Somo kwa CCM: Unaweza kulazimisha kupata madaraka lakini sio kupata watu

Somo kwa CCM: Unaweza kulazimisha kupata madaraka lakini sio kupata watu

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Somo kwa CCM: Unaweza kulazimisha kupata madaraka lakini sio kupata watu. kuajiri kwa kuhonga ajira, undugu, rushwa na wizi wa kura una mwisho wake.

Tuna serikali na chama cha CCM ambacho hakiendani na hali halisi ya nchi ilivyo. wakati wizi, rushwa, undugu, utekaji unaendelea ndiyo hivyo hivyo watanzania wengi mnazidi kuwapoteza sasa imefika wakati upinzani unapendwa na watanzania kuliko CCM .
 
Kwenye siasa za kweli ambapo watu hawabebwi na malori, trekta au daldala

Bloemfontein, South Africa
TAREHE 28 APRIL 2026 SIKU MUHIMU YA KIHISTORIA YA FREEDOM DAY YA SOUTH AFRIKA RAIA WASUSA KUFIKA UWANJANI
1777561435330.jpeg
1777561514640.jpeg


View: https://m.youtube.com/watch?v=1-EQf6jhtFA

Siku ya kuadhimisha Kumalizika Ubaguzi, iligeuka kuwa shubiri kwa chama cha kina Nelson Mandela, Oliver Tambo, Mbeki, Sobukwe, Luthuli waasisi wa ANC wakati wa Rais Cyril Ramaphosa akipokelewa na aibu ya kususiwa na viti vitupu vya kushangaza huko mjini Bloemfontein jimbo la Free Stste . Kile kilichokusudiwa kuwa sherehe ya kitaifa yenye nguvu kilizua maswali mazito kuhusu hisia za umma na kutengana kisiasa chama cha ukombozi cha ANC.

Lakini badala ya kushughulikia jambo lililo wazi, chawa ktk serikali ya umoja wa kitaifa GNU Bw. Gayton McKenzie wa chama cha PA - Patriotic Alliance alijitokeza kumtetea rais Cyril Ramaphosa wa chama cha ANC, akipuuza kile ambacho wengi wanakiita aibu iliyo wazi.

Wakosoaji hawakubaliani nacho - na Waafrika Kusini wanauliza: je, hii ilikuwa ni mipango mibaya tu, au ishara kubwa zaidi ya kuchanganyikiwa kunakoongezeka? Je, hii ndiyo hali halisi ya nchi hivi sasa? Na kwa nini viongozi wanakataa kukubali hilo?
 
28 April 2026
Bloemfontein
Republic of South Africa

FREEDOM DAY YAGEUKA AIBU KWA CHAMA CHA ANC SAUZI, RAIA WASUSA KUFIKA UWANJANI


View: https://m.youtube.com/watch?v=CwUDgnJQWXA
Katika mahojiano haya yenye nguvu ya mtaani kutoka Bloemfontein, wakazi wa eneo hilo wanaelezea sababu zao za kweli za kutohudhuria tukio la Rais Cyril Ramaphosa kwenye uwanja huo siku ya Freedom Day 28 April 2026 ikiadhimisha kumalizwa ubaguzi.

Kuanzia ukosefu wa ajira na kukatishwa tamaa na utoaji wa huduma hadi kukatishwa tamaa na uongozi mbovu na ahadi zisizotekelezwa, watu wanazungumza waziwazi kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo kila siku.

Video hii inawapa raia wa kawaida jukwaa la kutoa maoni yao kuhusu siasa, utawala, na uhalisia wa maisha nchini Afrika Kusini. Sauti zao zinaonyesha wasiwasi wa wengi wanaohisi hawasikilizwi pia kudharauliwa na chama cha ukombozi kikichoondoa ubaguzi .

Tazama, sikiliza, na ujiunge na mazungumzo. Je, unakubaliana na watu wa Bloemfontein?
 
CCM, ANC, FRELIMO, MPLA vyama dola muda wenu umekwisha. Maandamano ya Mozambique 2024, Maandamano ya MO29, 2025 Tanzania ni jumbe tosha.

