Somo kwa magicfm - morning magic, kupaka rangi

Somo kwa magicfm - morning magic, kupaka rangi

Miwatamu

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2012
Posts
1,450
Reaction score
489
Mahsusi kwa Orest Kawawu, Merry Edward na Salum Mkambala.

Binafsi naomba niseme kuwa kwa kipindi kirefu nimekuwa mdau wenu sana katikakusikiliza kipindi hicho, ila katika siku za hivi karibuni mmekichakachua sana na kujikuta mkitumia kipindi hicho kama cha ENTERTAINMENT wakati ni kipindi mahsusi kwa watu kuchambua masuala mbalimbali ya mstakabali mzima wa nchi yetu.

kutokana na matangazo ya biashara kuwa mengi, sasa hata muda wa wasikilizaji kupiga simu na kutoa michango yao umekuwa mfupi sana.

Ni kweli kuwa matangazo nidiyo tegemeo kubwa sana la chanzo cha mapato kwa vyombo vya habari, ila sasa uwepo mpangilio ambao hautawaboa au kuwanyima nafasi wachangiaji. ukiangalia siku hizi matangazo tu kabla ya kipindi cha KUPAKA RANGI yanachukua dk30 au zaidi, simu za wasikilizaji hazizidi 6. Sasa hapo uwiano upo wapi?

Msije mkafikiri kuwa ongezeko la wasikilizaji wa kipindi hicho ni kwa kupenda matangazo, bali kwa kuwa wanapata nafasi ya kutoa dukuduku zao kwa mstakabali wa taifa lao.

TAFAKARINI.
 
duuh umekosea jukwaa mkuu hebu peleka kule kwa CELEBRITIES
 
Back
Top Bottom