SORRY MADAM (100) final episode
(Destination of my enemies)
WRITER………………………………………………………………….
………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level
Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..……
www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..
………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT……………………………………………………………
…………….0657072588/0768516188
JIUNGE NA MAGROUP YANGU YA WHATSAPP NA
FACEBOOK, YANAYO HUSIANA NA HADITHI TU KWA
KIIINGILIAO CHA SH 2000 KWA MWENZI.
0657072588.
ILIPOISHIA
“Shitiii”
Agnes akaikoki bunduki yake na kumuelekezea
mtu huyo na kumpima maeneo ya kichwa. Mzee
Godwin hadi anakaribiana na Erickson akaweza
kuona alama nyekundu ya buduki ikiwa imemlenga
Erickson kifuani. Kwa haraka Mzee Godwin
akamuwahi Erickson ambaye anatambua ni mkwe
kwa mwanaye Manka, akamsukuma na risasi
ambayo ilipangwa kumpiga Erickson ikapiga mzee
Godwin mgongoni na kumuangusha chini na
kumfanya Eddy kushangaa na kwaharaka akaipiga
magoti chini na kumgeuza Mzee Godwin na
kumkuta akimwagikwa na damu mdomoni.
“BABABAAAAAAAAAA”
Eddy alipiga kelele humu machozi yakianza
kumwagika usoni mwake na kumfanya Mzee
Godwin kutabasamu na kumshika mkono wa kulia
Eddy na kuuweka kifuani mwake.
ENDELEA
“Eddy”
Mzee Godwin aliweza kuitambua sauti ya Eddy na
kulia kwake. Eddy kwa hasira akaanza kuivua sura
yake ya bandia, japo imeshikana sana na ngozi ya
uso wake, ila hakujali hayo maumivu. Mzee
Godwin akaendelea kumuangalia Eddy kitu anacho
kifanya hafi ikafikia hatua akamaliza kabisa kuivua
sura yake na kubaki na sura alisi.
“Baba fungua macho please”
Eddy alizungumza huku machozi yakimwagika
usoni mwake. Japo baba yake huyo ameweza
kumfanyia mambo mengi mauvu katika maisha
yake yote ila damu ni nzito kuliko maji.
“Ku….uu…wa…..jasiri D.F.E1993”
Mzee Godwin alizungumza maneno hayo kwa
shida kidogo na hapo hapo akakata roho. Kitendo
cha mzee Godwin kuanguka chini na kunyanyuliwa
na Erickson, kiliweza kumstua Manka aliye anza
kushuka kwenye gari kwa garaka, na kuanza
kukimbilia eneo alipo kaa Mzee Godwin na
Erickson. Agnes hakutaka kumpa nafasi nyingine
mlinzi wa John ambaye alikuwa akihangaika
kuikoki bunduki yake. Akamtandika riasi moja ya
kicha na kumchangua hapo hapo. Makachero
wengine walipo ona makubaliano yameingia dosari
wakaanza kufaya mashambulizi kwa kina Rahab na
Fetty, ambao nao waliweza kuyajibu mashambulizi
hayo huku wakiwa amejificha pembeni ya gari lao.
Agnes akashusha pumzi huku akimtazama Manka
kwa kutumia lenzi ya bunduki yake, akikimbilia
eneo alipo Erickso.
“Mpumbavu wewe”
Agnes alizungumza huku akiikoki bunduki, yake.
Alipo hakikisha Manka amekaribia kufika karibu
kabisa na walipo Eddy na mzee Erickson, akaivuta
traiga ya bunduki hiyo na kuiruhusu risasi moja
kutoka kwa kasi. Kitendo cha Manka kumtazama
Erickson na kukuta akiwa ni Eddy, alistukia
akianguka chini na hapo hapo akakata roho, risasi
aliyo ifyatua Agnes iliweza kutua kichwani mwa
Manka ndio iliyo yakatisha maisha ya msichana
huyo.
Eddy alihisi kuchanganyikiwa, baada ya kumuona
Manka akiwa amelala chini, damu nyingi zikiwa
zimesambaa kwenye lami. Halima na Anna wakiwa
chini ya maji, waliweza kupambana na makachero
wengine ambao walitumwa kuimarisha ulinzi chini
ya daraja hilo. Mapambano yao yakawa ni kufa na
kupona. Halima akajitahidi kupambana kadri ya
uwezo wake, ila kwa leo bahati haikuwa kwake
kwani kachero aliye kutana naye aliweza kumzidi
kwa kila kitu na kujikuta akifia kwenye mikono ya
kachero hiyo kwa kuchomwa kisu cha shingoni.
