Somo la historia ulilosoma miaka ya nyuma, ukiwa shule ya msingi mpaka sekondari na wengine mpaka chuo; limekusaidiaje katika kujikimu kimaisha?

Somo la historia ulilosoma miaka ya nyuma, ukiwa shule ya msingi mpaka sekondari na wengine mpaka chuo; limekusaidiaje katika kujikimu kimaisha?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Ukitumia somo la historia, kama somo la kukupa mbinu za kupambana kimaisha, linaweza kukusaidia.

Ebu fikiria ukoloni ulivyoingia Afrika, kwa kutumwa wajumbe mbalimbali kuja kufanya utafiti na kuangalia namna ya kututawala pamoja na kumiliki mali zetu.

Na wengine kuuzwa kama mifugo ili kwenda kuwafanyia kazi wakoloni. Ile inatafsiri, ulimwengu tuliopo ili ufanikiwe lazime unyonyaji uwepo iwepo. Tajiri anamnyonya masikini ili awe tajiri zaidi.

Kwa elimu ya darasa la saba niliyonayo na mbobezi wa historia ya kina Vasco da gama, natumia historia kwenda huko kijijini ili kuwalaghai waniuzie nafaka, mifugo n.k kwa bei nafuu ili niwaletee mjini niwauzie kwa faida kubwa. Hii kitaalamu cha kihistoria, tunaiita 'exploitation'.

Hii ina maana, ukitumia somo la historia vizuri unaweza ukajiajiri n.k

Je, wewe unatumiaje somo la historia katika harakati zako za maisha?​
 
Naomba uniache tu nahisi kuchanganyikiwa hapa kila nikishtuka usiku naamka kukemea pepo la elimu niliyokaririshwa "ZWANGENDABA MPUTAMASEKO"
 
Kingereza muhimu by Mangungo
Nataka nitumie hiyo mbinu,niingie hukousukumani ndani ndani, ambapo wakiona gari wanahisi wameona tembo,ili nifanye nao mikataba ya kilaghai niweze kununua gunia la mahindi kwa 10,000​
 
Naomba uniache tu nahisi kuchanganyikiwa hapa kila nikishtuka usiku naamka kukemea pepo la elimu niliyokaririshwa "ZWANGENDABA MPUTAMASEKO"
Unatakiwa uende huko ndani ndani ukamiliki kijiji,kiwe kinakulimia mazao 😀
 
Kujua tulikuwa Baboons.

Historia Kama ilivyo vifurushi vya uongo vinavyosimulia vitu visivyokuwepo vikisimuliwa na mtu ambae hakuwepo.

Tungejua Historia yetu tusingeletewa Mungu mzungu Wala Mungu Mwarabu kwenye mabrifukesi

Kama yanayotokea Leo mengi yamejaa uongo , Je Historia ni mbaya kiasi gani ?
HIS+STORY.
 
Back
Top Bottom