Soma kwa makini na toa ushauri wako nini kifanyike kwa watu wenye kipaji lakini mfumo hauwatambui

Soma kwa makini na toa ushauri wako nini kifanyike kwa watu wenye kipaji lakini mfumo hauwatambui

MeinKempf

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
11,093
Reaction score
7,229
kipaji2.JPGmasatelite 4.JPG

Katika hali ya kushangaza, mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Ali, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, amekamatwa na polisi baada ya kudaiwa kuunganisha visivyo halali, mitambo ambayo iliwawezesha watu kuangalia matangazo ya televisheni ya vituo mbalimbali kwa malipo rahisi.

Awali, msamaria mwema mmoja alipiga simu na kutonya juu ya uwezo wa mtu huyo anayewashangaza kwa utaalamu wake wa kuunganisha mitambo hiyo bila kugundulika.

“Hapa kuna watu kama 80 hivi wameunganishwa, wanaangalia televisheni za Azam, Zuku na nyingine kwa bei chee, lakini wanaangalia mipira, filamu na kila kitu, yaani huwezi kuamini kaka,” chanzo hicho kilinyetisha

Katika kujiridhisha, kikosi kazi chini ya kamanda mkuu, kilitembelea eneo la tukio na kufanya ukaguzi wa siri, uliothibitisha kuwepo kwa huduma hiyo, lakini bila ya kuwepo kwa dekoda za vituo hivyo vya televisheni vinavyotolewa kwa malipo.

Baada ya kujiridhisha huko, baadae mawasiliano yalifanyika kwa wahusika wa vituo hivyo, ambao nao walitembelea eneo hilo la tukio na kujionea wenyewe. Wahusika hao walikuwa ni Afisa Leseni wa DSTV na Afisa Mauzo wa Azam Tv pamoja na mtu mmoja kutoka chama cha hakimiliki cha COSOTA.

Afisa Leseni kutoka chama cha hakimiliki COSOTA, Zephania Lyamuya (kulia) akisimamia zoezi.

Baadae maofisa hao walishauriwa kuripoti jambo hilo kituo cha polisi, ushauri ambao waliukubali na kwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Oystebay ambao waliongozana na watu hao hadi Mwananyamala.

Madishi ya Satelaiti yanayotumiwa na Bw. Ali kurushia matangazo ya televishen yakiwa juu ya nyumba yake.

Kufika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo ambaye pia ni maarufu kwa jina la utani kama Masetelaiti, Polisi walifanikiwa kumkamata na baada ya upekuzi, waligundua kuwepo kwa mitambo ya aina mbalimbali, vikiwemo ving’amuzi vya aina mbalimbali, modulators, Receivers na vifaa vingine vikionekana vikiwa vimeunganishwa kwa utaalamu wa hali ya juu katika ukuta wa sebule yake.

Masetelaiti alikiri kuendesha maisha kwa staili hiyo na kudai kuwa utaalamu wa kuunganisha ving’amuzi hivyo ni wake mwenyewe na amekuwa akifanya hivyo kwa muda mrefu.

use1.JPG

Afisa Leseni kutoka Cosota, Zephania Lyamuya alisema jamaa huyo anastahili kupelekwa Polisi kutoa maelezo kwani licha ya kutokuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo, pia amekuwa akiwanyonya waigizaji wanaostahili kulipwa kila filamu zao zinaporushwa katika televisheni za nje.

Naye Afisa Mkuu wa Mauzo kutoka kampuni ya Azam aliyejitambulisha kwa jina la Shah Seffu (pichani kulia), alisema kuwa operesheni hiyo ni moja kati ya hatua walizozipanga kumaliza tatizo la kuingilia mawasiliano ya televisheni jambo ambalo limeonekana kukua kwa kasi nchini.

Baada ya kuvikusanya vifaa hivyo vilipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay sambamba na mtuhumiwa kutoa maelezo ambapo jalada lilifunguliwa OB/RB/16106/2014, KUINGILIA MAWASILIANO YA TELEVISHENI
Toa maoni ya nini kifanyike kwa watu wenye kipaji kama huyu jamaa....mimi naona wangeweza kutumiwa na wizara ya sayansi na teknologia kukuza vipaji vyao.
 
Kiukweli hapa Tz hakuna mfumo wowote kuwaendeleza watu kulingana na vipaji vyao, tunaingia kwenye mfumo wa elimu ya kikoloni na bila shaka twajua kuwa hii elimu wameturithisha wakiwa na lengo la kujinufaisha wao hivyo sisi hatuwezi kuza vipaji vyetu zaidi ya kuendelea kuwategemea wao.....
 
mfumo mbovu sana wa kutegemea kuajiriwa hivyo yule ambaye ajaajiriwa anaonekana hana hata akili ya kufanya chochote wala kuchangia chochote katika taifa hili hasa wale wagunduzi wadogo wadogo kama huyo kijana hapo
 
Utafanya nini? Wenye uwezo wa kufanya hawataki!
 