Kifo cha Halima, kilimshangaza sana Anna, aliye
jikuta akiivunja shingo ya kachero aliye kuwa
akipambana naye na kuimtoa mtungi wa gesi alio
jifunga nao mgongoni. Akamfwata kachero aliye
muua Halima, akaanza kuparanganaye, mapigano
kati yao yaliweza kumpa ushindi Anna japo naye
aliweza kujeruhiwa na kisu cha kachero hiyo ila
akafanikiwa kummaliza maisha yake. Taratibu Anna
akaanza kuufwata mwili wa Halima sehemu unapo
elea elea. Akaushika, na kujikuta akianza kulia kwa
uchungu, kwa maana hakutarajia kama rafiki yake
huyo anaweza kukutwa na mauti. Agnes kazi yake
ikawa ni kuwaua makachero wote ambao
wanapambana na kina Fetty na Halima. Haikuwa
kazi ngumu kwake kwa maana sehemu alipo jificha
ni si rahisi kwa mtu kuweza kumuona ila yeye
aliweza kuona eneo zima.
***
Wanajeshi na walinzi walio weza kubaki ikulu kwa
ajili ya kuimarisha ulinzi kwa siku hiyo hawakuwa
na bahati, kwa maana waliweza kushambuliwa na
wanajeshi ambao wamevalia kombati za jeshi la
taifa, ila utoafuti ni kwamba karibia wote
wamejifunga vitambaa vyekundu katika mikono yao
ya kushoto. Walijitahidi kuilinda Ikulu ila
hawakuweza kwa maana shambulizi hilo ni kubwa
na la kustukiza. Meja Paul Msuya aliweza
kuwaongoza vijana wake katika kufanya mapinduzi
hayo ya kuing’oa serikali yam zee Godwin
madarakani.
Zoezi lao halikuchukua muda mrefu sana, wakawa
wamesha maliza kazi yao na kuiwek aikulu chini
ya ulinzi wao. Meja Msuya akatuma wanajeshi
wengine kwenda katika daraja la kigamboni
kumsaidia mkuu wao ambaye ni Rahab. Milio ya
risasi, iliwafanya wakazi wa maeno ya Posta na
Kigamboni kuingiwa na hofu kubwa sana, kwa
maana sio hali ya kawaida na hawakujua ni kitu
gani kinacho endelea. Wananchi wengi walio
ingiwa na woga, kila mmoja aliweza kujificha
sehemu ambayo alihisi anaweza kuokoa maisha
yao. Wapo ambao waliweza kujificha chini ya
vungu za vitanda vyao, wengine walijificha kwenye
makabati, wengine waliamua kujifuanika mashuka
gubigubi na kujinyoosha vitandani mwao na
kuigiza kama wamekufa. Ukawa ni usiku mgumu
sana kwao. Wanajeshi wanao muunga mkono
Rahab, wakafika katika dareja la Kigamboni na
kukuta mambo ndio yanamalizikia malizikia, huku
walinzi wengi wa raisi Godwin wakiwa wamesha
potea maisha yao. Wakaweza kuuona mwili wa
mzee Godwin na mwanaye Manka wakiwa tayari
wamesha teketea kwa kupigwa risasi.
Ushindi huo uliweza kumfurahisha kila mmoja aliye
husika katika oparesheni hiyo ya kuipindua serikali
yam zee Godwin, mtu ambaye walimuona ni kama
diktekta katika kuiongoza nchi.
“Kwa nini mumuue na Manka ana kosa gani?”
Eddy alizungumza huku akimgandamiza Rahab
kwenye gari huku akiwa amemkuja kombati la jeshi
alilo kivaa maeneo ya kifuani.
“Eddy please reduce your anger”(Edd tafadhali
punguza hasira yako)
“Nipunguze vipi hasira, wakai mumemuua mtu
ambaye hata hatia eheee”
Eddy aliendelea kufoka, huku akiendelea
kumkandamiza Rahab kwenye gari hilo. Fetty na
Agnes ambao wapo pembeni, walikaa kimya huku
Agnes akiwa haamini macho yake kwamba
Erickson ambaye alikuwa anampenda siku zote
kumbe ni Eddy ambaye tayari alisha weza kuiona
sura yake kwenye picha na kuelezwa na Manka
kwamba waweze kumuangamiza.
“Eddy am sorry”
Agnes alizungumza huku akipiga magoti chini,
Agnes akatoa bastola yake na kumkabidhi Eddy.
“Niue kwa sababu mimi ndio niliye muua Manka”
“Umemua Manka kwa wivu wako wa kijinga, Manka
mimi ni dada yangu”
Eddy alizidi kuzungumza kwa hasira, akaitazama
bastola aliyo ipokea kutoka kwa Agnes, kwa hasira
akachomoa magazine yake na kuigawanya vipande
viapnde na kuitupia ndani ya bahari. Eddy
akaondoka eneo hilo huku akiwa analia kwa
uchungu. Akaeleka hadi kwenye mwili wa Manka
ulio zungukwa na wanajeshi wa mapinduzi.
