Somalia yakana kuuza bloc za Kenya, za gesi na mafuta baharini

Somalia yakana kuuza bloc za Kenya, za gesi na mafuta baharini

pingli-nywee

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
11,923
Reaction score
13,350
https://www.the-star.co.ke/news/201...il-and-gas-blocs-in-kenyan-territory_c1896109 Ghafla Somalia imekuwa ndogo kama piriton. Hii ni baada ya Kenya kutishia kusitisha uhusiano wake na 'serikali' ya Somalia. Ikumbukwe kwamba rais Farmaajo ameingia madarakani kwa mgongo wa Kenya na juhudi za wakenya na KDF kuhakikisha kwamba Somalia ina serikali dhabiti ya kupambana na magaidi wa alshabaab ili malengo ya Kenya yatimie ndio vikosi vya Kenya vya kijeshi vitolewe Somalia. Zaidi ya hayo Kenya imekuwa hifadhi ya maelfu ya wakimbizi wa kisomalia kwa miongo zaidi ya miwili. Huku vikao vya rais na mawaziri na pia bunge la Somalia vikifanyiwa Nairobi, Kenya kwasababu ya ukosefu wa usalama Mogadishu.
 
Wakenya wanataka kuipokonya haki somalia kisa KDF yao ipo Somalia
 
https://www.the-star.co.ke/news/201...il-and-gas-blocs-in-kenyan-territory_c1896109 Ghafla Somalia imekuwa ndogo kama piriton. Hii ni baada ya Kenya kutishia kusitisha uhusiano wake na 'serikali' ya Somalia. Ikumbukwe kwamba rais Farmaajo ameingia madarakani kwa mgongo wa Kenya na juhudi za wakenya na KDF kuhakikisha kwamba Somalia ina mamlaka dhabiti ya kupambana na magaidi wa alshabaab ili malengo ya Kenya itimie ndio vikosi vya Kenya vitolewe Somalia.
Acha kichaa chako hakuna mtu anaweza kuchukua mafuta ya Somalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kichaa chako hakuna mtu anaweza kuchukua mafuta ya Somalia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hivi niulize, umebofya hiyo link ukasoma taarifa yenyewe kabla ya kurukia kwenye comment? Katika barua ambayo serikali ya Somalia imetumia wizara ya Kenya ya masuala ya nje leo hii Somalia imekana madai kwamba imeuza bloc za mafuta na gesi ya Kenya baharini. Pia wameongeza kwamba hawana mpango wowote wa kuanza shughuli zozote zile kwenye eneo hilo ambalo mgogoro kuhusu umiliki wake upo mbele ya mahakama ya U.N. yaani ICJ(International Court of Justice). Najua ulifurahia sana kusikia kwamba Kenya imeingia kwenye mgogoro na Somalia, pole sana kama matumaini yako ya kichawi yakuona damu ikimwagika haraka iwezekanavyo yameambulia patupu.
 
Serikali ya Somalia imetumia akili katika kuijibu Kenya kwenye tatizo hilo ila mwisho wa siku hakuna kubadilisha mpaka wa nchi hizo na mafuta itabaki ya Somalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za kutamausha zaidi kwa team roho mbaya. Serikali ya Somalia imesema barua inayosambaa mitandaoni ikidai kwamba wakenya wote ambao wapo Somalia wanatakiwa waondoke ni feki.
 
Serikali ya Somalia imetumia akili katika kuijibu Kenya kwenye tatizo hilo ila mwisho wa siku hakuna kubadilisha mpaka wa nchi hizo na mafuta itabaki ya Somalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama huelewi lolote kuhusu mgogoro huo wa mpaka kati ya Kenya na Somalia baharini ni bora ubaki kimya. Msimamo wa Kenya ni haki kabisa, Somalia ni ving'ang'anizi tu.
 
lwiva tuambie mipango ya Somalia kuhusu hili alafu utueleze kuhusu mipango ya Tz kuhusu kupotea kwa $1B tafadhali ukizingatia 'mind your own business ' ama kwa Kiswahili 'nyani haoni kundule '.
 
The-EAC-maritime-domain-Map-modified-from-Google-maps_Q320.jpg
Hii ni kwa wale ambao wanashabikia vitu ambavyo hawavielewi. Mipaka baharini inaenda 'in a straight line' ndio maana Pemba ipo Tz na sio Kenya. Madai ya Somalia ni ya kinafik na wanafahamu vizuri kwamba mahakama itakapotoa maamuzi haitakuwa upande wao.
 
Serikali ya Somalia imetumia akili katika kuijibu Kenya kwenye tatizo hilo ila mwisho wa siku hakuna kubadilisha mpaka wa nchi hizo na mafuta itabaki ya Somalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali ya Somalia haijatumia hekima yeyote maanake wao wenyewe ndio walipeleka mgogoro huu wa mpaka kwenye mahakama ya kimataifa ICJ. Wanafahamu vizuri kwamba mgogoro kama huu ukiwa mbele ya mahakama eneo hilo halifai kuvurugwa au kutumiwa kwa njia yeyote ile na mtu yeyote yule hadi pale ambapo mahakama itatoa maamuzi yake. Kenya ipo sawa kwenye hili suala, kisheria na kidiplomasia pia.
 
Back
Top Bottom