Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Pongezi tele ziwafikie Wakenya. Hakika kifikra mmetuzidi mbali sana sisi Watanzania.
Pole nyingi pia kwa majeruhi wote wa matumizi ya nguvu ya polisi, wale waliopoteza maisha, pamoja na wapendwa wao.
Tumeona jinsi ambavyo Wakenya wanatambua haki zao za kikatiba.
Maandamano waliyoyafanya na watakayoyafanya, si hisani ya William Ruto na chama chake.
Na ndo maana hujawasikia wakisema ‘Ruto karuhusu au kapiga marufuku’ maandamano.
Hawezi kufanya hivyo kwa sababu hiyo ni haki ya kikatiba ya Wakenya wote.
Hiyo haki inatolewa na katiba. Siyo William Ruto na watu wake.
Katiba yao inaruhusu watu kuandamana na kuipinga serikali yao au kupinga jambo jingine lolote lile.
Huku kwetu mara nyingi tumewasikia majuha wakisema ‘Samia karuhusu mikutano ya kisiasa’, karuhusu hiki na kile!
Huo ni uongo, ujinga, na ujuha uliopitiliza.
Haki za kikatiba si hisani ya Samia wala CCM.
Inavunja moyo sana kuona tunaongozwa na watu walio mbumbumbu.
Ila kinachosikitisha zaidi ni jinsi Watanzania walio wengi walivyo mambumbumbu, wajinga, waoga, na majuha!
Kenya ya leo Hakuna mtu mwenye akili timamu atayetoa kauli ya kwamba Rais Ruto karuhusu au kakataza maandamano!
Jana na leo Ruto kalaaniwa vibaya sana kwa kutaka kulitumia jeshi la Kenya dhidi ya Wakenya wanaotekeleza haki yao ya kikatiba.
Kila kona amelaaniwa.
Ili na sisi tuwe walau kama Wakenya, labda ni miaka 100 ijayo.
Heko kwenu majirani. Mmeufikisha ujumbe na Ruto kaupata na amekubali.
View: https://youtu.be/txbCv_K0lPA?si=aZUE20fuN-UxK1zB