Taratibu Eddy akapiga magoti chini, kisha taratibu
akamnyanyua Manka kwa mikono yake miwili na
kuanza kutembea naye kuelekea kwenye gari walilo
kuja nalo. Wanajeshi wote wakasimama kwaenye
mstari mmoja na kumpigia saluti Eddy anaye
elekea kwenye gari. Akauingiza mwili wa Manka na
kuulaza katika siti ya nyuma ya gari hilo kisha
akapanda mbele, taratibu akalirudisha nyuma,
akakunja kona na kuondoka na kuwaacha
wanajeshi pamoja na Rahab wakimshangaa.
Rahab akawagiza wanajeshi wengine kuingia ndani
ya maji na kuanza kumtafuta Halima na Anna. Kwa
bahati nzuri akawaona wakiwa wapo eneo moja.
Wakamsaidia Anna kutoka kwenye bahari, huku
wengine wakiubeba mwili wa Halima na kutoka
naye kwenye bahari. Rahab, Fetty na Agnes
walivyo muona Anna ametoka ndani ya maji hayo
akiwa anamwagikwa na machozi, wakatambua kwa
haraka kwamba kuna jambo baya limeweza
kutokea.
Walipo uona mwili wa Halima ulio bebwa na
wanajeshi hao, machozi yakaanza kumlenga lenga
kila mmoja wao. Fetty na uhodari wake wote
akajikuta akiangua kilio huku akiumtazama Halima
kuhakikisha kama kweli amekufa au wanatania.
“Halipa tafadhali huwezi kufa kirahisi kiasi hichi”
Fetty alizungumza kwa uchungu na kuwafanya
wezake wengine nao kuangua kilio, japo Rahab
alijikaza na kulia taratibu taratibu. Wanajeshi hao,
wakauchukua mwili wa Halima na kuupakiza
kwenye gari, na kuondoka nao kueleka katika
hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kuihifadhi.
Wanajeshi wengine walio salia wakauchukua mwili
wa Mzee Godwin ambao hakuna mtu aliye
uthamini, sana. Wakautupia ndani ya gari na
kuondoka nao.
“Muheshimiwa Ikulu ipo tayari kwa ajili yako”
Mwanajeshi mmoja alizungumza na Rahab.
Wakaingia nanye kwenye gari moja ya ikulu walio
kuja nayo eneo hilo na kuondoka naye. Fetty na
wezake wakapanda katika magari mawili waliyo
kuja nayo na kuongozana na gari hiyo kueleekea
Ikulu.
***
“Hii Laptop ni ya nani?”
Sa Yoo aliuliza huku akiitazama Laptop aliyo
ipakata kwenye mapaja yake wakiwa ndani ya gari
kurudi Dar es Salaam.
“Nimeikuta humu humu, nahisi itakuwa ni laptop
ya Eddy”
Shamsa alijibu huku akeindelea kuongeza mwendo
kasi wa gari hiyo.
“Sasa tunakwenda wapi Shamsa?”
“Mama tunakwenda nyumbani kwako”
“Huoni kama kuna harari?”
Hakuna mtu, kupo salama kabisa”
Waliendelea kuzungumza huku wakizidi kusonga
mbele. Safari yao haikuchukua masaa mengi hii ni
kutokana hakuna magri usiku huo. Wakafanikiwa
kufika nyumbani kwa Eddy, Shamsa akashuka na
kufungua geti kisha akarudi kwenye gari akaingia
ndani, na kulisimamisha gari hilo mbele ya ngazi
za kupandia kueleka kwenye mlango wa kuingilia
ndani ya jumba hilo.
Wote wakashuka na Shamsa akaeleka getini na
kulifunga geti. Wote kwa pamoja wakaingia ndani.
Moja kwa moja wakaelekea chumbani kwa Shamsa,
ambapo Phidaya na Sa Yoo wakaanza kuoga kwa
kupokezana kwani ni kwa muda sasa miili yao
haijagusa maji kabisa.
“Shamsa hivi hii tv inafanya kazi kweli?”
Sa Yoo aliuliza huku akiitizama tv uliyopo ukutani
yenye ukubwa wa nch 41.
“Ahaa wala sifahamu ni muda sana sijaiwasha”
“Waya wake upo wapi?”
“Huo hapo chini una ning’inia”
Sa Yoo akauchukua waya huo na kuuchomeka
kwenye soketi. Akawasha Tv hiyo, kwa bahati
nzuri ikawaka na haikuwa na tatizo la aina yoyote.
“Ina king’amuzi chake ndani kwa ndani, unaweza
kupata local chanel”
“Ahhha sawa”
Sa Yoo akaanza kutafuta chaneli zinazo patikana
kwenye tv hiyo, kwa bahati nzuri akapata chaneli
ya TBC1. Miziki inayo onekana kwenye Tv hiyo,
ikawafanya waburudike japo wote sio wapenzi wa
muziki ila wanaburudika kiaina. Phidaya akatoka
bafuni akiwa amejifunga taulo.
“Jamani nimeimisi nyumba yangu”
Phidaya alizungumza huku akijitupa kitandani.
