Songea mbona haibadiliki? Kuna tatizo gani na mmekuwa na Mawaziri toka miaka ya 1960?

Nini kinakuzuia wewe kujenga jengo ndefu hapo Songea? Jenga wewe uwe jasiri mwongoza njia.
 
Mkuu taratibu, heshimu miji ya watu.

Sitokei Mbeya Ila binafsi napapenda. Kule Tukuyu ni mahali pazuri Sana. Kule Rungwe Pako poa mno.

Uchafu wa Mbeya labda ni Hapo Nzovwe na Mwanjelwa.

Unapozungumzia mahali ni lazima uhusishe na watu wake. Wale wadada wa kinyakyusa ni wakarimu Sana.

Wakati mwingine matarajio na matamanio yako binafsi yabaki kuwa yako Mkuu. Kumbuka tofauti ya kimtamzamo ndio inayoifanya dunia iendelee kuwepo.

Relax.
 
Tuambie kwenu wapi wewe tuone kama umepaendeleza
 
2025 songea na wilaya zote huku

Kura zote kwa ccm[emoji123],


Muendelee kukandamizwa huko mikoani kwenu,

Tunahakikisha unga mtanunua kilo sh,5000 na maharage kilo sh,8000

Hatunaga stress,tumeridhika na songea yetu.
Kumbe mchumba unatokea songea

Basi kila ilivyo utakuwa na uno la kingoni
 
Atleast mwanza wanaweza kujipiga kifua na kusema tumeendelea km dar
 
Tukuyu sehemu gani unaishi ili upewe ukweli wako, Maana mimi Mkinga nimetembea sana huko

Tukuyu pale mjini yaani Bagamoyo, Magereza, Bulyaga, Makandana, Mwisho wa mji au Kiwira Road, Soko mjinga

Sasa ongea tukupe ukweli wa huko Tukuyu au Kyela

Wanyakyusa bwana mna shida sana

Ahaaa sitakiwi niongee ukweli utalia

Kulikuwa na Mganga wa Kienyeji kule kunaitwa Bujinga shule ya msingi kama una kufahamu aliitwa Mwanyita sijui yupo

Unajua sisi wanasiasa tunahangaika sana sana
 
Mkuu hiyo ni Fasihi ya uandishi

Wewe sasa ni kichwa cha panzi huelewi lengo la muandishi bado

Muandishi ameandika kama kuwakejeli watu wa Mtwara, Neno M wanatamka n ndio maana kaandika Ntwara

Hata mimi napenda Mwananke ya Ntwara inakatika sana mauno

Na wewe basi hata uelewi

Huko kuna usemi wao "Mwananke yule kunoga sana"

Huna exposure wewe, Tembea uone

Sasa ukifika kilwa masoko huko wewe utalia sana, Huko hakuna neno naomba, Hakuna neno Samahani

Huko kitu ni chako lakini mtu anakuambia kwa command

Hata wewe Kilaza hapa JF Inaonekana kunoga sana

Ntwara huko kuna "kunoga sana"
 
Zee la mjini wewe
 
Ndio tumuulize mtoa Post kuwa amekuja Songea hipi ambayo haina mabadiliko kimapato na ,kimiundombinu?[emoji1787]
 
Songea Mjini ukitaka upate refreshment utembee mida ya jioni uwe na usafiri. Kama ulifika Bombambili ukakaa Hapo Hapo utasema mji mbaya. Piga Route kutoka Shule ya Tanga,Msamala,Bombambili,Matarawe,Mjini,SeedFarm, Ruhuwiko
Yaan jamaa inaonekana alifika sehem moja akaakaa kisha ndio akaandika post..sidhan kama alienda katika ya mji namna Magorofa yalivyojengwa..Barabara zilizovyotandazwa kuelekea Tarafa mbalimbali na Soko jipya la kisasa linalotarajiwa kujengwa kisasa
 
Songea Mjini pametanuka sana tofauti na Zamani, Makaa ya Mawe Kitai yametoa ajira na magari makubwa mengi yanapita njia ya Njombe na Tunduru raia wameanza kujiongeza Kwa kuweka Parking za kulaza magari na Lodge njiani
Sahii saiv waawekezaji wengi sana toka Rwanda na Kenya wananunua Viwanja kuwekeza Sheli ,Yafi na Rodge jamaa sijui alifika Songea ya wap
 
Labda kwa kuwa ilichelewa kupata umeme wa Grid inaweza kuwa sababu. Maana uwekezaji wa viwanda vikubwa haukuwepo na waliotaka kuwekeza waliambiwa umeme hautoshi maana ulikuwa wa majenereta.
 
Hata makaa ya mawe yanawabeba kwenye GDP
 
Mkuu, vipi kuhusu Tanga, kama umewahi fika? Na mrejesho kuhusu Lindi upo humu, maana ndio kwanza niko page 1.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…