Pre GE2025 Sophia Simba: Wanawake waliokaa muda mrefu kwenye Viti Maalum waachie nafasi kwa vijana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwanasiasa na Waziri Mstaafu, Sophia Simba, amesema ni wakati muafaka kwa wanawake waliokaa muda mrefu kupitia Viti Maalum Bungeni kuwaachia nafasi vijana ili kuendeleza harakati za uwezeshaji wa wanawake katika siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Februari 28, 2025, kwenye kongamano la kuadhimisha miaka 15 ya Taasisi ya ULINGO na miaka 30 ya Azimio la Beijing, Sophia Simba ameeleza kuwa Taasisi ya ULINGO, ambayo imefikisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwake, imekuwa chachu kubwa ya kuwainua wanawake katika siasa bila kujali vyama vyao.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Soma Pia: Kipindi hiki cha Uchaguzi wanawake wanapata nafasi ya kutosha kushiriki kwenye masuala ya uchaguzi?

“ULINGO imekuwa na mafanikio makubwa. Tumeona wanawake wengi wakiwa wabunge, madiwani na hata vijijini akina mama wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali,” alisema Sophia Simba.

Tume huru ifute viti maalum na badala yake viwepo vya makundi maalum tu kv walemavu, wavuvi , wastaafu, wachimbaji, wafugaji nk. Lakini posho na mishahara ya wanasiasa ipunguze pia !
 
Mhe. Lissu ana jicho la Ndege Tai

Aliliona hili kitambo kabisa, kumbe hadi CCM walihitaji mtu wa kulisemea 🤗
 
Niwakati familia zawatu waliokuwa viongozi wakaepembeni wanaposhika madaraka hawana uwezo wakutatua machangamoto zaidi yakupata mali nakuwaza madaraka zaidi
Familia za viongozi wa zamani ni wabinafsi sana qumamae zao. I hate those guys a lot. Kujilimbikizia mali tu na kupeana wao kwa wao ndio vitu wanajua.
 
Hivi mke wa spika wa zamani standard &speed bado yuko bungeni?
 
Kachaguliwa na wananchi kutoka jimboni na wala siyo Mbunge wa Viti maalumu. Kwa hiyo ukitaka ubunge nenda kagombee
Kama wananchi ndiyo mnachagua wabunge aina ya huyo mama, basi nyinyi ni zaidi ya vilaza. Inakuwaje mtu hata kujenga tu hoja hajui, halafu mnamchagua kuwa mwakilishi wenu!!
 
Itoke vishangazi vidogo tuingie na sisi 😹😹
 
Mwanasiasa na Waziri Mstaafu, Sophia Simba, amesema ni wakati muafaka kwa wanawake waliokaa muda mrefu kupitia Viti Maalum Bungeni kuwaachia nafasi vijana ili kuendeleza harakati za uwezeshaji wa wanawake katika siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Februari 28, 2025, kwenye kongamano la kuadhimisha miaka 15 ya Taasisi ya ULINGO na miaka 30 ya Azimio la Beijing, Sophia Simba ameeleza kuwa Taasisi ya ULINGO, ambayo imefikisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwake, imekuwa chachu kubwa ya kuwainua wanawake katika siasa bila kujali vyama vyao.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Soma Pia: Kipindi hiki cha Uchaguzi wanawake wanapata nafasi ya kutosha kushiriki kwenye masuala ya uchaguzi?

“ULINGO imekuwa na mafanikio makubwa. Tumeona wanawake wengi wakiwa wabunge, madiwani na hata vijijini akina mama wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali,” alisema Sophia Simba.

Leo kaongea point sana
 
Back
Top Bottom