Akalala chali huku akisikilizia ubaridi mkali wa AC
(Air condition) unavyo ipuliza ngozi yake.
“Breking News?”
Sa Yoo alizungumza huku akiongeza sauti ya Tv
hiyo. Wote macho wakayatolea kwenye Tv hiyo.
Wakamuona muandishi wa kike aliye jitambulisha
jina lake na kuzungumza alicho kizungumza.
“UTAWALA WA RAISI GODWIN UMEPINDULIWA, NA
SASA UTAWALA HUO UNAONGOZWA NA MKE WA
ZAMANI WA RAISI PRAYGOD MAKUYA ALIYEKUWA
RAISI ALIYE SHINDWA KWENYE UCHAGUZI MKUU
BI RAHAB PRAYGOD. TUUNGANE NA MUANDHISHI
WETU ALIYOPO IKULU KWA TAARIFA ZAIDI”
Wote ndani ya chumba wakabaki kimya huku
wakishangaa, hakuna aliye fahamu kitu kinacho
endelea kwa wakati huo. Swali walilo jiuliza ni
kwamba yupo wapi raisi Godwin. Wakamuona
Rahab aliye kaa kwenye meza iliyo jaa maiki za
waandhisha wa habari, huku yeye akiwa amevalia
mavazi ya kijeshi huku usoni mwake akiwa na
tabasamu pana.
“Ndugu zangu Watanzania. Nimatumaini yangu
mupo salama, japo wengi wenu muliweza kupatwa
na wasiwasi mkubwa juu ya mapinduzi haya yaliyo
weza kutokea. Ninamshukuru Mungu mapinduzi ya
serikali hii yamekwenda salama. Huku nikiwa ndio
kiongozi wa mapinduzi haya. Ninawahakikishia
wananchi wote wapenda amani na wapenda nchi
yetu kwamba, kuanzia sasa nchi hii ni nchi ya
amani na utulivu”
“Nipo tayari kuweza kusikiliza maoni ya wananchi
juu ya nani aweze kuongoza nchi hii. Mimi sio
mroho wa madaraka. Ninawatangazia rasmi
kwamba nchi kuanzia leo itaongozwa na jeshi hadi
pale atakapo patikana raisi ambaye mumemchagua
nyinyi kwa kura zetu”
“Pia ninawatangazia kwamba aliye kuwa ni mtawala
wa hi inchi, akatumia madaraka yake vibaya kwa
manufaa yake na familia yake hususasi mwanaye
wa kike, basi hadi ninapo zungumza sasa hatunao
kwenye huu ulimwengu. Nitaandaa utaratibu
ambao kila mwananchi atashiriki kupiga kura yake
kwa haraka iwezekanavyo ili kuweza kuhakikisha
kwamba nchi inapata kiongozi mahiri na hodari.
Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika,
asanteni waandishi wa habari”
Rahab alimaliza kuzungumza, na habari hiyo
ikaisha na miziki ikandelea. Kila mtu ndani ya
chumba hicho akawa kimya, hakuna aliye weza
uzungumza kitu chochote. Sa Yoo akashusha
pumzi huku akitabasamu.
“Sasa imekwisha”
Hata kabla hawajajibu chochote, wakastukia
kishindo kizito getini. Wote wakakurupuka, na
kushuka gorofani huko na kupita sebleni kwa kasi
na kutoka nje. Wakakuta gari moja nyeusi ikiwa
imesimama nyuma ya gari lao wlilo kuja nalo,
huku geti kubwa likiwa lienguka chini, inaonyesha
limegongwa na gari hiyo. Wote wakabaki kimya
huu wakilitazama gari hilo, hawakuweza kumuona
mtu aliyopo ndani ya gari hilo kutokana na vioo
vyote vya gari hilo nivyeusi.
Mlango wa dereva ukafunguliwa, ukatangulizwa
mguu wa kulia, kisha mtu huyo akatoka. Wote
hawakuamini walipo muona ni Eddy, akishuka
kwenye gari hilo akiwa katika sura yake ya asili.
Kwa haraka Phidaya akaanza kushuka kwenye
ngazi hizo, akamkimbili Eddy aliye simama
pembeni ya gari hilo akimtazama. Wakakumbatiana
kwa pamoja, huku wakipigana mabufu mfululizo.
Hakuna kati yao aliye weza kuzungumza zaidi ya
kumwagikwa na machozi tu. Sa Yoo na Shamsa
wakabaki wakitabasamu.
“Upo salama mke wangu?”
“Ndio honey”
“Matatizo yamekwisha mke wangu”
“Asante honeny”
Wakaachiana, Eddy akanyoosha mikono yake huku
kwa ishara akiwaita Sa Yoo na Shamsa ambao nao
walishuka kwenye gari hizo kwa kasi, na wote
wawili kwa pamoja wakamkumbatia Eddy kwa
nguvu. Furaha ikatawala kati yao, kila mmoja
alipatwa na furaha ambayo tangu azaliwe hajawahi
kuipata furaha hiyo. Phidaya naye akamalizia kwa
kuwakumbatia wote watatu kwa pamoja.
