Mwanatasnia maarufu Kutoka India Sophia Leone miaka 26 ameripotiwa kukutwa amefariki dunia nyumbani kwake, uku chanzo halisi Cha kifo chake kikiwa bado hakijafahamika kutoka kwenye mamlaka zinazohusika.
Chanzo: New York Times, New York Post
Nawaasa ninyi mlioangalia sehemu zake za siri, mkatubu, mumrudie Mungu wenu kabla hamjamfuata. Ni dhambi kuangalia sehemu za siri za mtu mwingine. nilishaandika humu kwamba, Yesu alisema ole wake amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini moyoni mwake. ukiangalia porno lazima utamtamani yule mwanamke au mwanaume, na kule kutamani tu umeshazini naye.
Porn inachafua nafsi, ambako Roho Mtakatifu anakaa, hivyo moyo wako unakuwa mchafu kwa mawazo ya uzinzi na picha za uchi. Mungu alivyotuumba aliumba tufiche uchi, na yule anayetazama uchi kwa makusudi ni kosa, sio mapendeleo ya Mungu wanadamu tuishi hivyo. wengi huwa wanasema labda kwasababu Biblia haikuandika moja kwa moja kwamba kuangalia porno ni dhambu au sio dhambi, wanasahau kuwa Roho Mtakatifu huwa anaweza kutushuhudia wazi wazi kwamba kitu fulani hata kama hakikuandikwa kwenye Biblia ila ni dhambi, Yesu alisema huyo Roho atatutia kwenye kweli yote. Biblia ingeandika kila kitu ingejaa dunia nzima. yapo mambo ambayo hayakuandikwa ila ni dhambi,ndio maana hata wafuata sheria kama wasabato waliong'ang'ania kwenye sheria chache, na kuacha sheria za roho wanaamni wamemaliza kumbe kuna mambo mengi sana ni dhambi na hayakuandikwa.
wakati Biblia inaandikwa, teknolojia haikuwa kama sasaivi, hata vita walitumia farasi, sio ndege na mabom kama sasa. porn zilikuwepo, ila ili mtu aone alikuwa analewesha mtu akilewa anaenda kuuangalia uchi wake. hapakuwa na mapichapicha kama yaliyopo sasa, au mavideo, ila watu walifanya pia kwasababu shetani alikuwepo.
pia,
Habakuki 2:15 inasema, Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kutazama uchi wao.
kumbe kuna watu hadi walikuwa wanalewesha mtu ili wauone uchi wao, na Mungu akawaonya. siku hizi tech imeboreshwa sio lazima umleweshe, yeye mwenyewe anajipiga anaweka mtandaoni na ku-share dhambi yake, yule anayeonyesha uchi na wewe unayetazama mtakunywa kikombe kimoja.
nawaasa okokeni, ikimbieni zinaa, mkabidhini Mungu maisha ili awasaidie kuishinda dhambi, dhambi ni utumwa. kama ungependa kuokoka, sema nami sala hii fupi, kabidhi maisha ya Yesu leo, hujui utakufa lini, inatosha sasa kwa dhambi ulizofanya, inatosha sasa kukaa mbali na Mungu, rudi kwa kunyenyekea na kusikitika kama mwana mpotevu, Mungu atakusamehe dhambi zako zote, utakuwa kiumbe kipya, na atakupa uzima wa milele.
sema:
Eeh Mungu, mimi ni mwenye dhambi, naamini moyoni mwangu ulimtoa Yesu Kristo akafa kama kafara la dhambi zangu, ninatubu dhambi zangu zote (zitaje unazozijua), namkiri Yesu Kristo kwamba ndiye Mwokozi aliyeninunua kwa Damu yake, naomba unisamehe, unioshe kwa Damu ya Yesu. nakabidhi maisha yangu kwako, sasa kwa Jina la Yesu.
kimchezo mchezo tu umeshaokoka, sasa soma Neno la Mungu, jiunge na wenzio waliookoka ili msaidiane katika Neno la Mungu na wokovu, hudhuria ibada kwa watu waliookoka (sio manabii wa uongo), mjaribu Mungu kwa njia hii uone kama hatakuokoa kabisa kabisa na kubadilisha historia ya maisha yako. Mungu akubariki.