Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Wakuu!
Hekaheka zinazidi kuendelea katika kipindi hichi cha uchaguzi. Naona watu wasiojulikana wamehamia CCM mbona kazi ipo
===================
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Itumba wilayani Ileje, Mkoa wa Songwe, Huruma Ally amevamiwa na watu wasiojulikana na kumvunja miguu yote miwili.
Akizungumzia tukio hilo leo Jumapili, Novemba 10, 2024 mjini Ileje, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM wilayani hapa, Maoni Mbuba amesema uvamizi huo umetokea usiku wa kuamkia jana Jumamosi, Novemba 9,2024, huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika.
Mbuba amesema katibu huyo amevamiwa saa nne usiku, eneo la Shule ya Msingi Itumba na aliokotwa na wasamaria wema akiwa katika hali mbaya, baada ya kuvunjwa miguu na kupoteza fahamu.
Soma Pia: Yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Songwe
Amesema alipelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matibabu, huku akisema kitendo hicho hakikubaliki na kimezua taharuki hususani katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Mbuba amesema CCM Wilaya ya Ileje inalaani kitendo hicho, huku akiwataka wanasiasa na watu wa kada zote kuacha kujichukulia sheria mkononi.