“Nawapenda sana, bila ninyi mimi sio kitu”
Eddy alizungumza. Wakaachiana kisha Eddy
akafungua mlango wa nyuma ya gari hilo.Wote
watatu wakastuka baada ya kuukuta mwili wa
Manka akiwa amelala kwenye siti hizo.
“Mungu wangu!!”
Phidaya alizungumza huku akijiziba mdomo kwa
kiganja, hakuamini, msichana mzuri kama Manka
anaweza kupoteza maisha kwa wakati kama huo.
Wakiwa wanaendelea kuutazama, simu iliyo
mfukoni mwa Manka ikaanza kuita, wote wakasita
kuitoa, ila Eddy akajikaza na kuingiza mkono wake
kwenye mfuko wa suruali ya Manka, akatoa simu
hiyo na kukuta namba mpya. Wakatazamana na
Eddy akaipokea na kuiweka sikioni.
“Manka ni kweli eti umekufa?”
Ilikuwa ni sauti ya madam Mery ambayo Eddy
aliweza kuitambua kwa haraka. Akashusha pumzi
kisha akazungumza.
“Manka amekufa”
“Ed…..d….e….d..y unach……o zaungu…..mza ni
kweli?”
Madam Mery alizungumza kwa kubabaika
akionyesha dhairi kwamba amesha patw na hisia
za kulia.
“Ndio mdam Mery na hapa nina mwili wake na
nipo nyumbani kwangu”
“Na…na….akuja”
Simu ikakatwa, Eddy akairudisha simu hiyo
mfukoni mwake, akiwa ana mawazo mengi,
hakujua ni nini anacho weza kufanya kwa wakati
huo juu ya mwili wa dada yake. Taratibu Eddy
akautoa mwili huo na kuubeba, akapandisha nao
ngazi na kuingia nao sebleni, akaulaza kwenye
kochi taratibu. Kwa haraka haraka ukiingia sebelni
hapo na ukiwa haujui ni kitu gani ambacho
kinaendelea unaweza kusema kwamba Manka
amelala tu na yupo hai. Haukupita muda mrefu
wakasikia mngurumo wa gari nje. Wakasikia hatua
za miguu zikianza kupanda kwenye ngazi hizo,
mlango ukafunguliwa kwa nguvu, akaingia madam
Mery ambaye nywele za kichwani mwake
zimechanguka changuka kwa kuchanganyikiwa.
Akaangaza macho yake huku na kule, yakatua
kwenye sofa alilo lazwa Manka huku pembeni ya
sofa hilo akiwa amekaa Eddy aliye jiinamia.
“Manka mwanangu vipi mama, mbona unalala
hivyo jamani”
Madam Mery alizungumza huku akiangua kilio
kizito. Akamkumbatia Manka huku akiendelea kulia
kwa uchungu. Hakuna ambaye aliweza
kuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya kukaa
kimya, ila Eddy machozi yalizidi kumtiririka,
hakuona sababu ya Manka kuweza kupoteza
maisha kwenye siku kama ya leo. Alianza
kujilaumu moyoni mwake kwa kuona kwamba
kuvaa sura yake ya bandia kulipekea Manka
kuweza kumpenda pasipo kufahamu kwamba wao
ni ndugu.
“Ohooo Manka, tazama sasa mdogo wako amebaki
peke yake, unahisi haya maisha yatakuwa vipi
sasa?”
Madam Mery alizidi kulalamika huku akiwa analia
na mikono yake akiwa imemkumbatia Manka.
Masaa yakazidi kwenda na kukatika hadi ikafika
majira ya asubuhi. Sa Yoo akatoa wazo la Manka
kupelekwa katika chumba cha maiti ili kuhifadhiwa
na wao wafanye harakati za mazishi.
Hakuna ambaye aliweza kupinga wazo lake kwa
maana, endapo watazidi kukaa na mwili huo humo
ndani, utaharibika. Eddy na Shamsa wakaupeleka
mwili huo hospitali ya Muimbili na kuwaacha Sa
Yoo, Phidaya na madam Mery wakimfariji.
Wakafanikisha kuuhifadhi mwili huo. Wakaanza
kutafuta sehemu za majeneza, ambapo
wakamchongeshea jeneza zuri lenye rangu nyeupe
pamoja na gauni moja zuri jeupe. Wakalipeleka
hospitalini hapo, ambapo mwili wa Manka
ukaoshwa kwa mara nyingine na wahudumu wa
chumba hicho cha kuifadhia maiti, walipo maliza
wakamvisha Manka gauni hilo, kisha wakamuweka
kwenye jeneza. Ukimtazama kwa haraka unaweza
kusema Manka ataamka pale utakapo muita, ila
sivyo tayari amesha ondoka duniani.
