LGE2024 Songwe: Jeshi la Polisi linawashikilia Gidion Siame na Fiston Haonga wa CHADEMA kwa kosa la kujeruhi

LGE2024 Songwe: Jeshi la Polisi linawashikilia Gidion Siame na Fiston Haonga wa CHADEMA kwa kosa la kujeruhi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linawashikilia Gidion Kefasi Siame (34) Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Momba na Fiston Alinoti Haonga (57) ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Jimbo la Momba CHADEMA wote Wakazi wa Kijiji cha Nakawale kwa kosa la Kujeruhi.

Tukio hili limetokea Novemba 27, 2024 majira ya 3:00 asubuhi huko katika ofisi ya Kijiji cha Nakawale Kata ya Ikana Tarafa ya Ndalambo Wilaya ya Momba Mkoani Songwe ambapo Amos Eliud Sikawanga (41) mwenyekiti wa CCM Kata ya Ikana Mkazi wa Kijiji cha Nakawale alishambuliwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali eneo la kichwani na watuhumiwa hao.

Pia soma:
- LGE2024 - Songwe: Mwenyekiti CCM achomwa kisu cha utosi, Polisi yawakamata Viongozi wawili CHADEMA

Uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha tukio hilo ni mihemuko ya kisiasa ambapo watuhumiwa walikuwa wanamzuia mhanga asiingie kwenye chumba cha mawakala wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika ofisi ya Kijiji cha Nakawale.

Mhanga yupo Kituo cha Afya Tunduma anaendelea na matibabu na uchunguzi wa tukio hili bado unaendelea na pindi utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe halitasita kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria dhidi ya mtu yoyote anayetaka kuvuruga amani.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Imetolewa na:
Augustino Senga -SACP
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Songwe

1732812860533.png
 
Back
Top Bottom