Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Kinachopelekea na kuchochea maandamano,machafuko na vurugu katika nchi yoyote ile kwa wananchi wake kuanza kumwagika na kumiminika mitaani kuandamana na kufanya vurugu kwa kiasi kikubwa huwa inatokana au kuchochewa na watu kukata tamaa na kukosa Matumaini ya kesho iliyo bora.
Pale watu wanapoona hakuna tumaini la kesho iliyo bora kuliko leo,hakuna haki katika vyombo vya utoaji haki,kuzidi na kukithiri kwa maonezi na unyanyasaji kwa wanyonge ,viongozi kuwa viziwi wa kero za watu na vipofu wa matatizo ya watu,viongozi kuishi maisha ya anasa na starehe huku wananchi wakiteseka katika dimbwi la umaskini,ubovu wa huduma za kijamii kama vile huduma za afya ,elimu,maji safi na Salama , kukithiri kwa rushwa na ufisadi ,wananchi kupuuzwa kwa kila kitu pamoja kuongezeka kwa kiwango cha walionacho na wasio nacho yaani wachache wanakuwa wanaogelea katika utajiri huku kundi kubwa likiteketea katika dimbwi la umaskini na ufukara uliokithiri na usiopimika mpaka watu wanatembea wakizungumza wenyewe njiani utafikiri vichaa ,huku nguo zikiwa zimejaa viraka na viatu vikiwa chini kwote kwenye sori vimechanika na hivyo kuwa kama wapo peku tuu.
Hayo yakitokea ,kuwepo ,kutamalaki na kukithiri katika jamii ndio huamsha hasira,chuki,vinyongo,visasi na ghadhabu ya umma bila kujali itikadi zao za kisiasa ,rika,dini,kabila,ukanda,jinsia n.k. vitu hivyo huchochea watu kuingia barabara bila kuhofia wala kuogopa risasi za moto wala mabomu ya machozi wala virunguu vya polisi wala magwanda ya jeshi wala mateke ya wanajeshi.
Watu huona bora kufa wakipigania haki yao kuliko kufa kwa njaa,watu huona bora kufa wakiwa barabarani kuliko kwenda kufia katika hospitali ya umma isiyo na dawa wala wahudumu wa kutosha wala huduma bora.watu huona ni bora wafe kwa risasi ili watoto wao na wajukuu zao waje wale matunda ya Damu yao iliyomwagika chini kwa ajili ya kulipigaia Taifa lao.hapo watu husonga mbele bila kujali nini kipo mbele yao,humkabili yeyote yule bila kujali kabeba nini mkononi mwake.wao nguvu yao huwa ni umoja wao.hawanaga cha kupoteza wala kuhofia watu waliokumbwa au kupitia hayo niliyoyaeleza kwa uchache na ufupi.
Lakini ukija Tanzania hali ni Tofauti sana,hali ni ya kutia matumaini kila uchwao.Serikaili ya CCM wakati wote wa uwepo wake madarakani imekuwa Sikivu sana kwa wananchi na watanzania wote kwa ujumla wake,imekuwa ikibadilika kulingana na wakati,imekuwa ikitoa majibu na majawabu kwa maswali ya watu kwa wakati.ndio maana hata wapinzani wa 1995 au 2010 au 2015 huwezi ukawakuta wote wapo bado upinzani.
Utakuta wengi wao wapo na wamerejea CCM.kwanini? Kwasababu wameona tumaini katika yale waliyokuwa wanapigania na kuyahitaji,wameona mwanga ,nuru na nyota njema mbele yao,wameona utekelezaji wa kasi wa yale waliyokuwa wanapigania na ndio maana wanaamua kurejea na kujiunga na CCM katika kuendeleza kazi hiyo njema.
Ndio maana leo hii unawaona watu kama Mheshimiwa David Kafulila,Mh David Silinde,Mh Juliana Daniel Shonza,Mh Joshua Nasari,Mh Peter Lijuakali,Mh Kitila Mkumbo,Mh Vincent Mashinji,Mh Julius Mtatiro,Mh Mwita waitara,Mh Godwin Molel ,Mh Bananga,Mh Patrobas Katambi,Mh Upendo Peneza ,Mh Mtera Mwampamba, Mh Pauline Gekul wote hawa na wengine wengi sana kwa sasa wapo ndani ya CCM ambapo awali walikuwa Upinzani.Lakini wamerejea na kuingia ndani ya CCM baada ya kuona kazi nzuri inayofanywa na serikali ya CCM.
Hii yote ni kutokana na kuona tumaini lililo bora na umahiri wa CCM katika kutekeleza ahadi zake na kuwa na ilani inayokidhi na kubeba mahitaji ya watu kulingana na Wakati husika na kwa kila kundi na rika..
Leo wakulima wana matumaini ya kuinuka kiuchumi kwasababu wamepewa mbolea za Ruzuku na soko la mazao yao ni la uhakika kabisa ,na hapo hapo serikali nayo hununua mazao yao kwa bei nzuri kabisa.mtu akienda hospitalini anao uhakika wa kupata matibabu mazuri,kijana anayeanza kidato cha kwanza anauhakika wa kufika chuo kikuu bila kikwazo chochote kile kwa sababu elimu ni bure mpaka kidato cha sita, huku chuo kikuu wote wenye sifa wanapewa mikopo bila shida.haki inatendeka vyema na hata Rais amekuwa akisisitiza jambo hilo na ndio maana ya kuja na falsafa ya 4R ,pamoja na kuunda tume ya masuala ya haki jinai ili kuhakikisha kuwa haki inatendeka hususan kwa watu wanaostahili kutenda haki kwa watu.
Kwa hiyo ni ngumu sana kumshawishi mtanzania mwenye akili Timamu na anayejitambua kuingia barabara kuandamana na kubomoa nchi yake kwa mikono yake.Mtanzania anajuwa akifanya kazi tu ni uhakika kabisa wakupata pesa.kwa sababu hata ardhi yenye rutuba na yenye kustawisha mazao ya kila aina ipo ya kutosha sana mpaka nyingine inabaki.tofauti na nchi nyingine ardhi tu ni shida sana kupatikana kwa mtu maskini kwa sababu ardhi yote ilishamilikiwa na watu wachache sana wenye mapesa yao na wale wanasiasa wakubwa na wa muda mrefu kutoka familia zilezile.ndio maana inawapa hasira sana wananchi wanapoona hawana hata pakulima mahindi ya kuchoma au chakula kwa watoto wao.
Naomba mniruhusu niweke kalamu chini maana naona andiko linakuwa refu tu wakati kichwani bado nina mengi sana nilitaka niwaeleze muelewe kwanini Tanzania imetamalaki kwa amani na utulivu na kwanini itaendelea kuwa Taifa lenye kutamalaki amani na utulivu kwa miaka mingi sana kwa kadri ya uhai wake.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.