"Soma kwa bidii ili ufanikiwe" msemo unaopatikana katika nchi maskini pekee

"Soma kwa bidii ili ufanikiwe" msemo unaopatikana katika nchi maskini pekee

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari,

Binafsi nikiri kuwa sijawahi kuvuka mpaka wa Tanzania ila nina exposure ya kutosha kuliko hata wauza unga waliozamia Afrika ya kusini.

O level nimefundishwa mathematics na walimu 3 Wakimarekani, nimefanya kazi na Wazungu kwenye kampuni 2 tofauti.

Kwahiyo Wazungu niliokutana nao wote ni wasomi na wana exposure kubwa. Marekani kusoma ni wajibu na elimu yao haina ujanjaujanja.

Mwanafunzi ukidanfanya kwenye mtihani hukumu yako ni kufukuzwa shule haraka endapo tu ushahidi ukipatikana.

Na mwalimu ukibainika kushiriki udanganyifu(cheating) kwenye mitihani ya wanafunzi wako unafukuzwa kazi haraka na sometimes jela utafungwa.

Kule ukiwa na degree ya sheria wewe ni mwanasheria haswa, engineer ni engineer kweli, afisa kilimo ni afisa kweli. Nchi maskini kwasababu ya uchache wa wasomi basi kila mtu humpigania mtoto wake apate elimu hata kama elimu yenyewe ni ya mchongo akiamini kuwa akifaulu vizuri ataajiriwa.

Msemo kama 'soma kwa bidii ufanikiwe', ' someni kwa bidii ili muwe kama fulani'. Target ni KUFAULU, huruma sana. Sasa ndio tumeanza kuwa na wasomi wengi wanaolia na ukosefu wa ajira ila ukimchallenge na maswali juu ya alichosomea ni mtihani.

Tubadili fikra zetu tusomeshe watoto watakaoleta matokeo chanya ndani ya jamii zetu.
 
Kutoka unajua Nini Hadi unamjua nani?

Kakaze shingo darasani uje ufie mtaani...japo sio kwa wote
 
Ingawa sio wote lakini mifumo ya elimu Africa hapo nyuma ilikuwa ni kukaririsha wanafunzi ili kufaulu mtihani lakini ukimleta mhitimu katika real world ni zero
 
Ingawa sio wote lakini mifumo ya elimu Africa hapo nyuma ilikuwa ni kukaririsha wanafunzi ili kufaulu mtihani lakini ukimleta mhitimu katika real world ni zero
Ni kweli kabisa. yani mfumo huu umetuharibu sana
 
Back
Top Bottom