Tupitie walipopita tuone nani anaweza kuongoza vizuri wanawake wa chama chake.
Huyo mwingine wa CHADEMA simjui, lakini tukianza na huyu Mama Simba naweza kusema mama wa CHADEMA lazima atakuwa bora zaidi kwa sababu mtu yeyote huwezi kuwa mbaya zaidi ya Mama Simba alivyo.
Mama Simba anaulizwa kwa nini unataka vyeo vyote hivyo, uwaziri, ubunge, UWT, and so forth, anajibu, "Uenyekiti wa UWT ni almost ceremonial tu."!!!
Mwenyekiti wa chama cha wanawake anakwambia kwamba kazi yake yani ni titular tu. Eti uendesha chama ni kazi ya katibu. Yeye ni kama figure head tu kawekwa pale. Kwa hiyo anataka nini, ujiko tu? Au apate sitting allowance za mikutano, maana anajua kitumbua cha uwaziri kinaweza kuingia mchanga 2010, maana ubunge wenyewe wa kupewa tu. Sasa huyo mtu atasaidiaje wanawake na chama chake kama cheo chake anakiona ni "ceremonial" ?????
Halafu akaendelea kuchemsha akasema something like "niko hapa naangalia ni jinsi gani nitamsaidia katibu ku run UWT"!! Sasa hebu nambie, mwenyekiti anayaeleza hivyo majukumu yake.
Anaulizwa kuhusu Rais kum-kampeinia kuhusu elimu yake, anasema "ulitegemea Rais aseme tuchague wasiosoma?" Yani anakubali kwamba Rais alimpigia debe!
Anasema anataka UWT iwe sehemu ambayo mwanamke akija na kesi za mume waweze kumwonyesha pa kwenda! Hiyo ndio vision yake na direction ya Jumuiya anayotaka "kumsaidia katibu" kuwapeleka!
Anasema, listen to this Asha, kiongozi wenu wa wanawake Tanzania anasema hiviii,
"katika karne hii ya utandawazi mwanamke amepata majukumu zaidi, kwa sababu wanaume wamekosa kazi kutokana na technolojia mpya hii, siku hizi kazi za maofisini zimekuwa finyu, wanawake wanaweza kufanya kazi nyingi ambazo sio za kuajiriwa, inabidi wawezeshwe..."!!
Yani Asha, nyinyi wanawake, Sophia Simba anamaanisha, you are good at, na muendelee kuwezeshwa kuwa good at, kusuka ukili, kupika maandazi, kuuza mama ntilie, kuchumishwa mboga!
I am not making this up, maneno hayo kwenye nukuu kayasema jana/juzi.
Halafu Waziri Simba mwisho akamtaja Rajab Maranda kama mfano wa wasomi ambao wamefanya ufisadi. Well, huyu Maranda bado hajashindwa kesi mahakamani, Waziri huwezi kutamka kwamba Maranda ni fisadi!!! Eti jamani Waziri wa Nchi ofisi ya Rais wa Tanzania hajui hicho kitu. Halafu una run campaign platform ya usomi?! Huyu ndio kiongozi wa Umoja wa Wanawake wa CCM, Taifa? Katika wanawake wote wa CCM duniani, ni huyu Sophia ndio wamemwona poa!
Hahahaha aa aaaaaaaaa!