Wakatafuta gari maalumu la kubebea amiti
wakaongozana nalo hadi nyumbani kwa Eddy
ambapo wakakuta watu ambao Sa Yoo aliweza
kuwatafuta, wakawa wamesha maliza kuchimba
kaburi na kulijengea, karibu kabisa na kaburi la
mama Eddy.
“Samahani tunaweza kupata mchungaji?”
Sa Yoo alimuuliza mmoja wa watu hao, walio
chimba kaburi hilo na kulijengea. Mtu huyo
akamjibu anaweza kupata mchungaji, akatoa simu
yake na kumpigia mchungaji wa kanisa lake analo
sali. Akamueleza kila kitu mchungaji huyo
hakuchukua muda mwingi sana, akafika katika
eneo hilo. Japo Manka ni mtu aliye kuwa
akiheshimika katika serikali ya baba yake, ila
mazishi yake yalihudhuria watu wachache sana,
kama mazishi ya raisi Praygod. Mchungaji
akafanya taratibu zote za mazishi na wakamzika
Manka, na watu hao wambao ni wataalamu sana
kwa kujengea makaburi, siku hiyo hiyo wakajengea
makaburi hayo na wakalipwa ujira wao na
kuondoka.
***
Viongozi na vijana wote wa kikosi cha D.F.E,
walipata pigo ambalo kila mmoja lilimgusa sana
kwenye maisha yake. Kufa kwa kiongozi na mmiliki
wa kikosi hicho chenye viongozi wengi kutoka nchi
mbalimbali duniani, kuliashiria hali ya kikosi hicho
kwenda kuanguka. John naye alihisi
kuchanganyikiwa baada ya kutuma vijana wake
wengien kwenda kumfwatilia kijana wake na kukuta
amekufa kwa kupigwa risasi na kazi ambayo
alimtuma iliwezza kushindwa.
Mikakati na mipango ya kuuiba mwili wa mzee
Godwin ndani ya mochwari ya hospitali ya
Muimbili ikaanza, hadi inatimu saa sita mchana
tayari mwili wa mzee Godwin ukawa umesha ibwa
ndani ya hospitali hiyo na moja kwa moja
ukasafirishwa kwa ndege hadi katika makao makuu
ya kikosi hicho. Kisiwa kizima ambacho ndio kina
kambi ya D.F.E kikagubikwa na majonzi.
Wakaandaa mpango mzima wa mazishi wa
kiongozi wao. Mazishi hayo yakaudhuriwa na
viongozi wengi kwa siri, sana pasipo wengine nchi
zao kuweza kutambua.
Mazishi ya mzee Godwin yakafanyika kwa mfumo
wa kijeshi. Mwili wa mzee Godwin ukachomwa
sindano ya kukaushwa ambayo inaweza kufanya
kazi katika mwili huo zaidi ya hata miaka kumi.
Wakautengenezea jeneza la vioo na kuihifadhi
mwili huo kwenye moja chunba maalumu,
ambacho kinalindwa kwa masaa ishirini na nne.
“Ni lazima tulipize kisasi juu ya kifo cha mkuu
wetu”
John alizungumza kwenye kikao hicho na
kuwafanya viongozi wezake ndani ya ukumbi huo
kukubaliana na wazo lake.
***
Rahab, Anna, Agnes na Fetty nao wakajumuika na
vionozi wengine serikalini kufanya mazishi ya
kiongozi wao Halima, ambayo yalifanyika katika
makaburi ya Sinza. Mazishi hayo pia yaliudhuriwa
na wananchi wengi ambao wamebeba mabango
yaliyo andikwa meseji tofauti tofauti. Huku wengine
wakisemea Halima, umekufwa kwa ajili ya
watanzania wote. Wengine waliandika na kusema
kwamba Halima ni mama wa taifa. Kila mmoja
aliweza kuguswa na kifo chake.
Mazishi yakamalizika, siku hiyo ikapita, siku iliyo
fuata kwa kupitia vyombo vya habari Rahab
akawatangazia wananchi jinsi ya kufanya maamzi
ya kumchagua ni nani wanaye ona anaweza
kuchukua kiti cha mzee Godiwn.
Japo Rahab hakujiweka kwenye kinyang’anyiro
hicho zaidi ya kuwataja viongozi ambao walikuwa
madarakani, ila wananchi karibia aslimia tisini na
sita wakamchagua Rahab na kumuhitaji awe raisi
wa kwanza mwanamke nchini Tanzania.