Maandamano ya March to March April 2026 South Africa yanaonesha vijana hawakubaliani tena na vyama kongwe vinavyodai vilileta uhuru ktk nchi zao

ANC YAKATALIWA NA RAIA SIKU YA FREEDOM DAY 28 APRIL 2026
Mjini Bloemfontein
Jimbo la Free State
Republic of South Africa


View: https://m.youtube.com/watch?v=ypsOeuO-RH0

 
Hivi KM wa sisiemu wa sasa anasimamia nini? Maana hasikiki
 
Watawala wa ccm wana kitu cha kujifunza kwa Lissu. Jamaa kwenye mikutano yake ya kisiasa hatumii malori ya polisi kupeleka watazamaji, hatoi rishwa ya aina yoyote ile, hatembei na wasanii wa kukodi wa bongo fleva, halazimishi watumishi wa umma na wanafunzi, mabalozi kupita nyumba kwa nyumba, nk. Na bado watu wanajaa na kumsikiliza kwa umakini!

MamaSamia2025 remember that, a good leader is the one who has followers, and not Chawaz.
 
CCM, ANC, FRELIMO, MPLA vyama dola muda wenu umekwisha. Maandamano ya Mozambique 2024, Maandamano ya MO29, 2025 Tanzania ni jumbe tosha.

Maandamano ya March to March April 2026 South Africa yanaonesha vijana hawakubaliani tena na vyama kongwe vinavyodai vilileta uhuru ktk nchi zao

ANC YAKATALIWA NA RAIA SIKU YA FREEDOM DAY 28 APRIL 2026
Mjini Bloemfontein
Jimbo la Free State
Republic of South Africa


View: https://m.youtube.com/watch?v=ypsOeuO-RH0



April 28 2026

Vijana weusi wa Afrika Kusini sasa wanaikataa ANC urithi aliouacha Nelson Mandela


View: https://m.youtube.com/watch?v=ii4rG_yejA8
Nelson Mandela alikuwa ametangazwa kama nembo ya kimataifa, na anapendwa na wengi mithili ya Julius Nyerere.

Wengi wao wanaoendelea kumpenda kumuona kama Nelson Mandela ni messiah na kuwa ANC ni wakombozi , Wengi wao ni wale ambao hawajui lolote kuhusu Afrika Kusini.

Hata hivyo, urithi wa Nelson Mandela kupitia chama chake kongwe cha ANC akiwa nyumbani, urithi wake unazidi kuchukiwa na kukosa umaarufu miongoni mwao Vijana Weusi wa Afrika ya Kusini

Sababu kibao za chama hiki kimojawapo kongwe barani Afrika kilichoasisiwa rasmi mwaka 1912 na kisha 1994 kupitia Nelson Mandela kuwezesha ubaguzi wa kisiasa, kielimu, huduma za kijamii kumalizwa na hivyo Afrika ya Kusini kuwa taifa lisilo na sera ya ubaguzi lakini miaka 32 baadaye yaani 2026 vijana wameamua kukipinga vikali chama cha ANC. vyombo vyake kama polisi, uhamiaji kutokana na kushindwa kuleta matarajio yaliyotegemewa mwaka 1994

TOKA MAKTABA :

 
Watawala wa ccm wana kitu cha kujifunza kwa Lissu. Jamaa kwenye mikutano yake ya kisiasa hatumii malori ya polisi kupeleka watazamaji, hatoi rishwa ya aina yoyote ile, hatembei na wasanii wa kukodi wa bongo fleva, halazimishi watumishi wa umma na wanafunzi, mabalozi kupita nyumba kwa nyumba, nk. Na bado watu wanajaa na kumsikiliza kwa umakini!

MamaSamia2025 remember that, a good leader is the one who has followers, and not Chawaz.
Huyo uliemtag ni kuku mmoja tuu ambae hata balozi wa nyumba kumi mtaani hamtambui
 
Back
Top Bottom