Sony & Honda wametengeneza EV inaitwa AFEELA ambayo unaweza kucheza Play Station 5 humo ndani!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Kampuni mbili kutoka Japan, Sony na Honda, wameungana kutengeneza joint venture inayoitwa Sony Honda Mobility kwaajili ya kutengeneza magari ya umeme (EV) yatakayoenda kwa jina la AFEELA.


Chuma ya kwanza imeshatoka, ni sedan, na kusema kweli inavutia. Ukiiona ni kama Lucid Air lakini hapana, hii imetoka JP sio USA.


Hii gari inakuja na electric motors mbili, mbele na nyuma, ambazo kwa pamoja zinatengeneza horsepower 480, na iko powered na battery la 90 kWh.


Sony kuonesha ubabe wake, katuwekea jumla ya camera na sensor 45 ndani na nje kwenye ili gari, kuhakikisha usalama na ulinzi wakati wa kuendesha au tukiwa tumepark.


Kwa mbele kuna mbwembwe ya screen ambayo unaweza kuunganisha na simu yako, uki unlock gari inakukaribisha kwa maneno matamu.


Mlangoni kuna camera ambazo zina sifa ya facial recognition, kwahiyo ukibonyeza open button kwenye cm yako, camera inajua uyu ni owner wa gari na ina unlock na kujifungua mlango automatically.


Tukianza na seat ya dereva, kwanza anakua na screen mbili za pembeni zinazotumika kama side mirrors kwasababu nje hamna vioo kuna camera.

Pia ana steering wheel ambayo ni Yoke style, ana instrumental cluster ambayo pia ni LCD na katikati kuna infotainment screen.


Seat ya nyuma pia ina independent screens.


Kuhusu kucheza PS5, Yes, ni kweli kwa kutumia feature ya PS5 ya “remote play” inayokuruhusu ku-stream game kwa kutumia internet kutoka kwenye PS5 console mfano labd ailo nyumbani. Kwahiyo utakogin kisha utaanza kucheza kwenye gari kwa kutumia pad au steering wheel (kama Tesla).


Hii gari ni Level 3 FSD kwa msaada wa LiDAR camera na sensors ambazo zipo ndani na nje.

Bei haijawa officially, ila rummors zinasema itakua arround $45,000 ambayo ikiwa kweli inamaanisha itakua sawa na Model 3 na chini kidogo Model S.

Hii nitasubiria used.
 
Chuma Hicho Na Sasa Kinatema Che~Che ~Che
 
Hata mimi passo yangu naweza cheza PS5. Nimefunga 32' tv kwenye boot😂.

Fake it, till you make it😂
 
Sioni kama ikitoboa naona wameweka vitu kibao visivyokuwa na maana kama vile wanatengeneza gadget za watoto.
Haitoboi kama lucid bahati ni kwamba saudia inaendelea kupump pesa kwa lucid.
Ila lucid mimi nazielewa sana sijui kwanini raia hawazinunui kwa wingi.
Ocean fisker chaliii
 
Lucid Air yupo vizuri sahivi kwenye mauzo. Vizuri sana mfano mwezi August na Sept kauza vizuri.

Tatizo la mauzo kutokua mazuri sana ni bei. Cheapest Lucid Puri ni $70,000 wakati hapo unapata Tesla M3 mbili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…