South African Airways kuanza tena Safar za Dar-JHB

South African Airways kuanza tena Safar za Dar-JHB

Mkuu ungeipanda kwanza ndio ukampinga hoja yake au kama umewahi ungetuelezea zaidi
Niamini mimi navyokwambia airline yoyote ile inayoendeahwa na mwafrika hamna kitu. Na usidhani kisa mie bodaboda sijawahi panda ndege...🤣🤣🤣🤣
 
Mateso gani jomba?
Mara nyingi hua kuondoka ni sa 9 ana 10 alfajiri, ufike Kenya ushuke, ufanyiwe security check, check in na usumbufu kama huo, baadae mkae hata masaa 4 ndio muondoke, Johannesburg mnafika sa 10 ama 11 jioni. The same na AA.

ATCL ni moja kwa moja na inaondoka sa 5 mnafika sa 7 ya kule.

Kwa sasa kwenda South Africa ni rahisi na starehe sana kwa ATCL.
 
ATCL ndio tamu zaidi.. Ndege Mpya ya Boeing 737-MAX 9

Kuondoka Dar: 11:00 am local
Kufika OR Tambo: 13:10 pm local
Hii route inalipa sana, japo kwa sababu zisizoeleweka tuliwaachia SA na sasa Airlink hivyo inabidi sasa tuanze kugombania abiria. Watu wetu wa marketing wanatakiwa waje na strategies (4p) zinazoendana na soko letu na sio kutegemea kukopy na kupaste.
Na huu utaratibu wa kukopy na kupaste vingine hata haviendani na mazingira yetu, sambamba na poor management of Income (wizi/maposho ya hovyo hovyo/ over employment nk) ndio vinafilisi mashirika ya ndege ya huku Africa
 
Mara nyingi hua kuondoka ni sa 9 ana 10 alfajiri, ufike Kenya ushuke, ufanyiwe security check, check in na usumbufu kama huo, baadae mkae hata masaa 4 ndio muondoke, Johannesburg mnafika sa 10 ama 11 jioni. The same na AA.

ATCL ni moja kwa moja na inaondoka sa 5 mnafika sa 7 ya kule.

Kwa sasa kwenda South Africa ni rahisi na starehe sana kwa ATCL.
Acha uongo. KQ unaondoka saa 9 usiku (kuna wakati mnapita Zanzibar then Nairobi unaweza ku-connect Nairobi saa 1 au saa 2 na ukafika Johannesburg saa 3 au saa 4 asubuhi.
** Kwa timings nadhani Malawian bado wanaongoza mnaondoka Dar saa 1 na dakika 40 asubuhi mnafika Johannesburg saa 5 asubuhi, misosi kama yote, huitaji kudamka kwenda airport. Same hata siku ya kurudi
 
Back
Top Bottom