Amani Dimile
JF-Expert Member
- Jul 27, 2022
- 243
- 399
Mwanangu leo kabla hujalala naomba unisikilize kidogo, ninalo neno nahitaji kukuusia huenda likakufaa kimaisha. Kama si leo basi kesho na kama si kesho basi mtondo ..
Mwanangu tupo chini ya mbingu, sababu ya Mungu. Yeye asiye na majungu, mwenye upendo usio na ukungu agaae riziki kwa mafungu. Mheshimu na umuogope sana yeye, kwa maana bila yeye sidhani kama sisi tungalikuwapo hapa.
Mwanangu maisha ya dunia yana siri kubwa, tena si kubwa bali kubwa sana, hivyo jaribu tu kuwa makini. Ukiwatazama wanadamu wafananishe na mihogo, kwa maana mihogo yote ina maganda sawa lakini haina ladha sawa yaani kila mhogo na ladha yake. Vivyo hivyo sisi, tuna ngozi na muonekano sawa lakini hatuna tabia sawa.
Dunia hii ni nzuri lakini haina mzuri, dunia hii ni njema lakini haina wema. Binadamu wameichafua sana, hasa kwa tabia zao zisizoelezeka. Kuwa makini sana na unafki, kwani maisha ya sasa yamejaa sana unafki na chuki. Ambao utawaaga na wakakwambia safari njema huenda wakawa ndio hao hao watakaochukia wakikuona umefika salama.
Ndio mwanangu usishangae, tena usishangae kabisa maana binadamu watatamani uwe bora lakini si bora kuwazidi wao.
Mwanangu maisha yamebadilika sana, siku hizi ukimya una thamani kuliko maneno mengi. Hivyo jifunze sana kunyamaza, jifunze kuwa mkimya, jifunze kufunga mdomo wako kwani hata samaki mfumba mdomo kamwe hanaswi na ndoano.
Epuka tamaa mwanangu, epuka sana narudia epuka sana tamaa. Maana tamaa na kuridhika havina undugu, yeyote mwenye tamaa hatosheki na anaetosheka katu hana tamaa. Asietosheka hana shukrani, asie na shukrani hatosheki, hivyo mwanangu jifunze kuwa na shukrani hata kwa kidogo ili ujifunze kuridhika . Yaani kama hutosheki kwa kidogo basi huwezi kuridhika kwa kikubwa. Kijana wangu kumbuka kama huwezi kushukuru kwa tone moja la maji utakalopewa basi kamwe hata ukipewa lita moja huwezi kushukuru.
Mwanangu zichunge sana hisia zako, zichunge sana. Maana zinaweza kukuongoza ndani ya dakika chache halafu zikaja kukugharimu maisha yako yote.
Mwanangu .............. (Itaendelea ✍🏽)
Wako katika kalamu Amani Dimile

Upvote
1