Kwa akili ya ziada huyu jamaa angechukuliwa na vyombo vya usalama na kuangalia uwezekano na namna ya kumtumia katika mambo ya mawasiliano na elektroniki baadala ya kutafuta namna ya kumfunga. Wajiulize hivi wakimfunga watapata nini? Na nini maana ya vipaji. Hiki kimeonekana ingawa katika sura ya uhalifu lakini kwani mfumo una namna ya kuvipata vipaji hivi? Jibu ni hakuna. Lakini vyombo vyenyewe vinategemea nani yuko pale na ana vision gani au lau anaeweza kusikia ushauri na kuufanyia kazi.
 
Tuna mtaalamu wetu anaitwa Transistor tafaadhali mkuu ushapita NA HUKU? back to the topic...labda inaweza isiwe ni jukumu la tanzania kama nchi ila kwa upande flani ni lazima nchi itambue jinsi ya kuendeleza watu kama hawa!! it's pity a graduate student hajagundua hata nati!!!! alafu watu kama hawa wana pelekwa police...inauma ila hii ndio nchi yetu!!
 
Last edited by a moderator:
Kiukweli hapa Tz hakuna mfumo wowote kuwaendeleza watu kulingana na vipaji vyao, tunaingia kwenye mfumo wa elimu ya kikoloni na bila shaka twajua kuwa hii elimu wameturithisha wakiwa na lengo la kujinufaisha wao hivyo sisi hatuwezi kuza vipaji vyetu zaidi ya kuendelea kuwategemea wao.....

Na kwa kudhihirisha hilo utakuta jamaa anaenda kupotezwa kabisa na kipaji chake.
 
Tuna mtaalamu wetu anaitwa Transistor tafaadhali mkuu ushapita NA HUKU? back to the topic...labda inaweza isiwe ni jukumu la tanzania kama nchi ila kwa upande flani ni lazima nchi itambue jinsi ya kuendeleza watu kama hawa!! it's pity a graduate student hajagundua hata nati!!!! alafu watu kama hawa wana pelekwa police...inauma ila hii ndio nchi yetu!!

Na wanapiga kelele kilimo kilimo kila siku wakati wengine wanafani zao za kiteknologia kama hizi. yaani huyu ingekuwa nchi za wenzetu wanaothamini ujuzi na maalifa , angeliweza kuwa mtu muhimu sana kwao. Ila kwa TZ anageuka kuwa memba wa lupango .
 
Last edited by a moderator:
Kwa akili ya ziada huyu jamaa angechukuliwa na vyombo vya usalama na kuangalia uwezekano na namna ya kumtumia katika mambo ya mawasiliano na elektroniki baadala ya kutafuta namna ya kumfunga. Wajiulize hivi wakimfunga watapata nini? Na nini maana ya vipaji. Hiki kimeonekana ingawa katika sura ya uhalifu lakini kwani mfumo una namna ya kuvipata vipaji hivi? Jibu ni hakuna. Lakini vyombo vyenyewe vinategemea nani yuko pale na ana vision gani au lau anaeweza kusikia ushauri na kuufanyia kazi.

Watu wenye ushauri na mawazo ya kujenga kama wewe hivi hapa TZ utakuta hawana nafasi ya kabisa ya kutoa mawazo mbadala kama yako.
 
Kwa akili ya ziada huyu jamaa angechukuliwa na vyombo vya usalama na kuangalia uwezekano na namna ya kumtumia katika mambo ya mawasiliano na elektroniki baadala ya kutafuta namna ya kumfunga. Wajiulize hivi wakimfunga watapata nini? Na nini maana ya vipaji. Hiki kimeonekana ingawa katika sura ya uhalifu lakini kwani mfumo una namna ya kuvipata vipaji hivi? Jibu ni hakuna. Lakini vyombo vyenyewe vinategemea nani yuko pale na ana vision gani au lau anaeweza kusikia ushauri na kuufanyia kazi.

Kabisa mkuu na angesaidia sn hyo sector na huenda kutokana na mazingira angegundua mapya zaidi.

Ooh naililia nchi yangu
Ht katiba haiwatambui
 
Sidhani kama mtu wa namna hii anafaa kuwa idara ya usalama atauza siri kwa tamaa. Watu kama hawa tunatakiwa tuwapige vita kama vita dhidi ya mafisadi.

Fikiria watu kama hawa wameingilia system za DSTV nk,itakuwaje siku wakaingilia system za bank(akaunti za watu),simu za mkononoi(mpesa,tgopesa),tanesco,mawasiliano ya polisi.

