thats why sanaa ya bongo haikui wala haindelei na sio katika movie tu hata muziki wengi wao hawafanyi hizo kazi ka ajira bali lengo lao kubwa ni kupata umaarufu, mademu na pombe za bure,vipamba kiaina na kuingia club bure hayo tu ndo wanafikiria ndo maana wanapewa vijihela kidogo na wadosi wanauza hadi hakimiliki zote za kazi yao. Mtu anakwambia kazi nimeuza ila hata hajui ni nakala ngapi, ye akishapewa starlet na millioni moja na akishobokewa na mademu baaasi, hataki tena. Ndio maana hata mapromota wanaweza sana wanamuziki anatafutiwa mademu, pombe afu bonge la show na watu wanaingia wengi anapewa laki moja anaambiwa tunakufanya maarufu umaarufu wa nini wakati huna pesa mfukon? Na hii sii akili ya Hemed tu ni ya wasanii wengi tu wengine ni wakubwa na maarufu hadi sometime najiuliza wabongo nani katuroga? Na mapromota na mameneja washawajua ukierevuka tu wanakubania mbaya
Pukudu @Ilkiding'a, Arusha