Lukonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 1,469
- 2,086
Habari Watanzania,
Baada ya kusoma na kusiliza hoja za waziri wa fedha mheshimiwa Dr. Mwigulu Lameck Nchemba, naona kama hajaelewa msingi wa manung'uniko au kelele anazozisikia. Naomba kumweleza yafuatayo, manung'uniko ya wananchi si neno kodi au Tozo.
Manung'uniko ni jinsi haya yote yanavyofanyika. Kuna mtenda na mtendwa. Tuicheze ngoma wote.
Fuatana nami:
1: Tatizo la Watanzania si kuchangia au kutoa Tozo au kulipa kodi kwaajili ya maendel
Tatizo kuu ni kiasi cha tozo na mara ngapi tozo inatolewa kutoka kwa kipato cha mtu mmoja. Hii inakuja kufanya tozo vs kodi kuwa kubwa sana kwa Watanzania.
Inafikia wakati ukiunganisha pesa inayochukuliwa kwenye mshahara ni asilimia 60 ya kipato cha mtu, je ataishije? Hii inaumiza hata kama ni uzalendo(PAYE 25% au zaidi+VAT18+TOZO+PSSSF/NSSF+ NHIF). Hapo usiwe na mkopo benki au loan board.
Kama taifa limepitia stress nyingi, tuzigawane : post Covid19 stress , Uongozi wenye mlengo mmoja, Uchumi/Tozo unaenda kuendeleza kudumaa kwa afya ya akili ya watanzania wengi kama hautatizamwa vyema. Tunaendelea kuongeza idadi ya mtanzuko wa afya ya akili ndani ya Taifa, tuliponye kwa kulionjesha furaha na amani ya moyo kwa kila mmoja wetu. Tusione tu matukio ya ajabu yanatokea, wengi miongoni mwa watu hawako vyema kiakili kwa sababu ya mambo haya.
2: Matumizi ya Serikali baada ya kutoza tozo
Hakuna hatua yoyote iliyoonyeshwa ya wazi kwa serikali kuepuka matumizi ya ANASA. Hii inahusisha kulipana posho kwa kazi za msingi za wahusika tena zikiwa ni posho za kiwango cha juu sana.
Hii inahusisha viongozi wakuu wa serikali, wabunge, mawaziri na viongozi waandamizi wa serikali, kwani wao uzalendo hauwahusu?
Hata kama kuna policy zinasema hivyo, wakati wa dharura naamini tukiamua kufunga mikanda mambo mengine huahilishwa kwa muda. Pesa hizo zingeelekezwa kwenye hiyo miradi na kupunguzia wananchi kiasi na idadi ya TOZO.
Ununuzi wa magari ya kifahari, ziara zisizo na tija, mikutano ya ana kwa ana na semina wakati kuna teknolojia nk. Kusimamia value for money kwa miradi mingi ya serikali na kuondoa 10% nyingi.
Haya yote yanaonyeaha serikali haijawa na nia ya dhati/yanayoelezwa hayatoki moyoni, onyesheni mfano kwa kufunga mikanda ili kuonyesha njia.
3: Ni nani anahusika na uzalendo huu. Tozo vs kodi (solidarity fund).
Kinachoonekana hii inagusa wapangiwa/wasio na sauti/wasio viongozi. Hatujaona viongozi wakuu, mawaziri na wabunge etc. Wakiguswa na hili, tuongee lugha moja.
Wakiziondoa zile exemption zao kwa muda ili tukipite kipindi hiki kigumu wote. Mfano: wote tulipe kodi kwenye ujira wetu, punguza marupurupu kwa kiasi fulani au ondoa, achaneni na magari ya kifahari yanayogharimu pesa nyingi kununua, service za gharama kubwa na mafuta mengi kwa umbali mdogo.
Fanyeni kazi au vikao kwa uzalendo kwa kuondoa baadhi ya posho zenu ili uzalendo utiririke kuanzia juu mpaka chini kwa mwananchi wa kawaida naamini hakutakuwa na malalamiko.
Namalizia kwa kusema tatizo la msingi lipo kwenye: nani anachanga, kiasi gani, mara ngapi, nani anatumia na kwa mwenendo upi.
Hapa shida ni nani wa kumfunga paka kengele. Tuuvae uzalendo wa kweli.