Songea tuiache Majimaji ishuke, tuisaidie JKT Mlale ipande

Songea tuiache Majimaji ishuke, tuisaidie JKT Mlale ipande

mdundo ngoma sana

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2016
Posts
1,002
Reaction score
955
Kwa muda mrefu sana timu ya Majimaji imekuwa ikiendeshwa kienyeji hali ambayo imekuwa ikitupa hasira,majonzi, mateso na stress zisizokuwa na kikomo.

Timu imekuwa ikishuka daraja kirahisi na wanasiasa wanaipandisha kwenye uchaguzi.Kwa hali ilivyo ni bora timu hii ishuke daraja na ife kabisa kwa maana hakuna inachofanya.

Viongozi wamesajili utumbo mtupu, sijawahi kuona timu mbovu kama Majimaji.

Natoa wito kwa wanasongea tuipiganie JKT Mlale, wale ni wanajeshi hawataweza kutuangusha.

Tuachane na timu hii yenye asili ya vita vya Majimaji ambavyo babu zetu walionesha ari ya kuipigania nchi hii kinyume chake timu imekuwa ni daraja la kupitia kila timu.

Majimaji ni mbovu hata akiletwa GUADIOLA AU MOURINHO HAITASHINDA.
 
Itashuka kama ilivyopanda,ilipanda kisiasa na itashuka kisiasa .
 
Ushawaona akina Mpagwa son,Juma Pandu,khalfan yule mwenye vigari viliandikwa nokia,ottawa,kuna yule wa mbinga sijui nani hata akinunua bombadia anaipeleka kwao huko!?
 
Ushawaona akina Mpagwa son,Juma Pandu,khalfan yule mwenye vigari viliandikwa nokia,ottawa,kuna yule wa mbinga sijui nani hata akinunua bombadia anaipeleka kwao huko!?
Mfanyabiashara anakuja timu ikionesha mwanga, hawachangi tu kama harusi.
 
mzee kupandisha timu sio jambo la kitoto.bora muishikilie water water yrtu hiyo hiyo chonde chonde
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Back
Top Bottom