SOLVED: Kwa wale wote waliotuma maombi NBS na hawajatumiwa e-mail ya password fanya hivi

reyzzap

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Posts
6,813
Reaction score
21,807
Sina muda, fanya hivi...

Kwanza ingia Google tengeneza Email mpya(sipaswi kukukumbusha kukumbuka password)

Rudi Google kwenye www.nbs.go.tz

Anza kujaza fomu upya,
Katika zile taarifa zako za mwanzo badilisha vitu vifuatavyo..

1.Weka email mpya,
2. Badilisha Namba ya FM4
3. Badilisha Namba ya Nida

Kubadilisha ninakozungumzia ni kama unajikosesha hivi, mfano badala S0256-0067-2011 unaweka S0256-0056-2012, hivyo hivyo Nida unaweza ukabadili ter na mwezi

Halafu tuma maombi

NOTE : Hakikisha upo sehemu yenye mtando vizuri (H+) la sivyo Taarifa itaenda ila ikishindwa kuji refresh email haitarudi.

Watakuletea MSG na email yenye password

Badala ya hapo ukishapakua fomu

Rudi tena www.nbs.go.tz, fika mpaka hapa halafu bonyeza hapo namba 3


Copy and paste Email na Password waliyokutumia KAMA ILIVYO halafu ingia

Itafunguka, badala ya hapo kuna sehemu juu kabisa utaona amekuandikia "Huisha taarifa za Mwombaji".. bonyeza,
Itafunguka, sasa anza ku edit zile sehemu ulizojikoseha kwa kuweka taarifa SAHIHI kabisa.

Badala ya hapo nenda chini amekuandikia Tuma maombi, bonyeza

Kama kawaida watakuletea kupakua fomu, fanya hivyo, utakua umemaliza

Siandiki nadharia hapa, hiki nimewafanyia watu na imekubali.
 
Oya mkuu upo serious
 
Sehemu ya nida huwezi kuedit
 
Mkuu una uhakika na hiki ulichokiandika?

Mwanzoni kabisa baada ya tangazo nilimsaidia mdogo wangu kuomba japo yupo mbali na nilipo mimi ila mambo yalienda sawa kabisa.

Alipata password kupitia email yake akanirushia nikapakua form ili akaijaze kwa Mwenyekiti wa mtaa.

Kwa bahati mbaya alikosea mtaa nikamwambia inawezekana kubadili, basi nikafanya hivyo.
Katika kuhuisha form huwezi kubadili email, NIDA na Index Number.

Hicho ndicho nilichokiona.
 
Yeah sure. Nida hubadili
 
Ndugu yangu upo sahihi nimefanya hivo wameniletea nywila kesho naenda kukamilisha usajili
 
Yaani hapo unaweza mfumo ukakubali lakini baadae ukawa hujachaguliwa kwa taarifa za uongo. Kumbuka huu mfumo wameunganisha na baadhi ya taarifa kama NACTE, NIDA n.k hivyo unaweza ukadanganya harafu kwenye mfumo ukipeleka kwenye namba ya simu documents zako ukaja kurudi kwenye nida zinakuwa hazi match inakula kwako.
 
Siunarekebisha baada ya kulogin sio kwamba unaziacha hivyohivyo
 
HaRAfu ndo nini?
 
Anajidanganya ajui index number ya form four na namba ya nida zinaenda kufetch information zako na kuangalia uhalisia wa maajina uliyoandika kama yapo sawa na cheti chako cha kuzaliwa ndio maana ukikosea namba inagoma sababu tarifa zako zinakuwa haziwiani na majina uliyoandika juu
 
Nyie ndo mnasababisha tukutane na hili neno la kuwa index namba ya fomu four imetumika .Acheni kujisajilli kwa namba za wengine
 
Kwa faida ya wengi,,


Chochote utachofanya kwenye kujisajili NBS unaweza kujikosesha taarifa zako kama alivyosema mtoa mada hapo juu na ukaupdate hizo taarifa isipokuwa TU wadhamini usijikoseshe. Haeabadilliki
 
Mzee baba BIG UP na Asante Sana nimefuata hizo taratibu na imekubali....

Kwa walio na hofu, Hakuna kinachoharibika, kumbuka ndani ya siku hizi kabla ya kufunga maombi chochote unaweza uka edit maana bado hawajaanza kupitia hizo form.

Na wanaosema hii itafanya index namba za wengine ionekane imetumika si kweli sababu utaibadilisha, mimi niliweka ya mtoto wa anko, baadae kwenye ku edit nikaweka yangu ikakubadi na yeye nikamfungulia kwa hio yake ikakubali pia.
 
Mi nimefuata huo utaratibu na imekubali, nimesota siku nne napiga simu hazipokelewi, hii ndio ilikua beti yangu na imetick.
NIDA ya mara ya kwanza umeweka ya nani na hiyo nida mpya ni ya nani.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…