Uongozi wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Songwe, umevitaka vyama vingine vya siasa kudumumisha amani katika kipindi chote cha kampeni pamoja na siku ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mtaa, utakaofanyika Novemba 27, 2024 huku ukiwatahadharisha waliojipanga kuvuruga zoezi hilo.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Songwe Bi. Fatuma Hussein, ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafuasi wa chama hicho kwenye kampeni katika mji wa Tunduma wilayani Momba.