Solar Power

Status
Not open for further replies.

georgebest

Member
Joined
Feb 28, 2012
Posts
23
Reaction score
6
Habari zenu wote,
Naombeni msaada wenu mara moja. Nilitaka kununua solar panel ya nguvu ya watts 100 na nyingine yenye nguvu ya watts 1000 (kW 1) ya kuweka kwenye nyumba. Kwahiyo nilitaka kujua inaweza kua gharama gani ile ya watts 100 na gharama gani kuweka ile yenye nguvu ya watts 1000w? Sababu nimewatumia email kampuni zote kubwa kama rex, helvetic, ensol etc na hawajanijibu so kama kuna mtu anajua bei zao naomba msaada wenu.
Nawashukuru tayari sasa kwa msaada wenu.
 
Wasiliana na Chloride Exide watakusaidia wako Millenium Business Park, Shekilango - Ubungo..
 
Wasiliana na Chloride Exide watakusaidia wako Millenium Business Park, Shekilango - Ubungo..

Hii ndio shida kwa sasa siko nyumbani tanzania, ndio mana niliwatumia emails lakini hizi kampuni zetu sizielewi kabisa kwanini wanaweka email zao kama hawajibu.
Asante hivyo hivyo kwa msaada ndugu.
 
Hii ndio shida kwa sasa siko nyumbani tanzania, ndio mana niliwatumia emails lakini hizi kampuni zetu sizielewi kabisa kwanini wanaweka email zao kama hawajibu.
Asante hivyo hivyo kwa msaada ndugu.

Nitakusaidia kupata email ya hawa jamaa, uwe na amani.
 
Mkuu nyumba unayotaka kuweka solar iko mkoa/wilaya or kijiji gani? iko umbali gani kutoka kwenye umeme wa tanesco? unataka kutumia hiyo solar kwa vitu gani?
Ukinijibu haya maswali ndo nitajua nikushauri nini based on my experience!
 
Mkuu na mimi naomba nidandie. Nina nyumba iko Dar, bado sijaweka umeme nataka kuachana na Tanesco niweke angalau panels jumla 400-500 W. Naomba ushauri kuhusu experience yako. Ninaweza kuagiza hizo panels kutoka nje. Je batteries zinapatikana Tanzania kwa kiasi gani, na ni batteries ngapi kwa kiasi hicho cha panels?
 
Nina nyumba kimara,Tanesco walinisumbua saana,nikaamua kuweka panel ya 100W,na battery ya N95,nawasha taa 7,nachaji simu,natumia TV ya solar for 4 hrs a day,its quite effective and cheap!!
 
Naona mkuu majany ametoa experience yake hapa. So all in all inategemea na idadi ya vifaa unavyotaka kutumia. Huna hapa ya kuagiza toka nje, vyote vinapatikana hapa hapa TZ
 
Naona mkuu majany ametoa experience yake hapa. So all in all inategemea na idadi ya vifaa unavyotaka kutumia. Huna hapa ya kuagiza toka nje, vyote vinapatikana hapa hapa TZ

Tena nilianzia kwa kwenda kwa hawa suppliers wenye majina,bei walizonipa nikaogopa,kwa sababu budget yangu haikua jubwa kiivyo,ukizingatia nilikua ndio nimetoka kwenye ujenzi.Nikaenda kariakoo,pale kamata,kuna maduka meengi ya solar,Nikampata fundi mmoja mzoefu ambaye alishamfanyia jirani yangu...nilivipata kwa bei reasonable sana,tena wanakupa na 'PANEL GUARANTEE ya 5 years'.....lakini nakushauri ununue 'dry BATTERIES'..YAAN ZILE AMBAZO HAZITUMII MAJI.....Mgao nausikiaga tu mie.....IN FUTURE NATAKA KUFIKA MPAKA WATT 700,au 1KW,ambayo itafanya vitu vingi zaidi!!!!
 
Mkuu nyumba unayotaka kuweka solar iko mkoa/wilaya or kijiji gani? iko umbali gani kutoka kwenye umeme wa tanesco? unataka kutumia hiyo solar kwa vitu gani?
Ukinijibu haya maswali ndo nitajua nikushauri nini based on my experience!
Nyumba iko tabata dar, sitaki tanesco ndio mana nataka kuweka solar. Nimeshapigiwa hesabu na fundi wa solar na kaniambia nahitaji betri 4 za 12v kwa 100Ah na panels ya watts 1000. Kaniambia kua nikiwaambia hivi kampuni za solar wataniambia gharama zote mpaka napata umeme. Sasa nataka kujua gharama zikoje.
 
Nina nyumba kimara,Tanesco walinisumbua saana,nikaamua kuweka panel ya 100W,na battery ya N95,nawasha taa 7,nachaji simu,natumia TV ya solar for 4 hrs a day,its quite effective and cheap!!

Ah ok, na ulilipa bei gani?
 
Mhh, huyo fundi wako nina mashaka naye, betre 4 zichajiwe na panel ya watts 1000? sijui ni betri za N ngapi lakini kwa uzoefu wangu hiyo panel itaelemewa na matokeo yake zitakuwa hazijai. Mkuu majany uzoefu wako ukoje kuhusu hili?
 
Ah ok, na ulilipa bei gani?

System yangu kama nilivyoandika,ilikua ndogo,comparatively na unayoitaka,kwa sababu,panel ya 100w,ni TZS180,000,battery(N 95) ni TZS 345,000,Charger controller ni TZS 120,000,Inverter yake ni TZS 140,000.Jumlisha kama tzs 400,000 YA WIRES PAMOJA NA GHARAMA ZA FUNDI.Mchezo ukaisha...Though nilinunua na Tv ndogo ya solar kwa 350,000!!!
 
Ok Asante sana ndugu. Kwahiyo bira tv ni mln 1.2Tsh mtandao mdogo, nikifanya mara 10 ule mtandao mkubwa wa watts 1000 inaweza kua mln. 12TZs. Sio mbaya kwa miaka 25.
 
Si sawa kwani sijaona pannel ya watts 1,000. Kwa mahesabu ya haraka haraka utatakiwa pannel mbili za 110 watts na bettries 2 za 200Ah. Kwa kujua gharama na kila kitu kama charge regulator n.k waweza piga simu Zara Solar 0784299500 hawa wanauza vitu vyao vya jinioni na kwa bei nafuu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…