Soma maelezo ya singano inasikitisha

Soma maelezo ya singano inasikitisha

wakimataifa

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2014
Posts
942
Reaction score
168
kwa kweli maelezo ya ramadhani singano mesi kuhusu utata wa mkataba wake na simba inasikitisha sana kwanza anaishi kwenye skwata amenyimwa pacent yake kiujumla mkataba viongozi wa simba wamefoji wala simba wasikatae ila namshauri mesi japo simba wanamwita asiende wakutane mahakama ya fifa tff awepe taarifa tu wakati anaenda fifa aombe kibali fifa kwa kuchezea timu yeyote ili kiwango chake kisishuke
 
Sasa si uandike vizuri!
Kwanza huyo unayemsema ni nani? Ndio maana mpira wetu haupandi kiwango maana mashabiki, wachezaji wote akili kiwango sawa.
 
naona umeandika na jazba mkuu, kunywa maji kidogo, shusha pumzi, then njoo uandike
 
Mleta uzi naona umekurupuka hata habari yako haileweki rudi kajipange upya. Simba wameshasema wao wana mkataba na wako tayari kuuweka wazi. Sasa ni zamu ya ramadhani singano naye kuweka kopi yake mkataba wazi hapo ndipo itajulikana nani mkweli nani mwongo. Kitendo chochote cha kughushi ni kosa iwe kwa singano au kwa viongozi wa simba. Pili kama singano kapata timu na inataka kumlipa vizuri aende akawajulishe tu viongozi wake wampe baraka aondoke simba haijawahi kumzuia mchezaji kuhama rejea suala la kapombe. Timu inayowazuia wachezaji kuhama ipo na inajulikana hata upate timu ulaya watakuzuia tu lakini sio simba.
 
  • Thanks
Reactions: tyc
Ni wakati muafaka sasa kwa wachezaji wa kitanzania kuwa na aidha wanasheria au mameneja makini wenye ufahamu wa mambo ya mikataba wa kuwasimamia mikataba na masilahi yao. Wasiangalie tu faida wakubali kuingia gharama ya kuwalipa watu wenye utaalamu kuwasimamia kwani faida ni kubwa kuliko hasara wanayopata sasa. Tumechoka na hizi kelele zao kila mwaka hasa kipindi hiki cha usajili. Wakiwekewa milioni 20 mezani hata mikataba hawasomi kifungu kwa kifungu wanakimbilia kusaini tu baadaye inakuwa shida.
 
Mleta uzi naona umekurupuka hata habari yako haileweki rudi kajipange upya. Simba wameshasema wao wana mkataba na wako tayari kuuweka wazi. Sasa ni zamu ya ramadhani singano naye kuweka kopi yake mkataba wazi hapo ndipo itajulikana nani mkweli nani mwongo. Kitendo chochote cha kughushi ni kosa iwe kwa singano au kwa viongozi wa simba. Pili kama singano kapata timu na inataka kumlipa vizuri aende akawajulishe tu viongozi wake wampe baraka aondoke simba haijawahi kumzuia mchezaji kuhama rejea suala la kapombe. Timu inayowazuia wachezaji kuhama ipo na inajulikana hata upate timu ulaya watakuzuia tu lakini sio simba.

Bora umemsaidia mleta uzi,

Kitakachofanya tuamini Simba wameforge mkataba ni pale Rama atakapopeleka au kuonyesha original doc, kwa mujibu wa Hans Poppe Rama amewasilisha copy inayosema miaka 2 wakati Simba wana original inayosema miaka 3 sawa na ule uliokuwa TFF.
 
mpaka sasa hivi hatujui nani mkweli wakati simba wanasema waliongeza mkataba wa singano pale walipomrekebishia mshahara yeye anakana lakini kama kweli aliboreshewa mshahara lazima uendane na marekebisho ya mshahara pia kwenye mkataba kuna sahihi ya dole gumba badala ya kuanza kulalamikia upande mmoja ni bora kila kitu kikawekwa wazi ili mbivu na mbichi zijulikane
 
Hakuna wa kutueleza kwa kituo sisi ambao tumepitwa na hii?Naona hapa mnafikiri wote tunajua hii kitu
 
Hata hivyo singano bado hajafanya kile nilichotaraj miaka mitatu iliyopita
 
Kwa jinsi singano alivyoongea kwa jazba jana usiku wakati anahojiwa na shaffi dauda wa radio clouds naushauri uongozi wa simba uachane naye kwani inaonekana kuna watu wanamjaza upepo huyo dogo na pia kalewa sifa kwa kuitwa messi na hili kajisifia wazi redioni bila kificho. Simba ni taasisi kubwa sana huwezi linganisha na mtu anayeitwa ramadhani singano. Ikumbukwe simba waliwahi kupita mawinga wengi wakali sana wakina thuweni ally, dua saidi, mark sirengo n.k. Itakuwa singano bwana aende zake sisi atuachie simba yetu bana tumeshamchoka. Kimsingi aachwe akapate changamoto ya kupigania namba katika timu nyingine ili tuweze kujua kuwa ana uwezo au hana kwa sababu hapo simba alipata urahisi sana kwani kwa miaka miwili alikuwa yeye na okwi tu ndio mawinga.
 
Kama vipi jamaa aende kwa jinsi nilivyomsikia ata akibaki simba hatafanya kiroho safi kuna mtu anampa kiburi.
 
Sijui lini wachezaji wa bongo wataamka,ni wakati wa kuwa na wanasheria watakaowasimamia kwenye mikataba
 
Back
Top Bottom