Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Kiongozi wa uasi, aliyezungumza usiku ule (Emmanuel Nchimbi) kapewa onyo akiwa tayari Balozi, tena balozi ambae aliteuliwa baadae huku wenzake wa awali wakishinda pale foreign kwenye mabenchi wakisoma magazeti kusubiri vituo; Wafuasi wa nchimbi wanasamehewa/wanafukuzwa uanachama, tena baada ya mmoja wao (Sofia Simba) kuweka wazi kabisa kwamba yeye na siasa za CCM sasa imetosha.

Ama kweli CCM vituko kuisha mwiko.
Mabadiliko ya ccm yanakuumiza?
 
Sophia simba kajikomboa toka kwenye mikono ya wanyonyaji
Kama uyasemayo yana ukweli naye alihusika kutunyonya, vinginevyo angejiondoa mwenyewe mara baada ya kuhisi wananchi wananyonywa.
 
Mbona Waziri mkuu MKM alikuwa miongoni mwa watu waliosimama ukumbini na kuimba wimbo wa "Tuna imani na Lowassa"na hajafutiwa uanachama?

Ndiyo maana Taifa linakumbwa na misukosuko kila siku,kumbe hata sisi tusiomchagua tunaweza kuundiwa zengwe na kupoteza utanzania wetu,hii hatari sana.





Mods tafadhari pandisheni hiyo video ili jf iwasaidie hao viongozi kutendeana haki,wawafukeze wote walioonesha mapenzi/imani kwa mh.Lowassa.

ZIlikua njaa na bendera fata mkumbo
 
Hiki chama kinakoelekea ukibishana na mwenyekiti unanyongwa
Ndio wanakoelekea mtu visasi kwenye mambo ya kitoto. Huyo mama huwezi kumtreat namna hiyomtu aliyeshikilia nyadhifa mbalimbali serikalini na kwenye chama chao. Anyway waache nao waisome namba lakini
 
Sofia simba karibu sana cdm ili tuzidi kuisambaratisha ccm na waendelee kufukuzana hadi abakie lizaboni tu
Mchukueni tu maana namna jinsi tena kwani boss wake mnaye tangu 2015
 
Wamfukuze na Mwenyekiti wao.. Mbona naye anawasaliti?
 
Tangu linivulisikia kauli ya Mh. Majaliwa kumuunga mkono Lowasa??? Ulisikia akilalamika kuwa hakuridhika na maamuzi yaliyochukuliwa kumuengua Lowasa???

Hio video unamuona Mh. Majaliwavakiimba au amesimama kama ada iwapo Mwenyekiti anakuwa anaingia ukumbini??? Chadema acheni propaganda za kitoto....
Kwani ukikubali tu kuwa Majaliwa aliimba kuwa ana imani na Lowasa utapungukiwa na nini? Rudi tena na tena kutazama hiyo clip! Tatizo lenu ghafla mmesombwa na mkondo unaoamini katika visasi na chuki!
 
wangefukuzwa wote au wengine walitubu?
Pia kwa utawala bora, wanachama wajulishwe sababu za kina za makosa yao ili isionekana kuwa na mawazo tofauti na wengi ndani ya chama ni makosa
Sio kila jambo linaanikwa mpk uamuzi huo umefikiwa jpm hajakosea amechambua taarifa za vyombo vingi vinavyomzunguka katika mamlaka yake
 
Ukizoea kula nyama za watu hutaacha - Jk Nyerere .

Walianza kwa wapinzani sasa wanatafunana wenyewe .
 
Kosa la hawa waliofukuzwa Uanachama wa CCM kuanzia leo:
1. Sophia Simba;
2. Ramadhan Madabida;
3. Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa;
4. Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara; na
5. Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga.
ni bad timing. Walitumia muda wao vibaya. Wangeachana na CCM na kuhamia upinzani wakati wa kampeni za uchaguzi (2015) wangekuwa heros kwa UKAWA na hivyo wangebaki hai kisiasa. Kwa sasa ni bahati mbaya kuwa they slowing down to the dip. They are gone for ever from active politics.
 
Aiseh madabida! mara ya mwisho kumuona alikuwa pale mwalimu nyerere conversion centre na wale wasanii! pole sana! Sio mbAya kuna chama kipya kipo humu cha mwenyekiti mtarajiwa anaweza kufanya application
 
Kwa NCHIMBI CCM ilikuwa ni lazima waufyate kulikuwa hakuna namna,mtu walitangulia kumpa ulaji kwanza wakati alikuwa ni mtuhumiwa halafu wanazuga kwa kumuonya.
 
Back
Top Bottom