Song: Shahidi by Dizasta Vina Uchambuzi

Song: Shahidi by Dizasta Vina Uchambuzi

Foffana

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2022
Posts
861
Reaction score
1,547
Tarehe 27.4.2022 @dizastavina (Black Maradona) aliachia yet another lyrical masterpiece inakwenda kwa jina la SHAHIDI. Mdundo umeundwa na Ringle Beatz. Mashairi yameandikwa na Dizasta Vina.

• Ringle Beatz ni mmoja wa watayarishaji bora katika uandaaji wa midundo ya Hip Hop. Alianza kuonekana/kusikika vizuri miaka ya 2012 wakati akiandaa midundo kwa ajili ya kipindi cha Fidstyle Friday,

• DIZASTA ametumia hadithi za vigano katika kusimulia kisa cha SHAHIDI. Huko ndani unasikiliza soundtracks za vilio na maji kuendana na kisa chenyewe cha SHAHIDI aliyenusurika katika ajali.

• DIZASTA amesimulia jinsi meli ilivyozamishwa na vyanzo saba (7). Uvivu, Ulafi, Wivu, Kujikweza, Hasira, Tamaa ya madaraka, Tamaa ya ngono. Hii ni tofauti kati ya DIZASTA na watunzi wengine.

• Maudhui ya wimbo, mpaka kati ya makundi; DIZASTA amejadili kuhusu mpaka uliopo kati ya tajiri na masikini. Viongozi na wananchi. Watawala na watawaliwa. Wasomi na wasio wasomi.

• DIZASTA ameonesha jinsi kundi moja lilivyo na ushawishi katika masuala yanayoathiri sehemu zote mbili na lingine lisivyosikilizwa katika jamii kutokana na mtazamo wa kijamii wa kutokuwa na kitu.

• DIZASTA kwa wajihi wa SHAHIDI amezungumzia; ulevi, ujinga, uzembe kazini, matumizi mabaya ya madaraka, matumizi mabaya ya rasilimali za nchi, uonevu wa vyombo vya usalama,

• DIZASTA anataja alhamisi September 07. Anazungumzia @TunduALissu kupigwa risasi 07.09.2017. Sauti za wanahabari zinasikika. Utasikia jina la Martin Maranja Masese (MMM).

• Kwa sauti ya nyuma utamsikia Mwanahabari Martin Maranja Masese (MMM) anatoa taarifa mbili; (1) kuzama kwa meli iliyopewa jina la “T-912” na (2) kupotea kwa manusura wa ajali hiyo ya meli.

• Taarifa baada ya shambulio hilo la kuogofua zinaeleza Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi jumla 38. DIZASTA katika SHAHIDI anasema alifungwa katika chumba na kuchapwa mijeredi 38.

• T-912. ‘T’ ni Tanzania na ‘912’ ni siku ya uhuru wa Tanganyika (9/12). SHAHIDI anatueleza 07/09.2017 Tanzania ilipoteza ilichokitafuta na kusimamia 9/12/1961. Uhuru, heshima, haki na usawa.

• Walinzi ni vyombo vya usalama. Mrembo ni rushwa. Chumba cha sauti ni vyombo vya habari. Sasa SHAHIDI ambaye ametajwa na kuzungumziwa katika wimbo huu wa DIZASTA ni TUNDU LISSU.

• Nakuacha na swali. Kama SHAHIDI ni Tundu Lissu, katika ile meli nani ni matajiri waliompuuza SHAHIDI? Mafundi katika meli ni nani? Wasomi ni akina nani? NAHODHA wa meli ni nani? Naomba majibu yako.

Copied from Martin Maranja Masese
 

Attachments

Back
Top Bottom