Sola kwa Sasa lipo ujerumani

Sola kwa Sasa lipo ujerumani

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
8,581
Reaction score
15,618
Miaka ya 1980-90 mwishoni Mpira nzuri na wakuvutia ulikuwa ukichezwa nchini Italia. Ligi ya Italia Serie A likuwa ndio Bora kabisa duniani. Wachezaji wote wazuri na Bora toka mataifa mengine ya ulaya na America ya kusini pamoja na Africa walipenda kucheza Mpira nchini italia. Ligi yao ilisheheni wachezaji wakali. Diego Maradona, Ruud Gulit, Marco Van Basten, Jean Pierre Papin, George Weah, baadae wakaja kina Zanetti, Edger Davis Zidane Zizou, Zamarano na wakali kibao.

Miaka ya 2000 Mpira ukahamia Spain. Zama za kina Figo, dilima, gaucho, Redondo,Rivaldo, baadae wakaja wakali kina Messi na Cristiano Ronaldo. Zama zimepita. Sasa ni zamu ya Ujerumani. Mpira unaochezwa na vilabu vya kijerumani ni Mpira wa viwango vya juu Sana. Japo wachezaji wanaocheza wengi so wakutoka nje lakini mziki wa Bayern Munich, Monchengladbach, BvB, na Leipzig wote tunaujua. Baadae ya italia, na Spain Sasa ni zamu ya Ujerumani.

Wale wanazi wa epl mapovu ruksa. Japo najua kuwa Ligi yenu ni maarufu. Cristiano Ronaldo ndio mchezaji Bora aliyepata kuichezea Ligi kuu ya uingereza. Hao wengine wote ni everege players.
 
Nikikuelewa ntakuja kukoment, nimeshiba magimbi saivi.
 
Ahaa,Bundas kule ukiweka mguu unakuta kuna mguu mwingine tayari.
 
Kwakweli Mana Bunde kule kunapigwa boli hatari Sana mwendo wa 4
 
Bundasliga hawaeleweki Bayern ndio wana consistency!

Hao wengine BVB 09 ilikuwa zamani sasa bado hawaeleweki kabisa.

RB Leipzig ndio kule kule.

Bayern Leverkusen ndio wale wale.

Bayern Monchenglandbach ndio wale wale
 
Miaka ya 2000 Mpira ukahamia Spain. Zama za kina Figo, dilima, gaucho, Redondo,Rivaldo, baadae wakaja wakali kina Messi na Cristiano Ronaldo. Zama zimepita. Sasa ni zamu ya Ujerumani.
nadhani kuna sababu nyenginezo ndio zilizidi kushajihisha wachezaji hao uliowataja na wengineo kupendelea zaidi kucheza Spain miaka tajwa hapo juu kama vile jeografia ya nchi ya spain, maslahi binafsi ya wachezaji, aina ya soka linalochezwa spain pamoja na historia kubwa za timu hususani kwa real madrid na barcelona.

ubora wa timu tunaupima kwa kutumia kigezo gani na ubora wa ligi tunaupima kwa kigezo gani?
kwa sababu miaka ya 2000 kama ulivyosema hapo juu klabu ya real madrid walikuja na sera ya usajili wa galacticos, lakini cha kushangaza au kustaajabisha madrid iliosheheni vipaji vya wachezaji kwa kila idara walifanikiwa kubeba ubingwa wa ulaya mara moja tu (2001/2002 dhidi ya leverkusen) na ikawachukua tena miaka 13 kubeba ubingwa mwengine wa Ulaya(walikuwepo zidane, figo, delima, beckham, guti, raul, casillass, helguera, salgado, carlos n.k)

barcelona yenye wachezaji nyota kwa miaka tofauti iliwachukua miaka 14 kubeba tena ubingwa wao wa ulaya baada ya ule waliobeba mwaka 1991/1992(rivaldo, de lima, deboer, guardiola, kluivert, overmass, edgar davis kwa mkopo n.k )

ni kipi kinachotangulia kwanza kati ya ligi bora na timu bora?
  • kwa sababu unaweza kuwa na timu bora inayotokea kwenye ligi yenye ubora wa kawaida mfano psg ya miaka miwili iliopita na bayern munich ya miaka hii miwili na ukawatingisha vigogo wengineo (kwa tafsiri ya haraka naamini hakuna ulazima wa kuwa na ligi bora ili utoe timu bora)
  • unaweza kuwa na ligi bora yenye kutoa timu za kawaida, kwa mfano ligi ya uingereza miaka miwili nyuma kabla ya kuibuka kwa liverpool walikuwa wanafanya vibaya sana kwenye michuano ya ulaya licha ya ligi yao kuwa ni bora

unaweza kuwa na ligi bora na timu bora kwa wakati mmoja
  • rejea ubora wa timu za uingereza kuanzia msimu wa 2005 hadi 2008 (timu za kiengereza zilikuwa zinafika mbali sana kwenye michuano ya ulaya)........liverpool aliwahi kucheza na AC Milan huku akiwa na matokeo mabaya kwenye ligi kuu, timu za uingereza kwa nyakati tofauti zilitoana nusu fainali na robo fainali zaidi ya mara moja
  • rejea ubora wa timu za spain kuanzia msimu wa 2010 hadi 2017 (timu za spain zilikuwa zinafika mbali sana kwenye michuano ya ulaya)......kwa mfano madrid alimfunga atletico madrid mara mbili kwenye fainali na barcelona alishamtoa madrid nusu fainali.
je timu za bundesliga zipo kwenye kundi gani hapo?
kiupande wangu mimi ungeliniambia bundesliga timu zao zipo vizuri sana kwenye game managements pamoja na ufundi wa walimu basi ningelikubali kwa haraka sana
 
Kweli wewe mtu wa mpira...
 
