ya zaidi ya dola bilioni 2.5 katika ofisi za mauzo ya tiketi (box office). Crystal anaishi na mkufunzi na mmiliki wake Tom Gunderson huko Los Angeles, akishiriki makazi na mbwa, farasi, paka, na sokwe mwenzake wa aina ya "capuchin" anayeitwa Squirt.
SaveClip.App_821388685_18102486983575830_6210663232140976750_n.jpg

SaveClip.App_821468610_18102486980575830_3707235260609637174_n.jpg
SaveClip.App_819219128_18102487049575830_3002960594153894867_n.jpg
SaveClip.App_821281917_18102487040575830_2260974508694725700_n.jpg
SaveClip.App_818977121_18102487091575830_6723568333976851685_n.jpg
SaveClip.App_819193729_18102487052575830_1202218232564154616_n.jpg
SaveClip.App_821388685_18102486983575830_6210663232140976750_n.jpg
 

Attachments

  • SaveClip.App_819097511_18102487067575830_8007721908740037428_n (1).jpg
    SaveClip.App_819097511_18102487067575830_8007721908740037428_n (1).jpg
    213.2 KB · Views: 12
  • SaveClip.App_819097511_18102487067575830_8007721908740037428_n.jpg
    SaveClip.App_819097511_18102487067575830_8007721908740037428_n.jpg
    213.2 KB · Views: 10
duh... Angekuwa bongo angekuwa na chawa wengi sana....
 
Sokwe,nyani,tumbili,kima hua wanawachanganya watu hasa wenye kutafsili tokea kimombo tu kiswahili.Unaweza kutwa habari iliyoandikwa kwa kimombo inamuhusu sokwe kwenye tafsiri ya kiswahili unakuta ni tumbili au nyani au unaweza pewa picha ya tumbili na maelezo yakawa ya sokwe
 
Back
Top Bottom