Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Karibu chadema mama huko siko make mnambiwa mtoke hamtaki sasa umeona yalio kukuta kweli ccm mbele kwa mbele
 
Hapo CCM mtukufu mwenyekiti akisema niongezeeni muda wa kuwa mgombea wenu, wote mnasadiki na kuitikia ndiyo mtukufu.
Mlipobadilishiwa katiba ya chadema na kumpa uenyekiti endelevu Mbowe kwenu ilikuwa raha na kawaida na hamkuhoji, iweje unakuja na day dreams!! Eti akisema aongezewe! Wakwenu aliyekwishajiongezea haumsemi! Ndio maana mnaitwa nyumbu!
 
Sio CHADEMA wala Sio CCM, tena afadhali huku CCM kwa sasa wanafagia fagia hakuna anaeona vizuri hasa watu wa chini wapo tu tunakoenda ndio huko huko, utamshangaa mtu wa CHADEMA pove linamtoka utadhani kwake hakuna udikteta, tena huyo Tundu Lizu nani wa kupinga wazo lake, semeni ukweli? Na Mbowe nani wa kumkosoa kwa sasa? Si umeona waliojaribu yaliyowakuta, na najua hamna uchaguzi wa Mwenyekiti tena dah...

Siasa za Tanzania ni bora wale wasio na vyama lakini hawa mashabiki uchwara ambao hata katiba za vyama vyao hawazijui ni shida... wako kusubiri nani wa kumtukana na kuongea USHILAWADU badala ya kujadili hoja za msingi kwa maendeleo ya taifa hili..

CCM acha ifagie, wakimaliza tunasubiri kama CHADEMA na nyinyi mtafagia au hayo makombo waliotupa chini CCM ndio mtaokota kama kawaida yenu?

Maana hamtaki kujibidiisha na nyinyi mkae mezani mle chakula fresh sijaona hata program za kuelemisha vijana wenu kuhusu maono ya CHADEMA kila siku viongozi wenu kwenye makorido kulinda nafasi zao kwa kutafuta kashfa ya mahakamani au ya kuuchafua utawala, huku mkipata washabiki badala ya wanachama watakao kijenga chama.

Constructive criticism
 
Tuanze na Katiba Mpya, Katiba ya wananchi. Tumekuwa tukishauriana kujenga nchi kupitia hilo. Nje ya hapo ujenzi wa taifa ni porojo tu. Ni Bahati mbaya sana baadhi mmeingia kwenye hizo porojo baada ya Zitto na Slaa kusaliti harakati za Mabadiliko. Ni ushahidi kwamba mpo kutetea "personalities" as beneficiaries of the economic of affection, not "issues".
Mkuu issue ya Katiba mpya si issue ya Chama ....Chadema hawawezi kushinikiza na kushinda issue ya Katiba mpya bila kupata support kutoka CCM..... Ajenda ya katiba mpya ilibebwa na akina Warioba (wana CCM) na pia ilipingwa na watu ambao ndio wengine waliokuja kukimbilia Chadema na kupewa fursa ya kugombea Urais ....hivyo kwa Chadema ya sasa hiyo si ajenda tena (kama ilivyo ufisadi) ....Chadema inaishi kwa matukio na kwasasa haieleweki inasimamia nini (labda Bashite saga) ....na huwezi kusikia nyie manguli wa kuikosoa CCM mkitoa ushauri wa kisera huko Chadema hata wafanye makosa gani ....au chadema hawakosei? Au Chadema si muhimu kwavile hawana dola? ....
 
Jmn chadema inawapa homa sana ee manake ukichukua kikamanda kimoja tuu cha chuo kikuu inabidi uandaee wenyeviti hamsini hv wa wilaya kupingana nae kihojaaa[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji12] [emoji12]
Mwambie Mbowe kuwa wazazi wa Ben Saanane wanamtaka mtoto wao.Asijifanye kupotezea.
 
Kwani Majaliwa ndiyo kaibeba CCM? Angekutwa na hatia angefukuzwa pia, uwaziri mkuu angeteuliwa mtu mwingine.