“Hii ni nafasi ya pekee watanzani walio kupatia,
waonyeshe kwamba wanawake tunaweza na sisi ni
zaidi ya wanaume wao”
Fetty alimuabia Rahab, ambaye hakuwa na
kipingamizi. Hapakuwa na mwananchi ambaye
alimkataa Rahab, kwa kura hizo za mauoni Rahab
akachukua kiti cha uraisi. Siku ya kuapishwa
ikapangwa, katika uwanja wa taifa wa mpira
wananchi wengi wa kila rika waliweza kuhudhuria
eneo hilo, ambapo waliweza kushuhudia jaji mkuu
akimuapisha Rahab Praygod kuwa ndio raisi mpya
wa Tanzania. Shangwe nderemo zilirindima nchi
nzima, natumaini ya mabadiliko kwa Watanzania,
yakaanza kufufuka tena.
***
“Jamani mimi ninaomba niondoke na kurudi kwetu
Japani”
Sa Yoo alizungumza huku akitazama jinsi Rahab
akiapishwa kupitia tv kubwa iliyopo hapo sebleni.
Eddy na Phidaya wote wakamgeukia na
kumtazama.
“Sa Yoo kwa nini usibaki hapa?”
“Nimepakumbuka nyumbani nahitaji kwenda
kuwaona ndugu zangu, jamaa zangu na watu
wengine”
“Kusema kweli kwa mimi kama mimi siwezi
kukuzuia, ila kikubwa nakushukuru kwa msaada
wako wote ulio weza kunipatia”
“Na mimi nitamsindikiza”
Shamsa alizungumza, huku akishuka kwenye ngazi
za gorofa
“Ehee na wewe unataka kutukimbia?”
“Nitarudi, ila ninamsindikiza rafiki yangu
nitakwenda kukaa naye huko siku mbili tatu kisha
ninarudi”
“Mimi sina maneno”
Eddy alizungumza huku akitabasamu, kutokana
baba amekubali basi Phidaya hakuwa na namna
yoyote ya kuwazuia mabinti hao walio ishi nao
kwenye shida na raha. Siku iliyo fuata Shamsa na
Sa Yoo wakaanza mikakati ya kutafuta hati za
kusafiria, kwa kutumia pesa ya kuwahongo watu
wanao shuhulika na utengenezaji wa hati za
kusafiria, kazi kwao ikawa ni rahisi. Siku hiyo hiyo
wakapata hati za kusafiria na kurudi nyumbani.
Walishangazwa sana kukuta gari nyingi nyumbani
kwa Eddy huku kukiwa na walinzi wengi wanao
onekana kumlinda raisi.
“Ina maana Rahab yupo hapa?”
“Nahisi”
Walinzi baada ya kuwahoji maswali wakawaruhusu
kuingia ndani. Wakamkuta Rahab akiwa amekaa
sebleni pamoja na Eddy. Wakamsalimia, kisha wao
wakamuulizia ni wapi Phiday alipo, wakaelezwa
yupo jikoni na wao wakaenda eneo hilo na
kuwaacha waendelee na mazungumzo yao.
“Eddy bila ya wewe mimi siwezi kuiongoza hii nchi
peke yangu”
“Sasa Rahab unataka mimi nifanye nini?”
“Nataka uwe msaidizi wangu, nataka nikuteue kuwa
makamu wa raisi”
Eddy akaka kimya na kushusha pumzi. Akafikiria
ombi hilo kwa sekunde kadhaa kisha akanyanyua
sura yake na kumtazama Rahab.
“Nimekubaliana na ombi lako muheshimiwa raisi”
Eddy alizungumza huku akitabasamu.
Wakanyanyuka kwa pamoja na kupeana mikono,
Rahab akaonekana kuwa na furaha sana kwa Eddy
kukubali.
“Ila vipi kidonda chako?”
“Kina endelea kukauka taratibu”
“Basi jiandae kesho uweze kufika ikulu nianze
kukutangaza”
“Sawa”
Wakapata chakula cha mchana kwa pamoja kisha
Rahab akaondoka na kumuacha Eddy akiwa na
furaha sana, pamoja na familia yake kwa ujumla.
Eddy akawaelezea Rahab, Sa Yoo na Shamsa ombi
alilo elezwa na Rahab, wote wakafurahi na
kumuomba aweze kuhakikisha kwamba anafanya
kazi yake kwa juhudi na kwa manufaa ya
watanzania wote kwa maana nafasi hiyo waliitafuta
kwa muda mrefu.
“Madam Mery yupo wapi?”
Sa Yoo aliuliza huku akimtazama Phidaya usoni.
“Amesha ondoka na kuelekea Mwanza nyumbani
kwake”
“Hata kutuaga?”
“Nyinyi si muliondoka na kumuacha amelala”
“Sisi tutaondoka kesho mchana saa saba kuelekea
Japani, tumesha weka booking ya ndege”
“Ahaa basi, kila mmoja nitampatia kiasi cha dola
milioni tano tano”
“Kweli Eddy?”
“Ndio”
“Wee Sa Yoo sasa hivi usimuite Eddy, muite
makamu wa raisi Eddy”
Phiday alizungumza kwa utani na wote wakacheka.
