Somo la namna ya kufikiria lifundishwe shuleni na vyuoni

Somo la namna ya kufikiria lifundishwe shuleni na vyuoni

Utakijuaje kitu bila kukielewa?

Utathibitisha vipi kwamba huyu mtu anakijua hiki kitu ila hajakielewa?
Unaweza kutaja aina ya magari ambayo huwezi kuyaendesha, Kuna anayeweza kuyaendesha lakini hawezi kutatengeneza yakiharibika. Hivyo kujuwa na kuelewa nitofauti. Kujua Ni kufahamu, unaweza kufahamu jengo liliko lakini huelewi linavyotumika.
 
Safi sana.
Kwa kuongezea hapo mtu anayekariri yeye ataangalia rangi ya chama na kuweka tick kwenye viboksi vyote vyenye rangi ya chama hicho bila kuchambua ufanisi wa hao wagombea.
Exactly, Kuna mtu akisikia CCM anafikiri Ni ileile ya Nyerere, kumbe katikati hapo yaliingia mambo ya kupakia twiga mzima kwenye ndege chini ya CCM hiyohiyo iliyokuwa ya Nyerere zamani. Critical
Kwa mfano mtu anayekariri anajua kwamba magufuli anajenga flyovers,treni za mwendokasi na barabara. Lakini mtu aliyeelewa atakwambia kodi zetu zinajenga flyovers,treni za mwendokasi,barabara ila magufuli amejitahidi kusimamia kodi zetu.

UMEELEWA SASA TOFAUTI YA KUKARIRI NA KUELEWA NDUGU?
Exactly!!, tena ukimkuta mtu anakata vyuma vya flyover polisi watamkuta umeshamng'oa meno kwa mikono yako.

Ndio maana kule Ulaya mtu akikwepa Kodi atachongewa "TRA"na raia yeyote atakaemgundua
 
Kwa mfano mtu anayekariri anajua kwamba magufuli anajenga flyovers,treni za mwendokasi na barabara. Lakini mtu aliyeelewa atakwambia kodi zetu zinajenga flyovers,treni za mwendokasi,barabara ila magufuli amejitahidi kusimamia kodi zetu.

UMEELEWA SASA TOFAUTI YA KUKARIRI NA KUELEWA NDUGU?
Kujua na kuelewa kuna tofauti gani?
 
Na somo LA kubeti lifundishwe mashuleni kama alovyoshauri Rungwe
 
Kufikiria Ni taaluma Kama zilivyo taaluma nyingine. Mzazi asiyejuwa kufikiria itamfanya kila njia kumzuia mtoto wake pia asiweze kufikiria. Wazazi wa hivyo wanakuja na ACHA, ACHA, ACHA nyingi kwa watoto wao.

Mara nyingi watoto wanaokuwa bila wazazi au na mzazi mmoja tu (mama) huwa na uwezo mkubwa wa kufikiria kwakuwa walikutana na ACHA chache Sana utotoni
 
Kuelewa kuko ndani kujua
Unaweza kujua kitu lakini usikielewe, ila ukielewa kitu moja kwa moja unakijua.
Lakini kujua hakuko ndani ya kuelewa. Mtu anapotanguliza neno "nadhani/I think" maana kuelewa kwake Jambo hilo Kuna mashaka sio 100%, mtu anayejuwa kitu hasemi nadhani.

Lakini mada hapa Ni kuhusu kufikiria na kutafakari ambako watu wengi hawana taaluma hiyo. Hata watawala wetu hawana hofu na sisi tusiojua namna ya kutafakari. Ndio maana miradi mingi inaanzishwa na kumaliziwa uchaguzi unapokaribia, nyongeza za mishahara zinatangazwa uchaguzi ukikaribia, viongozi wengi Ni wapole Sana kipindi Cha uchaguzi ukikaribia, t-shirt, kofia na ubwabwa vinatosha kumpa mtu kura.
 
Back
Top Bottom