PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
'Mitatu' ni minini? Yaani kuishi kwangu kote huku Uskuduswazi umenitoa kapa. Halafu tulishakubaliana kuwa misemo mipya ya kiswahili isiwe inaanzia huko kwenu ushuani. Hamkawii kuja na misemo ya pizza nyie.Hilo swali anaweza kuuliza mtu ambaye hajawahi kwenda uwanjani.
Kilichotokea hakiwezi kuhusishwa na uongozi wa Club bali lawama zinaelekezwa kwa security team iliyokuwa getini.
Ni jambo ambalo limezoeleka mapolisi kuchukua hongo na kuruhusu watu wapite.
Hata mimi nimewahi kupita bila N-card.
Ilikuwa nimechelewa mechi nafika getini tayari mechi ishaanza.
N-Card yangu ilikuwa na tiketi nipo kwenye foleni natoa N-Card nampa jamaa aipanchi akaipanchi lakini kwa ghafla zikasikika kelele za mashabiki waliopo uwanjani wakiwa wanashangilia.
Kile kitu kilifanya watu waliopo nyuma kwenye foleni ya kupanchi tiketi wakawa wanatoka kwenye foleni wanakuja mbele kutaka awe wa kwanza kupanchi tiketi.
Kila mtu akawa na usongo wa kutaka kuingia ndani baada ya kupagawa na zile kelele
Maafisa wakaamua kusitisha zoezi la kupanchi ili kutuliza watu wakae kwenye mstari wafuate utaratibu. Baada ya watu kutulia mi nikawa nataka sasa nipite nikashangaa jamaa ananiambia lete N-Card.
Nikamjibu "mbona tayari umeipanchi?" wala hakunielewa akaniona mzugaji nataka kufanya uhuni, mchizi ndio kwanza akaniweka pembeni.
Basi namimi sikutaka makelele nikasogea pembeni nikawa nanunua haraka haraka tiketi kupitia simu.
Kwa bahati mbaya napo tiketi ikagoma kununulika kwasababu kwa mujibu wa system ilionekana tayari N-Card ina tiketi.
Nikafika kwa yule jamaa anayepanchi nikajaribu kumuoneshea hiyo meseji hata hakunielewa.
Pembeni kulikuwa kuna mwela mmoja kumbe alikuwa ameliona tukio lote tangu mwanzo. Akaniambia mi nimekuona ulivyompa tiketi na nimemuona alivyopanchi hiyo Card.
Nikasema kama ndio hivyo basi ongea naye, akasema hiyo haitawezekana kwasababu hawaruhusiwi.
Nikajiongeza nikamuambia mi hapa nimebakiwa na mitatu tu (wakati huo kiingilio ni 5,000)
Yule mwela akasema weka hiyo mitatu mfukoni, huku yeye akijidai anawapanga watu kama hakuna mawasiliano ya mimi na yeye.
Nikachukua ile mitatu nikatoa buku ikawa buku mbili nikaitia kwenye mfuko wake afu nikamstua kuwa tayari.
Basi fasta fasta bila hata kukagua nilichokiweka mfukoni akasema twende.
Akamuambia yule jamaa anayepanchi "oya mpitishe huyu jamaa kaishapanchi kitambo" Ndio nikapita.
Huku nyuma jamaa inaonekana baada ya kuingiza mkono mfukoni akakuta buku 2 atakuwa alimaindi.