Eddy akaingia kwenye chumba chake cha siri,
akatoa kiasi kikubwa cha pesa ambacho ni sawa
na milioni kumi. Sa Yoo na Shamsa akawapatia
kila mtu kiasi sawa, kisha wakazipakiza pesa hizo
kwenye magari lao na kwenda nazo benki. Shamsa
akaziingiza kwenye akaunti yake na Sa Yoo
akaiziingiza kwenye akaunti yake ya benki ya
Japani yenye tawi lake nchini Tanzania. Wakarudi
nyumbani na kufanya maandalizi ya kila kitu.
Siku iliyo fwata alfajiri na mapema gari kutoka
ikuku zipatazo nne zikafika nyumani kwa Eddy.
Kiongozi wa msafara huo akamtaarifu Eddy juu ya
ujio wao hapo ni kuwachukua na kuwapeleka Ikulu,
ambapo shamra shamra za kumuapisha makamu
wa raisi zimeanza.
Eddy na Phidaya wakajiandaa vizuri sana, Eddy
akavalia suti nyeusi na shati jeupe pamoja na tai
ndogo nyeusi, huku Phidaya akivalia gauni refu
jeupe lenye mstari mmoja mkubwa kiunoni wenye
rangi nyeusi. Huku miguuni akiwa amevalia viatu
vyeusi ambavyo ni virefu kiasi. Wakaagana Sa Yoo
na Shamsa, kwa maana hawato weza kuhudhuria
sherehe hizo za kuapishwa kwa Eddy kutokana na
ndege yao kuondoka saa saba mchana.
Eddy na Phidaya wakaingia kwenye gari hizo na
kuondoka. Sa Yoo na Shamsa nao wakaingiza
mabegi yao kwenye gari lao.
“Hiyo laptop si uingize chumbani kwa Eddy?”
“Yaa ndio nataka niipeleke”
Shamsa akaipeleka laptop ya Eddy ndani kwake,
kisha akatoka, wakaondoka na Sa Yoo. Wakapitia
kwenye maduka ya simu wakanunua simu nzuri,
na kuelekea uwanja wa ndege. Kutokana muda wa
kuripoti kwa abiria uwanjani hapo ni saa moja
kabla ya ndege kuondoka, ikawalazimu kuti sheria
hiyo.
“Hapa si kuna wifi?”
Sa Yoo alimuuliza Shamsa, ambaye alimjibu kwa
kutingisha kichwa. Sa Yoo akaanza kuperuzi
kwenye mtandano kwa kutumia Internet iliyopo
hapo uwanja wa ndege. Muda wa andege yao
kuondoka, ukawadia. Wao nao waka ni miongoni
mwa abiria wlio ingia kwenye ndege hiyo ya
shirika la ndege la Air Ways. Wakaka kwenye siti
moja, huku Shamsa akiwa ameweka earphone zake
masikioni.
Abiria wakatangaziwa kufunga mikanda yao, ndege
inaondoka. Shamsa na Sa Yoo wakafanya hivyo,
taratibu ndege hiyo ikaanza kuondoka eneo hilo la
uwanje wa Mwalimu J. K Nyerere. Ndani ya dakika
kadhaa tayari ikawa imesha iacha ardhi ya
Tanzania.
“Shamsa muone Eddy”
Sa Yoo alizungumza na kuonyesha video inayo
onekana kwenye simu yake, mbayo hayo ni
matangazo ya moja kwa moja yanayo ruka kutoka
katika viwanja vya Ikulu. Shamsa akamtazama
Eddy aliye shika biblia akiapa juu ya kulitumikia
taifa la Tanzania kwa haki na uadilifu.
“Ohooo mwangu, tazama ulivyo pata baba mzuri
na anaye jituma. Mungu akubariki nikuzae kwa
amani?”
Shamsa alizungumza huku akilishika shika tumbo
lake kwa kiganja cha kulia.
“I….iii ina maana Shamsa una mimba ya Eddy?”
Sa Yoo alizungumza huku macho yakimtoa
“Ndio, nina mimba yake. Na wewe ndio mtu wa
kwanza kukuambia hili. Na ninapo kwenda sinto
rudi tena nchini Tanzania”
“Kwa nini sasa?”
“Endapo Phidaya atagundua kwamba nimebeba
mimba ya Eddy, basi visa na mikasa mipya
inaweza kuibuka, jambo ambalo silitaki kuliona
linatokea katika maisha ya mwangu wala katika
maisha ya mwanangu. Nitamlea mwangu kwa
kadtr ya uwezo wangu na atapata malezi bora.
Ninakuomba Sa Yoo unitunzie siri hii”
“Usijali rafiki yangu siwezi kuitoa siri hii na sinto
fungua kinywa changu kuweza kumueleza yoyote
juu ya hii siri”
Sa Yoo alizungumza na wote wakashikana mikono,
na safari ikazidi kusonga wakielekea nchini Japani,
wote wakiwa na furaha na amani katika maisha
yao kwani kila kitu cha ubaya kimesha fika tamati.
MWISHO