Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
AminaPole sana MKUU..
Bado hujapatwaKuanguka chini inaweza kuwa ni ajali ila kulialia na kuendelea kukaa hapo chini ni choice
Changanya na za kwako...
Kabisa mkuuBado hujapatwa
Pole san@Kabisa mkuu
dollar 800 ni tsh ngapi kibongo bongoMkuu extrovert pole sana. Mimi nilipigwa kama dollars 800 hivi hadi nililetaga uzi humu 2019. Nimemkopesha jamaa toka kwa mikono yangu halafu nikimdai ananiambia nikitaka nimuue ama niende popote.
M2 na ushee ivi..dollar 800 ni tsh ngapi kibongo bongo
Kazi za usiku ndio zipi? MkuuKwenye harakati za utafutaji kupoteza ni sehemu ya maisha.
Jambo la msingi ni kupambana kupunguza risk za kupoteza.
Mimi nilifanya kazi za usiku, nikakusanya zaidi ya 1M nikaenda kulima mihogo huku Kibiti. Haikurudi hata 100.
So, ni kawaida tu.
Mo,GSM au BAKRES akipoteza 200M kwake sio kesi, ila kwako inaweza kuwa kesi.Watu tumepoteza karibu M10+ wewe icho ki M1 na nusu kinakutowa roho?? Acha kulia Lia bro, maisha Ni Vita..
HahIla mleta Uzi jina lako linaonyesha wewe ni kubwa la mandondocha , badili jina
Mambo/ shughuli zako zinaendaje kwa sasa?
Sio kama apo awali, mungu mkubwaMambo/ shughuli zako zinaendaje kwa sasa?
Wapendwa wanajf habari za usiku,
Leo akili imetulia nimeona nitoe simulizi fupi ya jinsi nilivyoweza kupoteza tsh 1.8M.
Mara baada ya kugraduate pale SUA na (BSC GM) na kushindwa kupata tempo nilijichanga katika kazi mbalimbali kama nyuzi zangu baadhi za nyuma zilivyoelezea mishemishe zangu ikiwemo shughuli za mchanga, tofali na tuition centre.
Kwa mwaka 2020 nilifanikiwa kukusanya kiasi cha shil milion 2 na laki 4 na niliamua hii pesa isikae benk tu kwavile bado naendelea kufight na mambo mengine basi niliamua kufanya biashara ya bodaboda.
Nilinunua bodaboda iliyokaribia kuisha kwa mkataba kwa tsh. 1.8M na kumkabidh mtu aendeshe kwa makubaliano tuliyoafikiana. Nilikuwa namfahamu lakini nilikua simjui sana kiundani na ndugu zake sana nilikuwa siwafahamu sana.
Nadiriki kusema nimeweza kupewa mrejesho wa siku 10 pekee na muda huu navyoongea zimepita takribani wiki 3 sijaweza kuonana wala kuwasiliana na dereva wangu, polisi nimeripoti kwa kufata taratibu lakini sioni matumaini ya kupata chombo changu, sijui mwenzangu ni mzima au ameaga dunia, nimejarbu kufatilia watu wake imeonyesha ni mhamiaji katika maeneo ya mkoa niliopo.
Nawaza sana, nimeweza kupoteza pesa niliyoitafuta kwa jasho sana ndani ya mwaka mmoja, nikiri sikuweza kulala kwa siku 2 mfululizo, Nimeamini hii dunia haina huruma.
Kuna muda nawaza ile hela bora ningeweka tu, kuna muda nawaza sana nikiona mtu anaongelea pesa tu nawaza zile pesa zangu, nimebaki na kiasi cha laki 5 kwenye akaunti yangu nawaza lini nitafika tena kwenye milioni mbili na laki 4.
Kuna muda huwa nawaza sana nikifikiria njia ngumu nilizoweza kupata hii pesa na njia rahisi ilivyoweza kupotea hii pesa, kuna muda niliona haya maisha hayana maana na kupitia huu mkasa i was so harsh, niliweza hadi kuseparate na mtu wangu, Ok ni hayo tu nimeona nishare nanyi wakubwa.
Muwe na usiku mwema.
Jambo la kushukuru, kila la kheri na mafanikio!Sio kama apo awali, mungu mkubwa
AminaJambo la kushukuru, kila la kheri na mafanikio!
Amina mkuupole sana natamani uni pm niweze kuwa karibu na wewe ili niweze kukushauri kwa karibu ila usikate tamaa up and down zipo
Nini kilitokeaMie niliibiwa kwenye daladala 6.4 M mwezi uliopita tena ya Ofisi, nikitembea nahisi moyo unachomoka nikikaa nahisi hivyo hivyo ni mateso ambayo sijawi kuyapitia toka kuzaliwa kwangu.