Kilichowaudhi upande wa somaliland ni Barre (late) kuishambulia wakati ule
Wewe unaonaje kuachana au kuwa nchi moja ipi bora
Maana upande mwingine hawataki kuwasikia kabisa Mogadishu
Kwa kweli inasikitisha sana maisha yao yalivyoharibika
Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Siad Barre aliipindua Serkali ya kiraia na akalivunja Bunge halafu akatangaza makubaliano yote yaliyifikiwa baina ya nchi hizo mbili ni Haramu wabunge wengi wa Somaliland walifia magerezani sababu wakiachiwa watahoji.
Wabunge wa Somalia walikuwa wanasamehewa na kupewa ukubwa kwenye mashirika ya Umma
Akaanzisha Ujamaa na kujitegemea na miradi ya kufutilia mbali umiliki mali wa raia haswa Somaliland
Akaanza mradi wa kuwatoa watu kusini na kuwahamishia Kaskazini Somaliland
Wakati huo wananchi wa Somaliland wengi wakaanza Kuikimbia Nchi yao
Siad Barre akaanzisha harakati za kuwakomboa watu wote wanaoongea Kisomali
Akaanzisha Shifta Movement ili kuivamia Kenya
Wakati huo huo Barre akawaalika Warrusi ili waje kufundisha Ukomunisti,Warussi kwa furaha kubwa wakaenda Mogadishu na kumwaga Silaha za kila aina kasoro nyukilia
Askari wa Barre wakapewa Mafunzo ya Mapigano ya nchi kavu na Anga
Barre akasema Tuvamie Ethiopia kwanza halafu kenya baadae 1977 Majeshi ya Barre yakaingia Ethiopia alichukua vijana wengi kutoka Somaliland na kuwatanguliza mbele.
Barre alikuwa anacheza gemu ya mauaji ya "Kimbari"kiaina wakatu huo Jeshi la Ethiopia lilikuwa linapambana na vikundi vya waasi wanaotaka kujitenga ili kuikomboa ERITREA ambayo ilikuwa Chini ya Ethiopia.
Majeshi ya Somalia yalikutana na Upinzani mdogo yakawa yanatwaa mji hadi mji
Raisi wa Ethiopia wa wakati huo Mangistu Haile Mariam akaenda Urusi kuomba msaada
Urussi ikamwambia Barre aindoe majeshi yake ndani ya Ethiopia Barre akakaataa katakata kama tunavyojua tabia ya hawa wasomali wa kusini.
Urussi ikaongea na Cuba ya Fidel Castro na Cuba ikatuma askari 15000 na silaha nzito
Barre akafukuza aAskari na raia wote wa Kirusi kutoka Somalia.
Urussi nayo ikatuma Makomando 3000 kuisaidia Ethiopia
Barre akala kichapo cha Haja hapohapo Wale askari wa Somaliland wakapata fursa wakaongea na Mangistu Haile Mariam na wakajiandaa jeshi la Somalia likarudishwa hadi Mpakani
Askari wenye Asili ya Somaliland wakajipanga na kuanzisha mapambano ya kuwatoa askari wa Mogadishu
Siad Barre akapata fursa ya kuwamaliza Raia wa Somaliland takeiban watu Laki tano waliuwawa
1988 askari wa Siad Barre wakawa wameshindwa na kujisalimisha Mkuu wa majeshi ya Somaliland akaongea na mtu ambaye alikuwa anaogopewa na Siad Barre huyo jamaa alikuwa anaitwa General Mohamed Farah Aidid wakati huo Barre alimfanya Balozi nchini India.
Gen Farah Aidid akawachukua wale askari waliojisalimisha na kushuka nao Mogadishu
Somaliland ikatangazia ulimwengu kuwa imejitoa kwenye Project ambayo iliwaletea Vifo ubakwaji na kila aina mateso.
Vita vimekuwa vikiendelea huko Somalia hadi wa leo.