Somo la historia ya Tanzania kuanza kufundishwa Machi 2021

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Somo la historia ya Tanzania litaanza kufundishwa katika shule za msingi kuanzia Machi, 2021 baada ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kukamilisha uandishi wa rasimu na mihtasari.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilolitoa wakati akiwaapisha mawaziri Desemba 9, 2020 Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Katika hafla hiyo Magufuli alimtaka Waziri wa Elimu nchini, Profesa Joyce Ndalichako kuanzisha somo la historia ya Tanzania na liwe la lazima kusoma.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumanne Februari 23, 2021 mwenyekiti wa bodi ya TET, Profesa Bernadeta Killian amesema baada ya kukamilisha uandaaji wa rasimu za mihtasari, shughuli inayoendelea ni kukamilisha kazi ya uandishi wa vitabu inayotarajiwa kumalizika Machi.

“Kutokana na mkakati tuliouandaa, shule za awali hadi darasa la saba masomo yataanza mwezi wa tatu na sekondari wataanza Mei. Vitabu vinaendelea kuandaliwa kwa uharaka na makini.”

“Katika utaratibu mzima wa uandishi wa muhtasari na vitabu TET hufuata hatua mbalimbali, moja ni kuwashirikisha wadau wa elimu, hivyo tumeandaa mkutano wa wadau. Baadhi yao ni taasisi za elimu ya juu, vyuo vya ualimu, asasi zisizo za kiserikali, wizara, mashirika mbalimbali na watekelezaji wa mwisho wa mtaala ambao ni walimu,” amesema.

Profesa Killian amesema wadau wengine ni taasisi za dini na viongozi wa kijadi wakiwemo machifu na mangi kutoka mikoa mbalimbali Tanzania Bara na wataalamu wa historia kutoka Zanzibar na chama cha historia Tanzania.

CHANZO: Mwananchi
 
Hakuna cha Historia yoyote sema wanataka kuweka tu bandiko la kusema 2015 Mpaka, alikuwepo Kiongozi aliyejenga SGR na Rufiji Dam.
 
Hahaha aisee..
 
Kama alivyosema hatuhitaji katiba mpya..basi na sisi hatuhitaji historia..kwanza lengo la kuanzisha zinajulikana sio historia ya nchi bali ni histori ya malaika mkuu...

Nchi inahitaji masomo kama ya kilimo,ufundi na ujasirimali,historia haitoleta hela kwenye maisha yetu na watoto wetu.

Mfumo wa elimu tunauchezea sana..sidhani kama tutafika popote kwa namna hii.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mambo yanakwenda kasi sana. Mtaala wake sijui umeandaliwa lini. Vitabu kwa ajili ya wanafunzi na kiongozi cha mwalimu sijui vimeandaliwa lini, vipi kuhusu ushiriki wa wadau wa elimu na maoni yao.
Anyway, machi tukutane darasani
 
Hivi naweza rudia shule purposely kwa ajili ya kusoma hili somo pekee?
 
Nakumbuka shule moja ya secondari, mwl wa history alinilazimisha kusoma history nikagoma alinitandika viboko hadi mkebe ukabonyea ulikuwa mfuko wa nyuma wa suluari, sijui kama leo nitamwambia mwanangu nimsaidie kujifunza hilo somo kwa upendo.
 
Ndalichako ni waziri wa elimu aliyefeli bora wangerudisha somo la agriculture, au wakaongeza somo la science and technology na sio utopolo wa historia
 
Somo la historia ya Tanzania litaanza kufundishwa katika shule za msingi kuanzia Machi, 2021 baada ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kukamilisha uandishi wa rasimu na mihtasari.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilolitoa wakati akiwaapisha mawaziri Desemba 9, 2020 Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Katika hafla hiyo Magufuli alimtaka Waziri wa Elimu nchini, Profesa Joyce Ndalichako kuanzisha somo la historia ya Tanzania na liwe la lazima kusoma.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumanne Februari 23, 2021 mwenyekiti wa bodi ya TET, Profesa Bernadeta Killian amesema baada ya kukamilisha uandaaji wa rasimu za mihtasari, shughuli inayoendelea ni kukamilisha kazi ya uandishi wa vitabu inayotarajiwa kumalizika Machi.

“Kutokana na mkakati tuliouandaa, shule za awali hadi darasa la saba masomo yataanza mwezi wa tatu na sekondari wataanza Mei. Vitabu vinaendelea kuandaliwa kwa uharaka na makini.”

“Katika utaratibu mzima wa uandishi wa muhtasari na vitabu TET hufuata hatua mbalimbali, moja ni kuwashirikisha wadau wa elimu, hivyo tumeandaa mkutano wa wadau. Baadhi yao ni taasisi za elimu ya juu, vyuo vya ualimu, asasi zisizo za kiserikali, wizara, mashirika mbalimbali na watekelezaji wa mwisho wa mtaala ambao ni walimu,” amesema.

Profesa Killian amesema wadau wengine ni taasisi za dini na viongozi wa kijadi wakiwemo machifu na mangi kutoka mikoa mbalimbali Tanzania Bara na wataalamu wa historia kutoka Zanzibar na chama cha historia Tanzania.

CHANZO: Mwananchi
Tupa kule!
 
Back
Top Bottom