SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Baada ya majadiliano ya jana baada ya uzinduzi wa jezi, nimepata wasaa wa kutafakari mtazamo wangu nilioutoa jana. Nitaelezea kwa ufupi sana ila huu utakuwa mchango wangu wa mwisho kwenye mada hii.
Kuna mawili, ni ama Simba imepatia sana katika hili jambo au imekosea mno.
Simba imepatia sana:
Kama zile 5 na 1 zilizopo kwenye jezi zina uhusiano wowote na kutumia neno Sanda ikiwa na maana ya Simba imezika kiimani na kiroho aibu yote iliyotokana na yale yaliyotokea msimu uliopita, basi hapo itakuwa imepatia sana na tutegemee Simba yenye mafanikio zaidi msimu huu. Kama nia ni kuendelea kusaka yeyote aliyehusika na hujuma ya zile goli 5 ili akiivaa jezi sanda imhusu, siyo mbaya ila naona kama tutakuwa tunaangalia nyuma sana (wale wa nyuma mwiko mpooo?). Haya ni mambo ya kiroho zaidi, nadhani mtajiongeza wenyewe.
Simba imekosea sana:
Kama yale niliyosema jana yamefanyika kwa hila za watu wachache walio ndani na nje ya Simba au kama ilikuwa ni nia njema asiyozaa matunda yaliyotarajiwa halafu Simba ikipokea kipigo kizito msimu huu kutoka kwa Yanga na isipofanikiwa kutwaa NBC na kutolewa mapema CAFCC, Simba inaenda kupotea mazima. Haya yakitokea msimu huu, tutegemee anguko kubwa la Simba litakalodumu muda mrefu sana.
Muda utasema lipi ni sahihi ila Simba ijitafakari sana. Binafsi sitatoa mchango zaidi katika mada hii.
Kwa kumalizia, soma Zaburi 132:18 na Zaburi 109:29.