PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Wakazi wa mkoa wa Songwe wameshukuru na kupongeza juhudi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwakumbuka makatibu wake kwa kuwakabidhi pikipiki mpya, maarufu kama Pikipiki za Mama.
Wakazi hao Wanasema hizo zimeleta mabadiliko makubwa ya kasi na ufanisi katika utendaji wa kazi za chama mashinani.
“Si kama zamani walikuwa wakitembea kwa miguu au kukopa usafiri, Sasa wanatembea hadi vijiji vya mbali bila taabu,” alisema Juma Mwambusi Ally mmoja wa wakazi wa Songwe kwenye Mkutano wa Kampeni ulipofanyika mkoani humo.
Hatua hii ya kutoa pikipiki imetajwa kuwa sehemu ya maono ya Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Mama Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha chama kinafika kila kona ya nchi.
Wengi wamesema Pikipiki za Mama si usafiri tu, bali ni alama ya maendeleo na dhamira ya kweli ya kuwahudumia wananchi.
Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt Samia Suluhu Hassan anaendelea na Kampeni zake na Kesho anatarajiwa kuomba kura kwa Wananchi wa Mkoa wa Singida.