Soma kidato cha 5 na 6 kwa Tsh 250,000 kwa mwaka

IPILIMO

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,819
Reaction score
801
Itende high School iliyopo Mbeya mjini, nje kidogo ya jiji, ina tangaza OFA kubwa ya ada ya shule KUTWA sh 250,000 kwa mwaka mzima:

  • Hii na kidato cha 5 & 6 tu.
  • Kidato cha 6 ni kwa nafasi za KUHAMIA TU; zoezi ni sasa hadi June 30, baada ya hapo huwezi kuhama au kuhamia.
  • Kidato cha 5 kujiunga kwa wenye credit zote 3 au pungufu, Ila kwa watakao kuwa na pungufu watahitaji kuresit mwaka ujao (programu ya kuwasiadia ipo).
  • Michepuo ni HGL, HGK NA HKL kwa FORM 6
  • Michepuo kidato cha 5; HGL, HGK, HKL & HGE
  • Anaye taka kuishi bweni ADA JUMLA NI 750,000 SH KWA MWAKA.
  • KARIBU; FIKA AU KAMA UKO MBALI WASILIANA NASI KWA 0754-734009 AU itende2011@yahoo.com
  • WAHI HII NI FURSA NZURI KWA NAFUU YA ADA NA SEHEMU NZURI YA KUPATA ADVANCED SECONDARY EDUCATION.
 
Siku hizi matangazo bwana! Hapo utakuta ukishafika eneo husika unaambiwa shule iko gorofa ya tatu, unakuta chumba cha kulala wageni(guest room) kimebadilishwa kua darasa.

Haya me napita tu ila kesho namimi ntatangaza shule yangu, coz imekua fashion(hata nursery hawalipi 250,000/=)
 

Pole sana, inaonekana uko gizani, wasiliana nasi tukwambie kwanini hivyo!! Hiki si chuo cha gorofa ya pili wala ya tatu, hii ni marketing strategy tu! Kuna wakati hata ungekuwa wewe ungekuwa unauza goods au kutoa service utafanya promo, huku ukijua there is a time to loose for future gain.

So acha kubeza, It is a real thing and very serious in action! Wengine wanachangamkia opportunity hii!
 

kuna jukwaa la matangazo mkuu.. IPILIMO So umebugi men
 
Last edited by a moderator:
Bora shule ya Mulugo mkuu Shardcole,Itende napapata,ni mabanda ya kufugia wanafunzi tu,hakuna elimu pale.

ha ha ha ha! Mkuu kumbe hivyo, mi nilitaka kushangaa shule gani ada ndogo kama pocket money vile. Basi waige mfano wa shule kama za Swilla Sec na pandahili sec etc ambazo pale hakuna porojo bali ni kitabu kwenda mbele na wala hakuna promo zao JF bali kizuri kinajiuza chenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu IPILIMO kila la kheri,isikatishwe tamaa na member wa 'hotpot' family.
Piga mzigo mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Shule hadi jf, nitawaleta wadogo zangu 20, coz ada ni ndogo xana utadhani ni pesa ya kwenda kununua mbogamboga na matunda.
 
Shule hadi jf, nitawaleta wadogo zangu 20, coz ada ni ndogo xana utadhani ni pesa ya kwenda kununua mbogamboga na matunda.

Kwa jinsi ulivyo elewa!
 

Kabla hakijajiuza kilifanya promo! hayo ni mawazo mgando, pole sana (kama una uza kitu kizuri weka/fungia ndani kisha wambie watu nauza!!!!!!)
 
Ha! Hv ni shule! Mi nkajua ni kituo cha masomo ya ziada, pigen kaz wazee lakin wateja wenu watakuwa 4m4 failures. Hiyo nayo ni chalange u have to work on that.ha! ha! ha! ha! ha! haaaaa!
 

Ha ha ha ha......Mbona tayari umezifanyia promo hizo skuli.....!!
 
mkuu me nitawaleta wadogo zangu wawili wa kidato cha pili kutoka hapa FEZA BOYS watakusaidia kufundisha kidato cha nne (Form 4) hapo shuleni kwako.
 
msipende sana kubeza shule za watu wengine wakuu tutumie busara kwani kwa sasa kufaulu kwa mwanafunzi ni juhudi zake mwenyewe na wala si majengo.
 
mmh! mazingira mazuri create interest of learners, kwahiyo shule imejengwa kwa makuti ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…