Miaka ya 1980-90 mwishoni Mpira nzuri na wakuvutia ulikuwa ukichezwa nchini Italia. Ligi ya Italia Serie A likuwa ndio Bora kabisa duniani. Wachezaji wote wazuri na Bora toka mataifa mengine ya ulaya na America ya kusini pamoja na Africa walipenda kucheza Mpira nchini italia. Ligi yao ilisheheni wachezaji wakali. Diego Maradona, Ruud Gulit, Marco Van Basten, Jean Pierre Papin, George Weah, baadae wakaja kina Zanetti, Edger Davis Zidane Zizou, Zamarano na wakali kibao.

Miaka ya 2000 Mpira ukahamia Spain. Zama za kina Figo, dilima, gaucho, Redondo,Rivaldo, baadae wakaja wakali kina Messi na Cristiano Ronaldo. Zama zimepita. Sasa ni zamu ya Ujerumani. Mpira unaochezwa na vilabu vya kijerumani ni Mpira wa viwango vya juu Sana. Japo wachezaji wanaocheza wengi so wakutoka nje lakini mziki wa Bayern Munich, Monchengladbach, BvB, na Leipzig wote tunaujua. Baadae ya italia, na Spain Sasa ni zamu ya Ujerumani.

Wale wanazi wa epl mapovu ruksa. Japo najua kuwa Ligi yenu ni maarufu. Cristiano Ronaldo ndio mchezaji Bora aliyepata kuichezea Ligi kuu ya uingereza. Hao wengine wote ni everege players.
Umemkumbuka Ivan Zamorano umemuacha Marcelo Salas kweli?!
 
nadhani kuna sababu nyenginezo ndio zilizidi kushajihisha wachezaji hao uliowataja na wengineo kupendelea zaidi kucheza Spain miaka tajwa hapo juu kama vile jeografia ya nchi ya spain, maslahi binafsi ya wachezaji, aina ya soka linalochezwa spain pamoja na historia kubwa za timu hususani kwa real madrid na barcelona.

ubora wa timu tunaupima kwa kutumia kigezo gani na ubora wa ligi tunaupima kwa kigezo gani?
kwa sababu miaka ya 2000 kama ulivyosema hapo juu klabu ya real madrid walikuja na sera ya usajili wa galacticos, lakini cha kushangaza au kustaajabisha madrid iliosheheni vipaji vya wachezaji kwa kila idara walifanikiwa kubeba ubingwa wa ulaya mara moja tu (2001/2002 dhidi ya leverkusen) na ikawachukua tena miaka 13 kubeba ubingwa mwengine wa Ulaya(walikuwepo zidane, figo, delima, beckham, guti, raul, casillass, helguera, salgado, carlos n.k)

barcelona yenye wachezaji nyota kwa miaka tofauti iliwachukua miaka 14 kubeba tena ubingwa wao wa ulaya baada ya ule waliobeba mwaka 1991/1992(rivaldo, de lima, deboer, guardiola, kluivert, overmass, edgar davis kwa mkopo n.k )

ni kipi kinachotangulia kwanza kati ya ligi bora na timu bora?
  • kwa sababu unaweza kuwa na timu bora inayotokea kwenye ligi yenye ubora wa kawaida mfano psg ya miaka miwili iliopita na bayern munich ya miaka hii miwili na ukawatingisha vigogo wengineo (kwa tafsiri ya haraka naamini hakuna ulazima wa kuwa na ligi bora ili utoe timu bora)
  • unaweza kuwa na ligi bora yenye kutoa timu za kawaida, kwa mfano ligi ya uingereza miaka miwili nyuma kabla ya kuibuka kwa liverpool walikuwa wanafanya vibaya sana kwenye michuano ya ulaya licha ya ligi yao kuwa ni bora

unaweza kuwa na ligi bora na timu bora kwa wakati mmoja
  • rejea ubora wa timu za uingereza kuanzia msimu wa 2005 hadi 2008 (timu za kiengereza zilikuwa zinafika mbali sana kwenye michuano ya ulaya)........liverpool aliwahi kucheza na AC Milan huku akiwa na matokeo mabaya kwenye ligi kuu, timu za uingereza kwa nyakati tofauti zilitoana nusu fainali na robo fainali zaidi ya mara moja
  • rejea ubora wa timu za spain kuanzia msimu wa 2010 hadi 2017 (timu za spain zilikuwa zinafika mbali sana kwenye michuano ya ulaya)......kwa mfano madrid alimfunga atletico madrid mara mbili kwenye fainali na barcelona alishamtoa madrid nusu fainali.
je timu za bundesliga zipo kwenye kundi gani hapo?
kiupande wangu mimi ungeliniambia bundesliga timu zao zipo vizuri sana kwenye game managements pamoja na ufundi wa walimu basi ningelikubali kwa haraka sana
Ubora wa timu za England nakataa ukisema 2005 mpaka 2008 kwenye michuano ya Ulaya nakataa kwasababu.

2005 Liverpool alifika final akabeba.
2006 Arsenal alifika final akafungwa.
2007 Liverpool alifika final akafungwa
2008 Man U na Chelsea walifika final.
2009 Man U alifika fainal akafungwa.
2010 HAPA ndio walichemsha kwakuwa Man U pekee ndio ilifika robo final.
2011 Man U alifika final akafungwa.
2012 Chelsea alifika final akashinda.
 
Back
Top Bottom