Mshangazi mdogomdogo
Member
- Sep 23, 2024
- 64
- 43
Huku kwetu katika mitaa ya Manispaa ya Songea kuna wimbi la wizi wa Mita za Maji na kila aliyeibiwa anatakiwa kulipia Sh elfu 45 ili aweze kufungiwa mita nyingine.
Tunajiuliza huu ni mchezo ambao tunachezewa na baadhi ya watu wasiowaaminifu kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) au ni nini hasa kinachoendelea?
Ili Mita iweze kutumika inatakiwa kusajiliwa kwenye mamlaka husika, sasa hivi zinazoibwa zinaenda kutumika wapi? Hivi zina matumizi gani ya ziada mbali na idara ya maji? Au pia inabidi tuajiri Walinzi wa Mita?
Kila anayeripoti kuibiwa anapewa control number ili akalipie afungiwe mita nyingine, mnaweza kutufanya tuanze kuamini kuna watu wanacheza michezo michafu ili tulipe tena gharama za Mita.
Maji yenyewe baadhi ya mitaa ni shida tupu kwa wiki yanatoka mara moja wakati mwingine hadi wiki mbili tunakunywa maji ya visima ambayo usalama wake ni mdogo na hawasemi lolote kama kuna mgao au lah!
Wakati huohuo, Mita zinaibwa na Mamalaka inayohusika haijatoa mwongozo au neno kuhusu kinachondelea au kama kuna matumizi zaidi ya Mita zaidi ya hizi tunazozijua ili Wananchi wachukue tahadhari zaidi, wao wanaishia kugawa control namba tukalipe.
Pia soma ~ Afikishwa Mahakamani kwa wizi wa Mita za Maji - Kinondoni