Siyo wote waliosimama na kuimba "tunaimani na Lowassa" wamefukuzwa uanachama. Kuna sababu za msingi zilizofanya tuwafukuze tuliowafukuza.

Ikitokea Majaliwa anakiuka maadili ya chama, basi hata yeye hatakuwa na kinga ya kufukuzwa. Lakini, kwa sasa hivi, Majaliwa hana hatia yoyote ile.
Wamesahau ya NEC ya enzi ya Nyerere akamtoa juu kwa juu rais wa Zanzibar na kumweka mwingine, na ndiyo NEC hiyo inarudi! Chama shupavu kweli kweli! Hapa kazi tu!
 
Hilo azimio la kubadilisha katiba kumsimika mwenyekiti apite bila kupingwa mmeshalipitisha?
 
Hii sio democrasia, mbona republican karibu wote walimpinga Trump na hakuna hata mmoja aliyefukuzwa chama. Inaa maana wote walitakiwa kumuunga mkono mgombea hata kama walikua hawampendi?
Rejea tafisiri sahihi ya neno Demokrasia kama ilivyofafanuliwa na Nguruvi3, hiyo ni makubaliano ya namna ya kuendesha mambo baina ya kundi la watu, jamii ama nchi. CCM amekubaliana kujiendesha namna hiyo...kwamba hakuna " kukata rufaa kwa waliofukuzwa"
 
Mwanri si yeye bali Majaliwa ndiye aliforce awepo tu. Mwanri na Majaliwa wote walikuwa manaibu ofisi ya Waziri Mkuu na walikuwa marafiki wazuri tu..

OK, endeleeni kula mema ya nchi.. 2025 pia alete zengwe ahakikishe mrithi anatoka hukohuko kanda pendwa..
Michagga mijizi utaijua tu
 
bila itikadi ni kuchota maji kwa kutumia kikapu cha kindu. Chama cha siasa msingi wake ni itikadi. Vyama vya kitanzania ukianza na CCM vina itikadi au ni uchumia tumbo ?
Mkuu uko sahihi. Jana Humphrey Polepole alijiikanyaga sana alipoulizwa sababu ya mabadiliko hayo ndani ya CCM. Ukweli ni kuwa hapo hakuna mabadiliko ya ukweli kutokana na kwamba mabadiliko ndani ya Chama lazima yawe ya kiitikadi zaidi ili kukiwezesha chama kutekeleza majukumu yake na kukabili changamoto zinazojitokeza katika kuleta maendeleo ya nchi. Lakini hapa mimi silioni hilo. Na kwa kweli kuna mambo ya kuleta wasiwasi. Kwanza kukosa uvumilivu wa kusikiliza mawazo mbadala. Chama lazima kiruhusu mambo hayo hasa kwa ngazi ya Wenyeviti na Makatibu. Nyerere alifanya hivyo na Chama kiliimarika sana. Hii ya concentration of power at the top bila grassroots representaion itaua Chama. Pili CCM wadefine ideology yao ni nini na wanataka kufanya nini. Ningetegemea katika kikao hiki at least wangetoa angalau mwelekeo wa kiuchumi w nchi. Tatu katika kutathmini Uchaguzi uliopita CCM ingeachana kabisa na witchhunting kama ilivyofanya. Uongozi umekuwa na hasira sana kuhusu hao "wasaliti" kiasi cha kwamba tathmini halisi ambayo ilitakiwa kufanywa haitafanyika. CCM wangejiuliza kwa nini wameshindwa katika miji yote mikubwa Tanzania Bara na Visiwani? Dar, Arusha,Mwanza(ilirudi dakika za majeruhi), Mbeya, Iringa, Tanga na Mtwara kote huku Chama kiko hoi. Kujikita kuwafukuza akina Sophia Simba watu ambao wamekitumikia chama maisha yao yote naona siyo busara. Niwatakie kila la kheri!
 
Back
Top Bottom