Somo la 5: Faida ya pili ya uwekezaji kwenye soko la hisa — Gawio (dividends)

Somo la 5: Faida ya pili ya uwekezaji kwenye soko la hisa — Gawio (dividends)

Joined
Aug 26, 2022
Posts
64
Reaction score
124
📘

🔁 Katika somo letu lililopita, tulielewa vizuri dhana ya ongezeko la mtaji (capital gain) — faida unayopata pale bei ya hisa inapopanda.

📍 Leo, tunazungumzia faida ya pili: Gawio.

1️⃣ Gawio ni nini?
Gawio ni sehemu ya faida ya kampuni inayogawiwa kwa wanahisa wake, kawaida mara moja au mbili kwa mwaka.
Ni kama shukrani ya kampuni kwa kukuamini na kuwekeza mtaji wako kwao.

🧾 Mfano: Kama una hisa 1,000 za kampuni fulani, na kampuni hiyo itoe gawio la TZS 100 kwa kila hisa, utapokea TZS 100,000 bila kuuza hisa zako hata moja!

2️⃣ Mifano Halisi ya Magawio kwa Mwaka Huu (2024/2025)
Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni kutoka DSE:

■ CRDB Bank: TZS 65 kwa kila hisa — Dividend Yield: 8.32%
■ NMB Bank: TZS 428.85 kwa kila hisa — Dividend Yield: 6.81%
■ Mkombozi Bank: TZS 92.40 kwa kila hisa — Dividend Yield: 14.44%
■ TCC (Tanzania Cigarette Company): TZS 850 kwa kila hisa — Dividend Yield: 5%
■ Twiga Cement (TPCC): TZS 600 kwa kila hisa — Dividend Yield: 10.9%
■ SWISSPORT: TZS 70.72 kwa kila hisa — Dividend Yield: 5.89%
■ TBL (Tanzania Breweries): TZS 818 kwa kila hisa — Dividend Yield: 7.86%

💡 Hii inaonyesha kuwa hata usipouza hisa zako, bado unaweza kupata kipato cha mara kwa mara.

3️⃣ Gawio si tu juu ya namba kubwa – ni juu ya Dividend Yield
Watu wengi hupotoshwa na ukubwa wa gawio tu bila kuangalia dividend yield — yaani, asilimia ya gawio ukilinganisha na bei ya sasa ya hisa.

Mfano:
■ Kampuni A inaweza kulipa gawio la TZS 600, lakini bei ya hisa ni TZS 6,000 — yield ni 10%.
■ Kampuni B inalipa TZS 850, lakini bei ya hisa ni TZS 17,000 — yield ni 5%.

👉 Hivyo, licha ya B kutoa gawio kubwa kwa namba, A inakupa faida bora zaidi ukilinganisha na kiasi ulichowekeza.

4️⃣ Kwa nini Gawio ni Muhimu kwa Mwekezaji?

■ Ni chanzo kizuri cha mapato (cash flow).
■ Unapata bila kuuza hisa zako: Unaendelea kumiliki hisa zako na bado unalipwa.
■ Unaweza kuwekeza tena: Unaweza kutumia gawio lako kununua hisa zaidi.

5️⃣ Mikakati Mizuri ya Gawio.

■ Wekeza kwenye kampuni zenye rekodi nzuri ya kutoa gawio kila mwaka pia yenye ongezeko la faida.
■ Chunguza dividend yield, si tu kiwango cha gawio.

Zingatia:

Kama wewe ni mwekezaji mpya au unataka kuboresha taarufa zako hakikisha unajaza form kwa ajili ya kuhakiki taarifa zako— form hizo zinapatikana kwenye tovuti za kampuni husika/madali wa soko la hisa au DSE.

🔚 Hitimisho
Gawio ni kama mti unaozaa matunda kila msimu — bila kukata mti, bado unaendelea kufaidi. Ni njia salama ya kujenga kipato endelevu, hasa kama umejikita kwenye kampuni zenye mwenendo mzuri kibiashara.

❓Swali la siku:
Ukipokea gawio la TZS 200,000 leo, ungewekeza tena au ungetumia kwa kitu gani?

Tuambie hapa chini! 👇

Usisahau kufatilia somo lijalo 🫵
 
Somo zuri sana.
sasa somo la 1 hadi la nne nitayapataje?
Nashauri ungefanya mwendelezo wa masomo yako katika a single thread.
 
Sawa nitafanya hivyo, lakini ukiangalia kwenye posts zangu utaona mtiririko mzima.
 
Back
Top Bottom