Ukiangalia nyumba yake unagundua ni mtu mwenye uwezo wa kifedha lakini bado anataka kupata zaidi kwa kuwatapeli wengine,Kwa nini hicho alichokipata asifungue biashara halali?,Leo mtu kama yeye tukimpa kitengo cha mawasiliano JKTz hata alipwe mamilioni atauza siri kwa nchi madui zetu

Natoa witu watu kama hawa si wazalendo tuwakemee na apewe adhabu kali na faini juu ili iwe fundisho
 
huyu hakuna chochote alichogundua, mikoani hiyo mifumo imejaa wenyewe wanaita "kebo" wanatoza elfu 10 kwa mwezi unapata channel zote za dstv, ni illegal kwa sababu unakuwa unaibia hao provider. huyu ni mhalifu tu.
 
Navutiwa sana na watu wenye Vipaji kama Huyu bwana ALLY. Ni lazima nikiri wapo wengi sana ila nafikiri wanakosa tu Miongozo (si lazima kutoka kwa serikali) sahihi ya nini cha kufany, na hii ni kutokana na ufinyu wa kutumia akili zao vizuri.

Kwanini hicho kipaji / ujuzi wake asingeufanya bila mauzo, yaani angeandaa ka documentary kanakoonyesha uwezo wake halafu akakatumia kutafuta wadhamini / ajira?

My take:

Naamini Watu wenye vipaji wana uwezo mkubwa sana wa kufikiria, hivyo wawe wepesi wa kufikiria njia positive za ku-showcase hivyo vipaji vyao, si kwa uhalifu, kwa sababu sheria haina huruma, kosa la mhalifu litahukumiwa accordingly!!

Pia wao wenyewe wajitahidi kushirikisha washika dau kwenye angles husika, ili waweze kupata walau hata ushauri wa kitaalamu wa nini cha kufanya..

MUHIMU SANA:

Napinga Vikali watu Kutumia vipaji vyao kwa Uhalifu eti kwa kisingizio cha mfumo haujawatambua!!!!

KAMA UNAFANYA KITU USEFUL KWA DUNIA YA SASA NI RAHISI KUONEKANA SI TU NA SERIKALI, BALI HATA NA TAASIS ZISIZO ZA KISERIKALI, MATAIFA YA KIGENI NA WADAU WENGI KUTOKA SEHEMU MBALI MBALI DUNIANI..

WATANZANIA WAWE WEREVU SASA!!

na huyu hana ubunifu wwowote, kila kitu unachokiona hapo ni plug and play!
 
Mzalendo akichoka kuonewa anageuka kuwa muasi...kazi ipo kwa kweli kwenye huu utawala watu wanateseka na haya maisha magum..mpaka wanaibuka na fursa kama hzii
 
huyu hakuna chochote alichogundua, mikoani hiyo mifumo imejaa wenyewe wanaita "kebo" wanatoza elfu 10 kwa mwezi unapata channel zote za dstv, ni illegal kwa sababu unakuwa unaibia hao provider. huyu ni mhalifu tu.
Hata mimi sioni kipaji chochote kiukweli.
 
Mdau hata ISIS wanathubutu kufanya wanachokijua, je nao tuwapongeze?

miaka ya 90s tulimwona hamza kalala akirudi mikono mitupu zaire alipokwenda kudai malipo kwa wimbo wake wa dezodezo.
Hakukuwa na sheria ya hati miliki wakati huo.
Ndg madish atashitakiwa na nani kwa kosa gani?
-tcra kwa kurusha matangazo bila leseni
- dstv, azam, startimes kwa kudukua matangazo yao, au kuyarusha mara ya pili bila idhini.
- cosota kwa kurusha michezo yenye hati miliki ambayo tayari inarushwa na vituo kadhaa
- mashitaka yake yanaweza kuwa 101, au 1 na akaishia kuachiwa huru.

Tunawahitaji watu hawa kupanua uelewa wetu wa mambo, kwa kushughuliki hili tcra na taasisi shiriki watapata kuona mianya iliyopo.

Miaka ya mwisho ya 90 marekani waliuhusisha uislamu na ugaidi, wengi hatukulikubali. Makundi yale yaliyotumia mwamvuli wa dini yanabadili mbinu kila kukicha toka makundi makubwa ya kijeshi mpaka bateri (kikosi kidogo cha watu hata 8 wenye msimamo sawa na kikosi mama lakini hakipati amri ya moja kwa moja toka kikosi mama kutimiza malengo yao). Mabadiliko ya jinsi ya wahusika wa ugaidi kutoka waarabu, ... sasa tuna waindi na wazungu.
Kuangalia uthubutu wa magaidi tunajifunza kujikinga nao na si kuwapongeza si ajabu ugaidi ukaanzisha vita ya tatu ya dunia kama hatuta angaza mianya itakayo wapa uthubutu.
 
Nchi zilizoendelea zimeajiri top hackers kuwa moja ya staffs wao kwenye ku tackle ciber crime baada ya kutumikia adhabu ndogo. Tafadhali nasi tujifunze.
 
Back
Top Bottom