DOKEZO Songwe: Machinga 1,300 wakimbia eneo walilowekwa kwa muda baada ya ujenzi wa Soko kutelekezwa Tunduma

DOKEZO Songwe: Machinga 1,300 wakimbia eneo walilowekwa kwa muda baada ya ujenzi wa Soko kutelekezwa Tunduma

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wafanyabiashara wadogo walioondolewa pembezoni mwa barabara Mwaka 2022 na kupelekwa katika eneo la Kata ya Majengo ilipokuwa Stendi ya Zamani ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma Mkoani Songwe, wamelazimika kulikimbia eneo hilo baada ya sintofahamu ya kusimama kwa ujenzi wa Soko la Kisasa la Machinga Complex lenye thamani ya Tsh Bilioni 6.8 lililokuwa linajengwa pembezoni mwa barabara ya Tunduma-Sumbawanga katika eneo hilo.
photo_2024-08-09_13-40-29.jpg
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara Wadogo (Machinga) Mkoa wa Songwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamachinga katika eneo hilo JASTIN KASHIRIRIKA amedai Juni 2022 Halmashauri ya Mji wa Tunduma iliwaondoa Machinga barabarani na kuwapeleka eneo ilipokuea stendi ya zamani kwa makubaliano ya kufanyiabiashara kwa muda huku wakisubiri kukamilika kwa ujenzi wa Soko la Machinga waliahidiwa baada ya miezi mitatu ujenzi ule ungekamilika.

Kashiririka amesema Novemba 2022, Machinga 1,500 walitoka katika maeneo yasiyo rasmi (barabarani) na kukusanyika eneo hilo wakiwa na matumaini makubwa ya kuboreshewa miundombinu.

Soma Pia: Soko la Kijichi (Temeke) limejengwa kwa Mamilioni ya mkopo wa Benki ya Dunia lakini halitumiki, nini hatima yake?
photo_2024-08-09_13-40-19.jpg
Ujenzi ulisimama na hakuna majibu waliyopewa, ndipo taratibu Wafanyabiashara walikata tamaa na kuanza kulikimbia eneo hilo.

Baadhi ya Wafanyabiashara wamerudi maeneo ya barabarani licha ya kudai ni hatarishi kutokana na barabara za Tunduma kukumbwa na msongamano wa Malori yanayovuka mpaka kuelekea Nchini Zambia na baadhi yao wamevuka mpaka kwenda kufanyia biashara upande wa Zambia kutokana na miundombinu ya kibiashara upande wa Zambia.
photo_2024-08-09_13-40-27.jpg
Kashiririka ameongeza kuwa mpaka sasa Wafanyabiashara takribani 1,300 wamekimbia eneo hilo na kubaki 210 tu.

Akieleza sababu zinazowafanya Machinga kukimbia eneo hilo, Kashiririka ametaja kuwa zipo sababu kadhaa za kimiundombinu ya kibiashara kuwa mibovu na ambapo haiwezeshi wateja kufika katika eneo hilo kama ifuatavyo.

Mojawapo ya sababu inayowakimbiza ni kuona eneo ambalo soko lilikuwa linajengwa pamegeuzwa matumizi na kuwa uwanja wa mpira kinyume na makubaliano ya Wafanyabiashara na Serikalli kupitia Halmashauri ya Mji wa Tunduma.

Pili, eneo hilo kuna Barabara ya Tunduma-Sumbawanga na baadhi ya Wafanyabiashara wamevuka upande wa pili wa barabara ambako ndio wateja hutokea, hivyo inakuwa vigumu wateja kufika katika soko hilo la muda.

Tatu, ushirikishwaji wa maendeleo ya ujenzi wa soko baina ya Wamachinga na Serikali umevunjika kutokana na kinachodaiwa kuwa ni ubadhilifu wa fedha ya Serikali uliofanywa na baadhi ya Watumishi wa Halmashauri, kutokana kwamba licha ya Serikali kutoa Tsh. milioni 383.

Halmashauri iliongeza zaidi ya milioni 100 za mapato ya ndani kukamilisha ujenzi huo lakini awamu ya kwanza ya ujenzi ikashindwa kukamilika.

Upande wake Afisa Biashara wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma, CHARLES MAZENGO akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji amekiri kuwepo kwa changamoto ya kusimama kwa ujenzi wa Soko lililokusudiwa kujengwa kwa thamani ya Tsh Bilioni 6.9 na Serikali Kuu ilitoa kiasi cha Tsh milioni 383 pekee kama sehemu ya kuanza ujenzi na baadaye haikupeleka fedha kutokana na sababu ambazo hazijawekwa wazi kulikosababisha ujenzi kusimama mpaka sasa.

Imeelezwa kuwa licha ya Halmashauri ilishaandika barua ya kukumbushia kuomba fedha Serikali bado haijatoa fedha jambo ambalo Halmashauri ilitegemea fedha kutoka Serikali Kuu.

Kuhusu eneo hilo kugeuzwa uwanja wa mpira, Mazengo amesema hakuna barua ya kiofisi isipokuwa Watu wameamua kugeuza matumizi ya eneo hilo baada ya kuona eneo hilo liko wazi baada ya wigo kuondolewa na kwakuwa walikosa maeneo ya kufanyia mazoezi wakamua kwenda kwenye eneo hilo.
 
Huku rukwa wamekuja viongozi wa machinga taifa badala ya kuja kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa machinga wamekuja kujenga vijiwe vya ccm kwenye masoko katibu wa machinga wilaya sumbawanga alipohoji walimpeleka polisi
 
Back
Top Bottom