Somalia yamfukuza balozi wa Kenya na kumuondoa balozi wao Nairobi

Somalia yamfukuza balozi wa Kenya na kumuondoa balozi wao Nairobi

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617

Somalia yamuita balozi wake wa Kenya mzozo ukitokota


Na BENSON MATHEKA
NAIROBI, Kenya


SOMALIA imemfukuza balozi wa Kenya nchini humo huku mzozo mpya katika ya nchi hizi mbili ukitokota.

Mnamo Jumapili, serikali ya Somalia ilimuita balozi wake Kenya Mohamoud Ahmed Nur ‘Tarzan’ kurudi Mogadishu kwa mashauriano na ikamuagiza balozi wa Kenya Lucas Tumbo kuondoka.

Somalia inalaumu Kenya kwa kushinikiza viongozi wa jimbo la Jubaland kukataa makubaliano yanayohusu uchaguzi unaotarajiwa mwezi huu.

Kwenye mkataba huo uliotiwa saini Oktoba, pande zote zilikubaliana raia wa Somalia kuchagua wabunge moja kwa moja.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Somalia Mohammed Ali Nur, alilaumu Kenya kwa kusukuma kiongozi wa Jubaland Mohamed Ahmed Madobe kukataa mfumo huo wa uchaguzi.

“Somalia inasikitishwa na hatua ya serikali ya Kenya ya kuingilia masuala ya ndani na kisiasa ya serikali ya majimbo ya Jamhuri ya Somalia inayoweza kuwa kuzingiti kwa uthabiti, usalama na maendeleo ya eneo nzima,” Bw Nur alidai.
“Serikali ya Somalia imetambua kuwa serikali ya Kenya inamwekea presha Rais wa jimbo la Jubaland, Bw Ahmed Mohamed Islan Madobe kwa lengo la kuendeleza ajenda yake ya kisiasa na kiuchumi Somalia,” alidai bila kutoa ushahidi wowote.

Madai hayo yanajiri siku chache baada ya Somalia kufungua ubalozi wake Nairobi uliofungwa nchi hiyo ilipokubwa na ghasia nayo Kenya ikafungua upya jengo mpya la ofisi za ubalozi wake jijini Mogadishu iliyojenga kuanzia 2018.

Somalia ilimfuta waziri wa mashauri ya kigeni Ahmed Isse Awad, aliyefungua ubalozi wake Nairobi.

Hii ni mara ya pili ya Somalia na Kenya kuzozana mwaka huu.

Mnamo Februari 2020 Kenya ilimuita balozi wake kurudi Nairobi kwa mashauriano na kumuagiza Tarzan kuondoka Nairobi. Hii ilitokea Somalia ilipojaribu kuuza sehemu ya bahari yenye utajiri wa mafuta ambayo nchi hizi mbili zinazozania.

Mnamo Jumapili, katibu wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Kenya Macharia Kamau alisema kwamba hatua ya Somalia ya kumuita nyumbani balozi wake Kenya inasikitisha.


====

MY TAKE: Wakati Tanzania tukiongeza ushirikiano na Msumbiji katika vita dhidi ya ugaidi, Kenya ndio kwanza inakua ni chanzo cha machafuko na mafarakano ndani ya Somalia.

Kenya ni nchi ambayo kwa muda mrefu sana imekosa uongozi bora na makini, matatizo yanayoikumba Kenya ni kutokana na kukosekana uongozi bora.

Jeshi la Tanzania limeanza kuingia Msumbiji ili kuwasaka na kuwaangamiza Magaidi waliokua wameshikilia sehemu kubwa ya kaskazini mwa Msumbiji, lakini kutokana na ushirikiano wa karibu na serikali na wananchi wa Msumbiji, jeshi letu limefanikiwa kukomboa maeneo yote na muda si mrefu hao magaidi watabaki katika vitabu vya kumbukumbu kama M23
 
Serikali ya Somalia imesema kuwa imemuita nyumbani balozi wake nchini Kenya Mohamud Ahmed Nur Tarzan, na kuishutumu nchi hiyo kwa kuingilia siasa za nchi yake.

Somalia pia imemtaka balozi wa Kenya nchini Somalia kufunga virago "kwa ajili ya majadiliano".

Somalia imeishutumu Kenya kwa kushinikiza serikali ya Jubbaland kukataa makubaliano ya uchaguzi yaliofikiwa Septemba 17, katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwezi ujao.

"Serikali ya Somalia ilichukua uamuzi huo kulinda eneo lake la utawala baada ya kujitokeza kuwa Kenya inaingilia kimaksudi masuala ya Somalia eneo la Jubbaland," Mohamed Ali Nur, Waziri wa mambo ya nje wa Somalia amesema katika taarifa iliyotolewa.

"Serikali] ya Somalia imeonesha kusikitishwa kwake na serikali ya Kenya kwa kuingilia moja kwa moja masuala ya ndani ya siasa za Somalia hatua ambayo inaweza kuchangia ukosefu wa uthabiti, usalama na maendeleo kwa eneo zima,” taarifa hiyo imesema.

Kenya inaunga mkono utawala wa Ahmed Mohamed Islam maarufu kama "Madobe" huko Jubbaland, kwasababu ya maslahi yake ya kiusalama na kieneo.

Chanzo: BBC
 
Nchi ambayo sisi ndio tulihost serikali yao ya kwanza hapa Nairobi sasa inaona imemea pumbu sasa inataka kupigana na baba yake? Kha! Watoto siku hizi hawaheshimu wazazi wao.
Tulimwaga damu kwa kuwakomboa Msumbiji lakini hatuwanyanyasi wala kujaribu kuwapa amri, tunaishi nao kama ndugu zetu, ninyi hamna nidhamu ya maisha, mtagombana na majirani wenu wote.
 
Kenya wanajikuta wao Ni USA ya Africa, Mara huku kwetu wapandikize Kigogo...Mara Kule sijui nani hivyo Sana Hawa watu.
mtajuaje sisi ni superpower tusipowacontrol kama gari ya remote?
 
mtajuaje sisi ni superpower tusipowacontrol kama gari ya remote?

tatizo mnalazimisha hadhi ambayo hamna,ndio maana mambo yanakuwa magumu.

sasa somalia ni wa kuwakazia kweli!!!
 
Nchi ambayo sisi ndio tulihost serikali yao ya kwanza hapa Nairobi sasa inaona imemea pumbu sasa inataka kupigana na baba yake? Kha! Watoto siku hizi hawaheshimu wazazi wao.
Hata sio hivyo pekee, serikali zao nyingi zimeundwa pale Nairobi.
 
Kumbe FRELIMO nikitengo cha Tpdf ?😂😂.....
Huyu jamaa huwa anatudanganya eti Tanzania ndio ilikomboa Mozambique. Anadhani hatujui kama Samora Machel ndio waliikomboa Mozambique? Frelimo ndio iliikomboa Mozambique
 
Back
Top Bottom