pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
https://www.the-star.co.ke/news/201...il-and-gas-blocs-in-kenyan-territory_c1896109 Ghafla Somalia imekuwa ndogo kama piriton. Hii ni baada ya Kenya kutishia kusitisha uhusiano wake na 'serikali' ya Somalia. Ikumbukwe kwamba rais Farmaajo ameingia madarakani kwa mgongo wa Kenya na juhudi za wakenya na KDF kuhakikisha kwamba Somalia ina serikali dhabiti ya kupambana na magaidi wa alshabaab ili malengo ya Kenya yatimie ndio vikosi vya Kenya vya kijeshi vitolewe Somalia. Zaidi ya hayo Kenya imekuwa hifadhi ya maelfu ya wakimbizi wa kisomalia kwa miongo zaidi ya miwili. Huku vikao vya rais na mawaziri na pia bunge la Somalia vikifanyiwa Nairobi, Kenya kwasababu ya ukosefu wa usalama Mogadishu.